PIGO KWA TASNIA YA MUZIKI WA INJILI TZ...
Tasnia ya muziki wa injili leo imempoteza mwimbaji wake nyota na
mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti Mtoni almaarufu kama Lulu choir kutoka kanisa la
Kilutheri, George Bonge Njabili aliyefariki dunia mchana wa leo katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
George enzi za uhai wake
Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo
November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema, marehemu George
alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam wakati
akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda mrefu na mwimbaji huyo
kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.
Marehemu George atakumbukwa kwa huduma yake njema ya uimbaji
kupitia kwaya ya Lulu ambako aliongoza nyimbo mbalimbali ukiwemo Around the
corner Jesus coming, Tazameni Upendo huu, Haleluya na nyingine nyingi huku
akiipamba vyema DVD ya kwanza ya kwaya hiyo iliyobebwa na wimbo wa Lulu. Ni
takribani miaka mitatu sasa toka aliyekuwa mwalimu mkuu wa kwaya ya Lulu
kufariki dunia, kifo ambacho wengi walidhani aliyefariki ni George kiasi kwamba
taarifa za kifo chake hii leo kimepokelewa kwa tofauti hasa baadhi ya watu
wakidhani alishafariki siku nyingi.
Marehemu George Njabili almaarufu kama George Bonge akiwa na mkewe enzi za uhai wake |
No comments:
Post a Comment