Tuesday, 2 December 2014

KUSIFU NA KUABUDU : KUSUDI KUU NA LA KWANZA

             
                      SOMO:: KUSIFU NA KUABUDU
                          SEHEMU YA NNE
 KUSUDI KUU NA LA KWANZA
Katika sura iliyopita, tumegundua sababu inayomfanya Mungu kupenda sana sifa na ibada,; na sit u kupenda, bali pia kutaka sana sifa na ibada. Huko mbeleni, tutaona hata jinsi anavyoagiza kwamba, watu wote wamsifu. Hiyo sasa imegeuka kuwa amri! Kumsifu Bwana ni agizo! Tutaiangalia hiyo baad ya muda mchache. Lakini katika sura iliyopita, tumeshaelewa kwanini Mungu anahitaji sifa na kwanini anataka sifa na ukuzo. Tumegundua kwamba, mungu anataka hvyo vyote kwasababu yeye anaishi katika sifa na tukuzo za watu wake. Na tumeona jinsi Mungu alivyo very very serious kuhusu kupata hayo sifa na utukufu wake.

Yaani katika hili, Mungu yuko very serious, wala hatanii na wala hataki mchezo, kuhusu ibada. Nenda kamuulize mwanamke mmoja anaiwa Mikali,  mke wa mfalme Daudi, atakueleza ukali wa Mungu juu ya sifa na ibada. Hapo ndio utaelewa vizuri nini maana ya Mungu kutopenda utani kuhusu maswala haya ya kusifiwa na ibada. Maana Biblia inatuambia kwamba, Mfalme Daudi alipokuwa akimsifu Mungu na kucheza mbele za Mungu kwa muziki mzuri, mbele ya watu wengi, Daudi alicheza sana mpaka nguo zake zikaanguka, akabaki kifua wazi. Piga picha, Mfalme alibaki kifua wazi mbele ya kadamnasi, kwasababu ya kucheza nyimbo za kumsifu Mungu.


Basi Biblia inasema, mke wa Daudi alikuwa ghorofani, akiangalia ile ibada. Na moyoni mwake, alikereka sana kumwona mume wake anavyocheza na kuangusha mavazi yake ya kifalme, hata kubaki karibu na ‘uchi’ mbele za watu. Hicho kilimkera sana Mikali binti wa Sauli, ambaye alikuwa mke wa Mfalme Daudi. Na Biblia inasema kwamba, huyu mwanamke, alimdharau sana na kumdhihaki sana mume wake kwa kile kitendo cha kucheza kwa ajili ya Mungu, hata kuangusha nguo zake. Basi Mfalme Daudi alipomaliza ibada, akapanda ghorofani kwake ili kuoga, ndipo alipokutana na mke wake aliyekuja sura na kuvua midomo yake pembeni kwa dharau, huku akimpiga jicho mume wake, kuanzia juu mpaka chini, kwa dharau kubwa kabisa.



Biblia inasema, huyu mama alianza kumporomoshea mume wake maneno ya dharau na aibu, eti kwa vile alivyoonyesha kifua chake na mapaja yake mbele za watu, hasa mabinti waliokuwepo pale katika uwanja au katika ua wa hekalu. Biblia inasema, huyu mama alidiriki hata kumwita mume wake ‘baladhuli mkubwa’ yaani pumbavu, punguani au mshenzi. Duh! Kweli huyu mwanamke, alikereka. Lakini Biblia inasema kwamba, Mfalme Daudi, hakutetereka. Bali alimwambia mke wake kwamba, yeye ataendelea kumsifu Mungu hata kama watu hawatamwelewa.

Sasa, nimekusimulia hii habari ya kweli kabisa, ili tu kukuonyesha jinsi ambavyo, Mungu huwa hataki utani wala mzaha wala mchezo katika sifa zake. Yaani utaona jinsi ambavyo, Mungu hataki uzembe wala mchezo wa aina yoyote, inapokuja katika maswala ya kumsifu na kumtukuza yeye. Ninaomba uisome mwenyewe hii habari, ili upate picha yako binafsi kadri Mungu atakavyokusaidia kuielewa. Lakini katika habari hii, Mungu alikuwa mkali sana. Kwasababu kabla hata mazungumzo yao hayajaisha, Mungu alikuwa ameshuka kwa hasira. Maana Biblia ibasema kwamba, Mungu alimfunga tumbo Yule mama, tangu siku ile aliyoleta madharau yake kwa Daudi ambaye amekuwa chombo cha Bwana kiteule kwa sifa na ibada.

Biblia inasema kwamba, Mikali alikufa bila kupata mtoto, kwasababu ya kujaribu kumkatisha tama Daudi. Mimi najaribu kupiga picha ya kibinadamu, jinsi Mungu alimkaripia yule mama. Japo Biblia haisemi, lakini mimi nafikiri tu kibinadamu, jinsi Mungu alivyoteremka kwa hasira kali kabisa, akitaka kumzaba kibao huyu mwanamke, kwasababu ya maneno yake ya kukatisha tama na matusi yake dhidi ya chombo cha Mungu, yaani Daudi. Yaani ni kama vile, feni zote zimezimika, halafu kuna feni moja tu imabaki ndiyo inayofanya kazi, halafu anakuja mtu mmoja mjinga, asiyejua umuhimu wa feni, na kuanza kuichokonoa akitaka na yenyewe eti izimike kama zingine.

Hebu piga picha jinsi baba mwenye nyumba, anayeishi kwa hewa itokanayo na feni ile, jinsi ambavyo angesimama kutoka kwenye kochi alilokuwa amejipumzisha, na kumwendea mjinga huyu kwa hasira, akitaka kumzaba makofi, kwa jinsi anayochezea feni yake tukufu. Japo Biblia haisemi, lakini mimi najaribu kupiga tu picha ya kibinadamu, jinsi Mungu alivyomteremkia Mikali kwa hasira, akitaka kumzaba makofi, kwasababu ya maneno yake ya kedehi na matusi, kwa mtumishi wa Mungu Daudi; ambaye kwa wakati huo, ndiye alikuwa kama vile ndiye feni pekee ya Mungu, iliyokuwa inampa Mungu hewa saaaaafi wakati wa joto, hewa hiyo inaitwa, sifa na ibada. 

Mimi naamini, Mungu alisimamisha au alizuia kofi lake, sentimita chache tu kutoka shavuni kwa Mikali. Mimi naamin kwamba, Mungu alijua, nikimtandika mwanamke huyu kofi, lazima atakufa; na akifa, hapo nitakuwa nimeleta msiba na huzuni nyumbani kwa mwanangu Daudi. No! ngoja niache. Ndiyo maana Mungu alizuia kofi lake, sentimita chache tu kabla halijampata Mikali shavuni kwake. Ni kwasababu ya Daudi tu, rafiki wa Mungu, ndiyo maana Mungu alimsamehe Mikali. Yaani isingekuwa Daudi, mimi naamini kwamba, Mungu angemkaanga huyu mwanamke, kwa radi na moto wa mbinguni (Soma 2Wafalme 1:10-14, uone mfano wake).

Kwahiyo, mimi naamini kabisa ya kwamba, Mikali alipona kifo, ni kwasababu tu ya Daudi, rafiki wa Mungu. hakika asingekuwa mke wa Daudi, mimi naamini kwamba, Mungu angeshamkaanga kabla hata hajamaliza makebehi na matusi yake. Yaani nakwambia, kwa radi na moto wa mbinguni vingemteremkia huyu mama. Lakini Mungu akayatunza maisha yake, japo alikuja kwa hasira na nguvu, lakini Mungu aliyatunza maisha yake, kwasababu ya daudi rafiki yake. Lakini pamoja na hayo, Biblia iansema kwamba, Mungu hakumwacha hivi hivi tu bila angalau kumfinya kidogo. Lakini kabla Mungu hajageuza kurudi mbinguni, Biblia inasema kwamba, Mungu alimfinya huyu mwanamke tumbo lake.

Katika mawazo yangu, ninaweza kupiga picha Mungu akimwambia Mikali kwamba, ‘ni kwasababu tu ya rafiki yangu Daudi nimezuia mkono wangu usitue juu yako; lakini pamoja na hayo, siwe ondoka hapa nikuache hivi hivi bila alama yoyote. Kuishi, utaendelea kuishi, hiyo nimekupa; lakini kuanzia sasa (Mungu akamshika tumbo na kumfinya huku akiendelea kusema) … lakini kuanzia sasa, hautashika mimba tena! Mwone kwanza! Na usirudie kuwakebehi na kuwatukana watu ambao ni kama feni au air-condition kwangu. Tena utasa wako na uwe fundisho kwa wenzako wote wanowadharau wale ambao huwa wananisifu na kucheza mbele zangu ibadani. Nenda ukawape salamu zangu.’ Ndipo Mungu akaondoka zake.

Jamani, ngoja niwe wazi mapema, kabla haujagundua mwenyewe. Ukienda kuisoma hii habari katika Biblia, hautaikuta kama hivi ninavyosimulia. Mimi nimetumia tu lugha nyingi ya kimawazo inayofanana na uhalisia wa maisha ya kibinadamu, jinsi ambavyo sisi kama binadamu, huwa tunakarika na kuadhibu watu. Ila ukienda kuisoma mwenyewe, utaelewa jinsi mawazo yangu ambavyo hayako mbali na vile ilivyoelezewa katika Biblia. Mimi ni mwalimu, kwahiyo ninajaribu tu kukutengenezea picha ya uhalisia wa dhana au concepts hizi ninazokufundisha na ninazokusomea katika maandiko matakatifu. Kwahiyo, usiache kwenda kufungua Biblia mwenyewe. Habari hii imeandikwa katika Kitabu cha Pili cha Samweli, Sura ya Sita yote. Japo nimekuchanganyia lugha ya picha, na nadhani imekusaidi kuelewa jinsi ambavyo Mungu ni mkali sana kuhusu sifa zake. Kama tulivyoona kule mwanzoni kwamba, Mungu yuko very very serious, kuhusu sifa na ibada. Yaani hataki utani wala mchezo. Na tumesoma jinsi Mungu alivyokuwa mkali kwa Mikali mke wa Daudi, na jinsi alivyomfurikia, yaani jinsi alivyomjia kwa nguvu na kwa jazba na kwa hasira kali kama mafuriko. Kwahiyo, kuhusu sifa, Mungu ni mkali sana. Hii ni kwasababu, Mungu anapenda sana sifa na anataka sana sifa na tukuzo.


Pengine wewe umeona mtu kufungwa tumbo na Mungu kwasababu ya kebehi juu ya ibada, ni kitu kikubwa sana. Lakini ukisoma kuanzia mstari wa 1 hadi wa11, wa kitabu hiki (2 Samweli 1:1-11), tunaona jinsi ambavyo Mungu alikuwa tayari hata kuuwa mtu, eti tu kwasababu, taratibu zake za ibada, hazikufuatawa. Kufunga tumbo ni kitu kidogo sana ukilinganisha na kuuwawa kwa mtu. Mungu ni mkali sana inapofika katika maswala ya kusifiwa na kuabudiwa. Biblia inasema kwamba, Daudi alilibeba sanduku la Bwana juu ya gari la kuvutwa na ngómbe, badala ya kubebwa na makuhani. Biblia inasema, Mungu alimwagiza Musa kusema kwamba, sanduku hilo la agano, litabebwa na makuhani na walawi peke yao.
SOMO LITAENDELEA


No comments:

Post a Comment