SOMO:SIFA NA KUABUDUDU
sehemu ya tatu
SIFA NA IBADA YA MBINGUNI
Katika Sehemu ya pili , tumejifunza maana ya neno
la kiingereza la habitat au habitation, jinsi linavyoweza
kubadilisha uelewa wetu juu ya sifa na ibada kwa Mungu. tumejifunza kwamba, Habitat – is a special place where living things
are found naturally; yaani, habitat
ni mahali maalum, viumbe wa asili
hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu. Kwahiyo
Biblia inaposema katika kitabu cha Zaburi 22:3 kwamba, Mungu ana-inhabit
au ameweka kiti chake katika mazingira yaliyo na sifa za Israel (au sifa za
watu wake), hii ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za
watu wake.
Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe
wake tujue kwamba, hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama
nilivyosema hapo juu kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na
kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya
kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Tumejifunza kwamba,
kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo
kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio maana, hata kule mbinguni, tutakapofika,
hatutafanya kitu kingine zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana.
Hii inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha
thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi
katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mungu
ana-inhabit
sifa za watu wake, kama Zaburi
22:3 inavyosema. Sasa katika sura hii, nimeazimu kukuonyesha jinsi Mungu alivyo
serious
kuhusu ksifiwa na kuabudiwa. Serious ni neno la kiingereza lenye maana ya kumaanisha
sana. Mtu aliye serious, ni mtu asiyetaka utani,
uzembe wa mchezo-mchezo katika mambo yake. Na vivyo hivyo, Mungu wetu
yuko very serious katika swala la
sifa zake na ibada yake, yaani hana utani, wala hataki uzembe wala mchezo
mchezo inapokuja katika maswala ya kumsifu na kumtukuza, yuko very very serious. Katika sura hii,
nataka nikuonyeshe jinsi ambavyo Mungu anaheshimu sana sifa. Hebu twende
mbinguni kidogo, ili nikuonyeshe hii kitu ninasema.
Kwa Mfano wa ibada ya Mbinguni;
Biblia inaeleza kwamba, kule mbinguni, Mungu
amejizugushia maelfu na maelfu ya malaika wengi, ambao kazi yao pekee, ni
kumsifu na kumwabudu Mungu, usiku na mchana. Ngoja tusome wote;
Ufunuo 4:9-11, Biblia inasema kwamba, mbinguni kuna viumbe fulani wane, wenye uhai;
“Na
hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na
ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu mwenyezi, aliyekuwako na
aliyeko na atakayekuja. Na hao wenye uhai, wanapompa yeye aketiye juu ya
kiti cha enzi utukufu, na heshima, na
shukurani, yeye aliye hai hata milele na milele, ndipo hao wazee ishirini
na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele
na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu,
kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu
vyote, na kwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
(Ufu 4:9-11)
Katika Ufunuo
5:11-14, Utaona Biblia inasema kwamba,
“Kisha nikaona, nikasikia sauti ya malaika
wengi pande zote za kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa, elfu
kumi mara kumi elfu, na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili mwana kondoo aliyechinjwa,
kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya bahari na vitu
vyote vilivyoko ndani yake, nilivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza, una yeye aketiye juu ya kiti cha
enzi, na yeye mwana kondoo, hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne
wakasema, Amina. Na wale wazee
wakaanguka wakasujudu.”
(Ufu
5:11-14)
Mpendwa, hivi ndivyo ambavyo Mungu anathamini
sana kusifiwa na kuabudiwa au ibada. Hivi ndivyo ambavyo
Mungu anaheshimu sana kusifiwa na
kuabudiwa au ibada. Na
ndio maana anataka kusifiwa au anaagiza kusifiwa au anaamuru
apate kusifiwa. Jamani, Mungu anathamini sana kusifiwa na kuabudiwa; hawa
malaika, ni maelfu mengi ya malaika, wanamsifu na kumwabudu Mungu kila siku,
tena kwa masaa 24 mfululizo, mchana na usiku, bila kupumzika. Ni maelfu na maelfu
ya malaika wengi sana, Mungu amejiwekea huko juu mbinguni, wamekizunguka kiti
chake cha enzi, usiku na mchana, wanamwimbia Mungu, wanamsifu Mungu,
wanamwabudu mungu, wanamsujudia Mungu na kuanguka mbele zake, ambaye ni muumba
wao.
Hawa malaika jamani, ni wengi sana. Hapo mbele
nitakuonyesha msatri mmoja unaoeleza hesabu ya kwamba wapo wangapi. Ni hesabu
ya kawaida kabisa, unaweza ukajaribu kuipiga ili uweze kujua, hii kwaya tu ya
mbinguni, ina malaika waimbaji wangapi; lakini ni malaika wengi sana. Na Biblia
inasema kwamba, hawa malaika wapo wa kabila mbili kubwa, wanaitwa Makerubi
na Maserafi.
Hawa malaika wa kabila hizi mbili, hawana kazi nyingine yoyote ya kufanya, zaidi
ya kumsifu na kumwabudu Mungu. Hawa malaika, hawana kazi ya kufua, wala kupika;
hawana kazi ya kulinda au kupeleka habari popote. Biblia inasema kwamba, hawaondoki
mbele za Mungu, bali kazi yao pekee ni moja tu, yaani kumsifu na kumwabudu Mungu.
Hiyo inatuonyesha kwamba, Mungu yuko ‘very
serious’ kuhusu kusifiwa na kuabudiwa, wala hataki mchezo kuhusu
kusifiwa na kuabudiwa, kwasabau kusifiwa na kuabudiwa ndiyo biashara muhimu
zaidi kwake kuliko kitu kingine chochote. Hebu tusome maandiko matakatifu ya Neno
la Mungu kwanza, ili nikuonyeshe hiki ninachosema hapa. Nataka uone mwenyewe jinsi
Biblia inavyosema kuhusu sifa na ibada ya mbinguni. Hii itakuonyesha jinsi ambavyo
Mungu yuko ‘very very serious’ kuhusu sifa na ibada za viumbe na watu wake.
Jamani, Mungu anathamini sana kusifiwa na
kuabudiwa; hawa malaika elfu nyingi, wanamsifu na kumwabudu Mungu kila siku,
tena kwa masaa 24 mfululizo, mchana na usiku, bila kupumzika. Ni maelfu na
maelfu ya malaika wengi sana, wamewekwa na Mungu huko juu mbinguni, kukizunguka
kiti chake cha enzi. Yaani, nikiongea kwa lugha ya kibinadamu, sifa kwa Mungu
ni kama maji kwa samaki. Sifa kwa Mungu ni kama ardhi kwa mimea. Sifa kwa Mungu
ni kama hewa ‘oxygen’ kwa binadamu. Mungu anaheshimu sana sifa kuliko kitu
kingine chochote. Ni kama wewe unavyoheshimu oxygen au kama samaki
anavyothamini maji.
Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya
Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio
maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya
kumsifu na kumwabudu Bwana; hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha
thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi
katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mungu
ana-inhabit
sifa za watu wake, kama Zaburi
22:3 inavyosema. Hiyo ndiyo maana ya habitation,
a special place for life.
Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit
sifa za Israel, ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za
watu wake. Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba,
hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu
kwamba, katika vitu vyote, hakuna
kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa.
Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio
hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote.
Na ndio maana huko mbinguni, Mungu amejizungushia
malaika maelfu elfu, Biblia inasema kwamba, ile hesabu ya tu, ya kwaya hii ya
mbinguni, elfu kumi, mara elfu kumi, mara elfu, mara elfu. Ni hesabu inayoweza
kupigika kabisa. Jaribu; ukishindwa tumia kikokotoo au ‘calculator’. Natamani uone jinsi ambavyo Mungu
hataki utani inapofika katika maswala ya kusifu na kuabudu. Jaribu kupiga hii
hesabu ya idadi yao, ili tuweze kujua, hii kwaya ya mbinguni ina waimbaji
wangapi. Hapo utaelewa jinsi Mungu wetu alivyo very serious kuhusu sifa na
ibada.
Hesabu ya mbinguni
Kama umefanya hii hesabu kwa usahihi, utakuwa
umepata namba yenye masifuri 14. Unajua kuna wengine wenu mikimbia hesabu
darasani, basi ngoja nikusaidie, tufanye wote. Biblia inasema kwamba, ile
hesabu ya hawa malaika tu, idadi ya kwaya hii ya mbinguni, ni elfu kumi, mara
elfu kumi, mara elfu, mara elfu. Hebu tujaribu kufanya Hisabati kidogo, tuipige
hii hesabu tuone idadi ya kwaya ya mbinguni, ili uweze kuona jinsi Mungu alivyo serious na ibada. Usiogope, ni hesabu
rahisi tu. Haya, twende darasani kidogo. Biblia inasema kwamba, ile hesabu ya
hawa malaika tu, idadi ya kwaya hii ya mbinguni, ni elfu kumi, mara elfu kumi,
mara elfu, mara elfu. Yaani hivi;
10,000 x 10,000 x 1,000
x 1,000 =
100,000,000,000,000.
Kwa wale mliokimbia hesabu darasani, ukitaka
kuifanya hii hesabu ya kuzidisha kwa njia rahisi nay a mkato, unafanya hivi; kwa
namba yenye masifuri mengi hivi, wewe yahesabu tu masifuri yooote ujue yako
mangapi, halafu, yaweke pembeni. Kwahiyo, katika
10,000
x 10,000 x
1,000 x 1,000
Wewe yakusanye masifuri yooote haya, yako 14,
kisha uyaweke pembeni, tutayarudishia baadaye. Kwahiyo, ukiondoa masifuri yote
haya kutoka katika hesbu yetu, utakuwa umebekiwa na namba zinazoonekana hivi,
1 x
1 x 1
x 1 =
1
Kwa hiyo, ukizidisha moja na moja, jibu letu ni
moja (1). Sasa, tuchukue yake
masifuri yetu, tuliyoyaondoa, na tuyapachike au yarudishie, na kuyabandika yote,
katika jibu tulilopata. Kumbuka kwamba, tuliondoa masifuri 14. Kwahiyo,
tukiyarudisha masifuri yote, na kuyabandika katika hili jibu tulilolipata, basi
jawabu letu litakuwa kama hivi.
= 100,000,000,000,000.
Kwahiyo, kama na wewe iliifanya hesabu hii kwa
usahihi, ni lazima utakuwa umepata namba yenye masifuri 14. Katika hesabu, hiyo
namba inaitwa Trillioni 100. Trillioni
1 ni sawa na Billioni 1,000. Kwahiyo Trillioni 100 ni mafungu 100 yenye Billioni elfu moja moja,
kila moja. Hao ni malaika wengi sana jamani. Na Biblia inasema kwamba, hawa
malaika Trillioni 100, ni hesabu ya malaika waimbani tu. Hiyo ndiyo idadi ya kwaya
ya mbinguni ndugu yangu. Halafu wewe tunakwambia uje kumsifu Mungu, bado
unaringa au unajifanya bize (busy). Mungu ana watu bwana. Kusifu ni kwa faida
yako pia mpendwa, ohooo! (Nitakufundisha hii baadaye).
Kwahiyo hawa ndio malaika walizungushwa katika kiti cha enzi cha
Mungu, ili kumsifu yeye, usiku na mchana, wako Trillion 100. Na kwa taarifa
yako, hapo hatujawahesabu na kuwajumkisha wale wa wizara zile nyingine mbili;
wale malaika wa wizara ya ulinzi na
usalama, malaika wanajeshi, au malaika wa vita, walio chini ya uongozi wa
Malika Mkuu Mikaeli; hatujawahesabu hao; na pia watujawahesabu wale malaika wa
wizara ya habari na mawasiliano, wale
wanaosambaza jumbe za Mungu, chini ya usimamizi wa Malaika Gabrieli; na hao pia
hatujawahesabu wala kuwajumlisha katika idadi hii ya Trillioni 100.
Kwahiyo, hawa malaika Trillion 100, ni malaika waimbaji tu; hawa
ndio walio katika wizara ya kusifu na
kuabudu, wizara ambayo zamani, ilikuwa chini ya Malaika
Lusifa, kabla hajasababisha ule uasi uliotokea mbinguni (kwa sasa, huyu Lusifa,
sasa ndiye ibilisi shetani). Lakini zamani, kabla hajaangushwa na kutupwa huku chini duniani, alikuwa
kiongozi wa hii kwaya ya mbinguni. Usome vizuri kitabu cha Ufunuo 12:3-4, 7-12, 27 na Isaya 14:10-16 na Ezekieli 28:11-19 utaiona
hiyo. Lakini nadhani hebu tusichanganye masomo; naahidi nitakufundisha vizuri
zaidi kipengele hiki, katika kitabu changu kingine cha Vita vya kiroho. Lakini kwa
sasa, hebu turudi katika somo letu.
Kwahiyo, hawa malaika Trillioni 100, ni wale ambao ni waimbaji tu; masaa
yote 24, hawa hawaondoki mbele za kiti cha enzi; kazi yao moja na ya pekee ni
kumsifu na kumwabudu Mungu tu. Hawa malaika, hawana kazi nyingine isipokuwa
kumsifu na kumwabudu Mungu; hawana kazi ya kulima, wala kuvuna; hawana kazi ya kufua
wala kufagia; hawana kazi ya kulinda pamoja na malaika walinzi wa Mungu walio
chini ya malaika Mkuu Mikaeli, wala kazi ya kupeleka barua au ujumbe popote,
pamoja na malaika walio chini ya Malaika Gabrieli, hapana! Kazi yao ya pekee ni
moja tu, kumsifu, kumtukuza na kumwabudu
Mungu tu!
Vitu vyote vimeumbwa, kwa
mahitaji na matakwa ya Mungu.
Biblia inasema kwamba, usiku na mchana, malaika hawa huwa mbele za Mungu
tu, wakikizunguka kile kiti cha enzi, na kumsifu na kumwabudu Mungu; tena huanguka
na kuinuka, huinama na kusujudu, wakisema “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, wewe ndiwe Mungu, uliyeviumba vitu vyote, na
kwasababu ya ‘mapenzi’ yako, vitu vyote vilikuwako, navyo vikaumbwa.” (Ufunuo
4:11). Maana ya sentensi hii
ya mwisho ni kwamba, ‘vitu vyote vimeumbwa na Mungu ili kutimiza ‘mapenzi’
ya Mungu.’ Na kwa shule tuliyojifunza katika sura zilizopita, tumejua sasa ya
kwamba, ‘mapenzi’ ya Mungu ya kwanza ni kusifiwa na
kuabudiwa.
Tafsiri zingine za Biblia, zinasema kwamba, hayo ‘mapenzi’ ya Mungu, si tu
kwamba ni ile nia ya Mungu au ni ule mpango wa Mungu, bali pia, hili neno
‘mapenzi’
ya Mungu, pia limemaanisha, ‘mahitaji’ ya Mungu au ‘matakwa’
ya Mungu. Na kwa shule tuliyojifunza katika sura zilizopita, tumejua sasa ya
kwamba, ‘mahitaji’ ya Mungu ya kwanza ni kusifiwa na
kuabudiwa. Kwahiyo, lugha nyingine ya neno ‘mapenzi’ ni ‘mahitaji’
au ‘matakwa’.
Kwahiyo, kwa uelewa huo, tukiuweka huo msamiati mpya katika ule mstari wa
Ufunuo 4:11, tunaweza kusema kwamba;
Wale malaika trillion 100, wanazunguka na kumsujudu Mungu wakisema “Mtakatifu,
Mtakatifu, Mtakatifu, wewe ndiwe
Mungu, uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya ‘matakwa’ yako vitu vyote
vilikuwako, navyo vikaumbwa.’ Au pia, inaweza kusomeka kwamba ‘… kwasababu
ya ‘mahitaji’ yako vitu vyote vilikuwako, navyo vikaumbwa.” (Ufunuo
4:11). Na kwa shule tuliyoipitia, sas tumeshajua, tena kwa hakika ya
kwamba, ‘mahitaji’ ya Mungu ya kwanza ni kusifiwa na kuabudiwa; au kwa lugha nyingine ni tunaweza
kusema kwamba, ‘matakwa’ ya Mungu ya kwanza ni kisifiwa na kuabudiwa.
Feni na Air-Condition za Mungu
Hapo juu tulisema kwamba, kama Mungu angekuwa
mwanadamu, anayeishi katika nchi yenye joto kali, kwa mfano la kule uarabuni, basi
sifa
na kuabudu ndivyo vingekuwa hewa yake. Sasa basi, hebu piga picha, katika
mazingira kama hayo, kama Mungu angekuwa mwanadamu, ni lazima angehitaji feni
za kumpulizia au air-condition ya kumpoozea joto na kumtengenezea hewa safi. Na
kama ingekuwa ndio hivyo, sifa na kuabudu ndivyo vingekuwa hewa ya Mungu. Na
kama ndivyo, basi wale malaika waliomzunguka Mungu, ndio wangekuwa vyombo
maalum vya kumtengenezea Mungu, ile hewa anayoihitaji, yaani sifa na ibada!
Kwa uelewa huu, basi hao malaika Trillion 100,
ndio wangekuwa hizo feni za Mungu za kumpulizia ili apate upepo mzuri wenye ubaridi
ili kumpooza na joto kali la duniani. Au hao malaika trillion 100, ndio
wangekuwa air-condition za Mungu, za kumpulizia hewa saaaaaafi ya ubaridi. Kama mwanadamu anavyoishi kwenye hewa safi,
ndivyo ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Halleluyah! Sasa piga picha, mtu aliyejizungushia feni
triliioni 100 anajaribu kukuonyesha nini? Fikiri tu mwenyewe. Kweli, mtu
aliyejitundikia air-condition trillion 100 kwenye sebule au ukumbi wake,
hivi mtu huyo anajaribu kukwambia nini? Umeweza kukisia, mtu kama huyu
anajaribu kutuambia nini sisi tunaomtazama?
Mimi nadhani, mtu wa namna hiyo anajaribu
kukwambia kwamba, yuko very very serious kuhusu kupata hiyo
hewa yake; yaani hataki mchezo. Basi na kwa Mungu ni hivyo hivyo; Jamani, ndivyo
ambavyo Mungu wetu alivyo; Mungu yuko very very serious kuhusu kusifiwa na kuabudiwa, kama
maandiko tuliyoyasoma, yalivyotuonyesha kwamba, Mungu wetu anakaa au anaishi
katika mazingira ya sifa na ibada. Na hataki utani wala michezo ya hovyo hovyo, juu ya ibada yake. Mimi
nadhani ndicho Mungu anachojaribu kutuonyesha na kutuambia; kwamba yuko serious!
Mabomba ya Maji ya Mungu
Nikupe mfano mwingine; piga picha, kama Mungu
angekuwa samaki, anayeishi kwenye Bwawa la maji, ni lazima angehitaji mabomba
ya kuingiza maji katika bwawa lake. Na kama ingekuwa ndio hivyo, basi hao
malaika trillion 100, ndio ambao wangekuwa ni mabomba ya kumuingizia
maji katika bwawa lake ili apate maji. Kama samaki anavyoishi kwenye maji,
ndivyo ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Halleluyah!
Sasa, piga picha, mtu aliyewekea mabomba
trillioni 100, hivi unadhani
anajaribu kukwambia nini? Mimi nadhani, mtu wa namna hiyo anajaribu kukwambia
kwamba, yuko very very serious kuhusu kupata hayo maji yake; yaani hataki
mchezo. Basi na kwa Mungu ni hivyo hivyo; Jamani, ndivyo ambavyo Mungu wetu
alivyo; Mungu yuko very very serious kuhusu kusifiwa
na kuabudiwa.
Sasa, kwa mfano huo huo, ni muhimu uelewe kwamba,
viumbe wote sisi, tumeumbwa na Mungu duniani, ili tuwe kwake kama vyombo
maalum vya kumsifu na kumwabudu yeye Mungu. Kusifu na kuabudu kunatupa sababu na maana ya sisi viumbe
kuishi. Na ndio maana Daudi alipoelewa
ufunuo huu, akajiambia mwenyewe, kusema “… Ee nafsi yangu, umsifu Bwana”. Halafu
katika mstari wa pili, Daudi anatuambia na sisi wengine kwamba;
“Nitamsifu
Bwana, muda ninaoishi, nitamwimbia
Mungu wangu ningali ni hai” (Zaburi 146:
1-2).”
Ufunuo wa Mfalme Daudi.
Na ndio maana, Roho Mtakatifu alipompa Mfalme
Daudi ufunuo huu; Kwamba viumbe wote ni vyombo maalum vilivyoumbwa kumsifu na
kumwabudu Mungu, Daudi akaandika tena waraka maalum au wimbo maalum kwa viumbe
wote, ili kuwaamuru na kuwakumbusha, watenge muda maalum wa kumsifu na
kumwabudu Mungu. Mfalme Daudi akaandika waraka huo au wimbo huo katika Zaburi 148.
No comments:
Post a Comment