SEHEMU YA PILI
KWANINI MUNGU ANATAKA KUSIFIWA
Katika sura iliyopita, tumejifunza kwamba, Mungu
anaheshi sana sifa na ibada, na Mungu anataka sana kusifiwa na kuabudiwa. Na kama
vile Mfalme Daudi alivyoandika katika Zaburi 22:3 kwamba; “Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya
sifa za Israeli.” Hivyo, tumeona kwamba, Mungu ametuumba sisi na viumbe
wote, ili tutimize mapenzi yake
au matakwa yake au mahitaji yake, amabyo ni kusifiwa
na kuabudiwa.
Ndio maana Mungu anataka sana kusifiwa na kuabudiwa; yaani sifa na ibada kwa
Mungu, ni vitu vya thamani sana na vya umuhimu sana. Kwakweli, Mungu anaheshimu
sana sifa na ibada
.
Na tumejifunza kwa maisha ya Mfalme Daudi, jinsi
alivyolielewa kusudi hili la Mungu juu ya maisha yake au juu ya maisha yetu sis
wanadamu, kwamba tumeumbwa tuwe kama chombo cha kumsifu na kumwabudu Mungu siku
zake zote za maisha yake, maadam tunaishi. Hivyo basi katika sura hii, kama
nilivyokuahidi, hebu tuchimbe zaidi na tutafute kujua, kwanini Mungu anataka
sana kusifiwa. Katika sura hii, nataka tujifunze kwa undani zaidi, sababu
inayomfanya Mungu kupenda sana sifa, na hata kuumba viumbe wote ili wawe au ili
tuwe, vyombo vyake viteule, vya kumsifu na kumtukuza yeye. Hebu tujifunze
kwanini Mungu anaheshimu sana sifa.
Mungu anaishi katika sifa na
ibada viumbe na watu wake.
Uuumm … Si watu wengi wanaojua kwanini Mungu
anaheshimu sana sifa na kwanini Mungu anapenda sana ibada na sifa. Na
hivyo basi, si watu wengi wanaojua kwanini Mungu anataka sana kutukuzwa na tena
ameagiza kwamba asifiwe. Kwahiyo, katika kipengele hiki, nataka nikupe ufunuo
huo, ili nawe upate kujua, kwanini Mungu aliumba viumbe vyote na alituumba na
sisi wanadamu. Nataka na wewe upate ufunuo huu, ili upate kujua sababu
inayomfanya Mungu kuheshimu sana sifa na ibada. Katika kipengele hiki, utaelewa jinsi ambavyo Mungu anaishi katika sifa
za watu wake, yaani jinsi Mungu anavyoishi katika sifa na ibada. Hebu
tuanzie katika mistari hii, ambayo tumekwisha kuisoma mara kadhaa; Zaburi 22:3 inayosema kwamba;
“Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za
Israeli.”
(Zaburi 22:3)
Ngoja nianze kwa kusema kwamba, Mungu alitumia
mstari huu mmoja, kufungua sana macho ya moyo wangu, ili kunipa ufunuo huu
ambao ulibadilisha maisha yangu, kama ulivyobadilisha maisha ya Daudi bin Yese. Mstari huu ulileta ufunuo
mkubwa sana maishani mwangu, hata kuweza kuelewa jinsi Mungu anavyoheshimu sana
sifa na ibada. Niliweza kuelewa kwanini Mungu anapenda sana sifa na ibada. Nami
nataka na wewe pia uweze kuelewa jinsi Mungu anavyoheshimu sana sifa na ibada,
hata akatuumba na sisi ili tumpe sifa na utukufu. Ni maombi yangu kwamba, Mungu
akupe ufunuo huu, afungue macho ya moyo wako pia, ili na wewe uweze kuelewa
umuhimu wa sifa na ibada kwa Mungu, na ili na wewe uanze kuwa chombo cha sifa
na ibada kwa Mungu. na Mungu akujalie kufanya wito huu kwa uaminifu na bidii.
Maandiko haya katika Zaburi 22:3 yanasema kwamba, ‘Nawe
U Mtakatifu, Uketiye juu ya
sifa za Israeli (au kwa maana nyingine, ukaaye katika sifa za watu wako).’
Angalia tena vizuri, hilo neno ‘uketiye’.
Hilo neno kuketi, halimaanishi tu kukaa, bali linamaanisha
pia kuishi.
Ni neno la kawaida kabisa tulilolizoea katika lugha za kila siku. Kwa mfano, mtu
akiulizwa kuhusu mahali gani anapoishi, mara nyingi huwa tunasema ‘mimi ninakaa
mtaa fulani’ au ‘mimi ninakaa kitongoji fulani’. Na
hapo huwa tunamaanisha kwamba, tunaishi katika mtaa huo au ‘tunaishi’
katika kitongoji hicho au eneo hilo, na sio kwamba huo mtaa unaokaa,
huwa unaukalia kama vile unavyokalia kiti
chako; haapanaaa! Bali huwa tunamaanisha kwamba, huko uliposema unapokaa ndipo mahali
pako au mahali petu pa makazi au maisha; yaani ndipo
mahali wewe unapoishi.
Kwa mfano; Mtu
anaposema mimi ninakaa Kinondoni, au Temeke au Ilala; au mtu anaposema kwamba ‘mimi
nakaa Ubungo au Kariakoo,’ huwa tunajua
kabisa ya kwamba, mtu huyo hamaanishi kwamba, Kinondoni ni kiti chake au Ubungo
ni kiti chake au huo mtaa alioutaja ni kiti chake cha kukalia; haapanaaa!
Bali mtu akisema hivyo, sisi wote tunaelewa, huwa anamaanisha kwamba,
yeye anaishi
Ubungo au anaishi Kinondoni au anaishi Mbagala au
anaishi
katika huo mtaa alioutaja. Kwa uelewa huu, huu mstari tuliousoma katika Zaburi
22:3 kwamba Mungu anaketi katika sifa za watu wake,
haumaanishi tu kwamba Mungu ameweka kiti chake katika sifa za watu wake, kwa
kuziheshimu sana; bali pia mstari huu unaweza kumaanisha kwamba, Mungu anaishi
katika sifa za watu wake.
Kwa dhana hii au kwa uelewa huu, utaanza kuiona
sifa na ibada kitofauti. Naamini utaiona sifa na ibada kuwa ni sehemu muhimu
sana ya maisha yako na utaiheshimu sana kama vile Mungu anavyoiheshi; kwani
Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Na hii ndio sababu kubwa inayomfanya
Mungu kupenda sana sifa za watu wake na si hivyo tu, bali hata kutaka sana
kufanyiwa sifa na ibada na watu wake. Na ndio maana Mungu anatuamuru sisi wote
tulio viumbe wake, kumsifu na kumwabudu yeye kila siku ya maisha yetu; na hii
si mpaka iwe siku maalumu ya ibada kama vile Jumapili, No! Bali ni kila siku ya
maisha yetu. Narudia tena kusema kwamba, kila siku ya maisha yetu, ni siku ya
ibada, na inatakiwa tuichukulie hivyo.
Ni muhimu sana mtu wa Mungu uelewe hilo na upange
vizuri ratiba zako kwa kila siku ili uweze kuishi katika kumpendeza Mungu.
Usingoje kumwabudu na kumsifu Mungu siku ya Jumapili tu au katika siku maalumu
iliyopangwa na kanisa lako ili kukutanika ibadani, haapanaaa! Mungu anataka tuwe tunakutana naye kila siku katika sifa na ibada. Kwahiyo, jenga nidhamu ya kukutana na Mungu kwa
sifa na ibada, katika nyumba yako au katika chumba chako au
katika mahali popote patulivu, utakapopachagua wewe. Mungu wet anataka tuwe na nidhamu ya kukutana naye ‘kila siku’ katika sifa na ibada. Kama
ulikuwa hujui, sasa umejua. Ibada kwa Mungu inatakiwa iwe kiiiiila siku.
Kwahiyo, kama nilivyosema hapo juu, ni muhimu sana
mtu wa Mungu uelewe hilo na upange vizuri ratiba zako kwa kila siku ili uweze
kuishi katika kumpendeza Mungu. usimalize siku nzima pasipo kupata muda wa
kukaa mbele za Mungu na kusema naye juu ya uzuri wake na utukufu wake. Panga
ratiba zako vizuri, na uuheshimu muda wa kukaa mbele za Mungu. kama unataka
Mungu akuheshimu mtaani au duniani, hebu na wewe mwonyeshe kwamba, unamheshimu
kwa muda wako. Narudia tena kusema, hebu usingoje kumwabudu na kumsifu Mungu,
siku ya Jumapili tu au katika siku maalumu iliyopangwa na kanisa lako ili
kukutanika ibadani, haapanaaa! Fahamu kwamba, Mungu
anataka tuwe tunakutana naye ‘kila siku’ katika sifa na ibada. Habari
ndio hiyo!
Na Mfalme Daudi alilielewa kusudi hili la Mungu
juu ya maisha yake, kwamba yeye ameumbwa awe kama chombo cha kumsifu na
kumwabudu Mungu siku zake zote za
maisha yake, maadam tu, anaishi.
Na Daudi alilitimiza kusudi hili vizuri. Na ndio maana anaandika kwamba; Halleluyah!
Ee nafsi yangu, umsifu Bwana. 2 (Nami Daudi) Nitamsifu Bwana, muda
ninaoishi, nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.” (Zaburi 146: 1-2)
Sifa na ibada ni kama mahali pa maisha ya Mungu
Kwa wale mnaoweza kusoma Biblia za kiingereza,
utaona katika baadhi ya tafsiri za Biblia za kiingereza, mstari huu umeandikwa
kwamba ‘Mungu ana inhabit the praises of Israel, yaani Mungu ana-ishi
katika sifa za watu wake. Hili neno ku-inhabit
linatokana na neno la kiingereza la habitat. Na kwa wale
mliosoma biology ya form one (sayansi ya viumbe ya kidato
cha kwanza), mtakumbuka kwamba Habitat – is a special place where living
things are found naturally. Yaani, ni mahali maalum, viumbe wa hupatikana
kuishi kwa asili. Kwa mfano; Siku Nuhu alipofungua mlango wa safina,
hakuhitaji kuwaambia wanyama waende wapi na wapi, bali kila mnyama alijua pa
kukimbilia; kila mnyama alikimbilia katika mahali pake maalumu pa kuishi, kutokana na ile
asili yake, aliyopewa na Mungu.
Naamini uakumbuka habari za Mzee Nuhu, aliyejenga
safina na kuingiza wanyama wote huko ndani. Kisha Mungu akafungulia maji, na
dunia ikazamishwa majini kwa muda wa siku zaidi ya arobaini. Siku Nuhu
alipotoka katika safina, na akaufungua mlango wa safina, wananyama wote
walitoka na kuanza kuimbia, kila mnyama kalilekea katika mahali pake maalum kwa
makazi yake, sawa sawa na asili ambayo Mungu amewaumbia. Tunasoma kwamba, Nuhu
hakuhitaji kuwaelekeza wanyama mahali pa kwenda, bali kila mmoja, sawa sawa na
alivyoumbwa, alivutwa na asili yake kuelekea kule ambako kwa asili, ndiko
maisha yake yalipo.
Nuhu hakuhitaji kumwambia samba, chui, fisi,
twiga, tembo na nyani waende wapi, bali kila mmoja wao, sawa sawa na
alivyoumbwa na Mungu, alivutwa na asili yake kuelekea kule ambako kwa asili,
ndiko maisha yake yalipo; kila mmoja alivutwa kwenda katika habitat
au habitation
yake. Pia, Mzee Nuhu hakuhitaji kumwambia chura, kobe na mamba waende kuishi
wapi, bali kila mmoja wao, sawa sawa na alivyoumbwa na Mungu, alivutwa na asili
yake, kwenda kuishi kule ambako kwa asili, maisha yake ndipo yalipo; kila mmoja
alivutwa kwenda katika habitat au habitation yake.
Wanyama wote walioumbwa kuishi maporini na
msituni, walikimbilia huko kwa asili yao, bila kupelekwa. Na ndege wote
walioumbwa kuishi maporini na msituni, walikimbilia huko kwa asili yao, bila
kupelekwa na mtu. Hiyo ndiyo maana ya habitat ua habitation, ni mahali maalum
kwa maisha ya viumbe, kwa asili zao, bila kupelekwa na mtu yeyote.
Lakini pia, Mzee Nuhu hakuhitaji kumwambia mbwa,
kuku na njiwa waende wapi, bali kila mmoja, sawa sawa na alivyoumbwa, alikamatwa
kubaki pale pale pamoja na familia ya Mzee Nuhu. Kwa asili ya wanyama hawa,
Mungu aliwapa kubaki kuishi na binadamu; kwani ndiko ambako kwa asili, ndiko
maisha yao yalipo; wameumbwa kuishi na sisi. Na ndio maana, kuna njiwa pori na
njiwa wa kawaida. Pia kuna mbuzi pori (swala) na mbuzi wa kawaida. Na mbwa pia,
kuna mbwa wa porini (fisi) na kuna mbwa wa kawaida. Hata na paka, kuna paka porini na paka wa kawaida.
Wa pori ni waporini, lakini, wa kawaida ni wa nymbani kwa binadamu; wameumbwa
kuishi na binadamu. Na wanyama hawa wote wana, wale wa porini na hawa wa
kawaida, wana tabia tofauti kabisa. Wa porini hawafugiki, bali wa kawaida,
wanafugika; ndivyo Mungu alivyowaumba.
Kwahiyo, siku ile maji ya gharika yalipokauka juu
ya uso wa dunia, Mzee Nuhu hakuhitaji kumwambia mbwa na kuku na njiwa waende
wapi, bali wanyama wote hawa, sawa sawa na asili yao waliyoumbiwa, asili yao
iliwakamata kubaki pale pale, kuishi pamoja na familia ya Mzee Nuhu; kwasababu,
kwa asili ya wanyama hawa, Mungu aliwapa kubaki kuishi na binadamu; kwahiyo,
ndiko ambako maisha yao yalipo; mbwa, paka, kuku, bata, mbuzi na njiwa (na
wanyama wengine wa kawaida ambao sijawataja) wameumbwa na Mungu kuishi na sisi.
Kwa lugha ambayo nimekuwa nikiitumia, wanyama hawa, habitat au habitation
yao ni pale binadamu alipo. Hiyo ndiyo maana ya habitat au habitation.
Kwahiyo, Habitat – is a special place where living things are found naturally; yaani,
habitat ni mahali maalum, viumbe wa asili hupatikana kuishi kwa asili zao,
pasipo kupelekwa na mtu. Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit
sifa za Israel, ina maanisha kwamba, Mungu anaishi katika sifa za
watu wake. Ngoja niongee kwa mifano ya kibinadamu, ili unielewe vizuri zaidi;
maana mwalimu bila mifano, shule haiingii vizuri. Ookeey! Kwa Mfano, kama vile samaki kwa
asili yake, anavyoishi katika maji, na ndivyo ambavyo Mungu anaishi
katika sifa za watu wake. Au, kama vile miti, kwa asili yao iliyoumbiwa na
Mungu, inavyoishi katika ardhi au katika udongo, ndivyo ambavyo Mungu anavyoishi katika
sifa na ibada za watu wake; Na kama vile binadamu, kwa asili yetu, tulivyoumbw
kuishi katika hewa, ndivyo ambavyo Mungu anavyoishi katika sifa na
ibada za watu wake.
Ngoja niongee kwa lugha ya kibinadamu kabisa;
Jamani, najaribu kusema hiviii, kama Mungu angekuwa samaki, basi sifa
na ibada ndio yangekuwa maji kwa Mungu; Kama Mungu angekuwa
mti, basi sifa na ibada ndio ungekuwa udongo kwa Mungu; na kama
Mungu angekuwa binadamu, basi hii hewa ya oxygen tunayoivuta, ndio
ingekuwa kama sifa na ibada kwake. Jamani, huu ni mfano tu, sijasema kwamba, Mungu wetu ni samaki au ni mti;
No! No! No! msije mkanitenga na kanisa. Nimeongea tu kwa lugha ya kibinadamu, ili
uweze kuelewa kirahisi uthamani na umuhimu wa sifa na ibada kwa Mungu wetu.
Kwahiyo basi, kutokana na ule mstari tuliousoma
katika kitabu cha Zaburi 22:3 unaosema; ‘Nawe U Mtakatifu, Uketiye (au an-inhabit) juu ya sifa za
Israeli’. Tumeona kwamba, lile neno ‘unaketi’ katika sifa za watu
wako, lina maana kubwa sana. Tumeona kwamba, katika tafsiri zingine za Biblia,
neno hilo linamaanisha ‘unaishi katika sifa za watu
wako’. Na kwa kiingereza, Biblia zingine zimesema kwamba, Mungu ana-inhabit
sifa za watu wake. Na kama Mungu inhabit au anaishi
katika sifa na ibada za watu wake, basi uwe na uhakika kwamba, sifa na ibada kwa Mungu ndio kitu cha
thamani kuliko vyote. Kwasababu, kama sifa na ibada ndiyo mazingira ya
Mungu ya kuishi (yaani ‘Habitation’ yake), basi hiki ndicho
kitu cha maana zaidi na ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu.
Kwa Mfano wa Samaki;
Piga picha mwenyewe, kitu cha kwanza na cha
thamani zaidi kwa maisha ya samaki ni nini? Mimi naamini kwamba maji ndio kitu
cha thamani zaidi kwa samaki, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu maji ndio
mahali yalipo maisha au habitation/habitat ya samaki. Ukimnyima
samaki maji, unamtakia mauti tu. Atakufa! Kwahiyo, hakuna kitu kingine chochote
kilicho cha thamani na umuhimu mkubwa kwa samaki kama maji.
Vivyo hivyo kwa Mungu wetu; kwasababu Mungu
anaishi katika sifa za watu wake au ana-inhabit sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3 inavyosema.
Hivyo basi, kwa ukweli huu, nakwambia kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa
Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo
shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na
ndio maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya
kumsifu na kumwabudu Bwana.
Hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu
cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu
anaishi katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu
tuliyojifunza, Mugnu ana-inhabit sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3
inavyosema. Hiyo ndiyo maana ya habitat au
habitation. Habitat – is a special place where living things
are found naturally; yaani, habitat
ni mahali maalum, viumbe wa asili
hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu.
Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit
sifa za Israel, ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za
watu wake. Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba,
hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu
kwamba, katika vitu vyote, hakuna
kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa.
Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio
hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote.
Kwa Mfano wa Mimea au Miti;
Hebu jiulize mwenyewe, hiviiii, kitu cha kwanza na
cha thamani zaidi kwa miti ni nini? Jiulize tu. Mimi naamini kwamba udongo na
maji ndio vitu vya thamani zaidi kwa miti au maua au mimea, kuliko kitu kingine
chochote; hii ni kwasababu udongo na maji ndio mahali yalipo maisha au habitation/habitat
ya mimea yote. Kwahiyo, hakuna kitu kingine chochote kilicho cha thamani na
umuhimu mkubwa kwa miti na maua na mimea kama udongo na maji.
Vivyo hivyo kwa Mungu, kwasababu Mungu anaishi
katika sifa za watu wake, basi katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha
thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa, kwasababu Mungu anaishi katika
sifa na ibada. Kusifiwa na kuabudiwa ndiyo haja yake kubwa. Kama nilivyosema
hapo kwanza, huko mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kazi nyingine yoyote
zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana. Hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio
kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote.
Kwa Mfano wa Mtu au Binadamu;
Hebu jiulize tena, hiviiii, katika vitu vyooooote
vilivyopo duniani, kitu cha kwanza na cha thamani zaidi kuliko vyote kwa
binadamu ni nini? Jiulize tu. Fikiria vizuri kabla ya kujibu. Je ni ardhi? Je
ni nyumba? Je ni chakula? Mimi naamini kwamba, kitu cha thamani zaidi katika
maisha ya mwanadamu, si chakula, bali ni hewa (yaani oxygen). Hewa ndio vitu
vya thamani zaidi kwa mwanadamu, kuliko kitu kingine chochote, kuliko hata
chakula. Hii ni kwasababu mahali popote penye hewa ya ‘oxygen’, ndipo mahali
yalipo maisha ya mwanadamu wote. Sikiliza, mtu anaweza kukaa dakika 5 bila kula
chakula, lakini mtu hawezi kukaa dakika s bila kuvuta hewa; lazima atakufa!
Kwahiyo, hewa ndio vitu vya thamani zaidi kwa mwanadamu, kuliko kitu kingine
chochote, kuliko hata chakula. Kwahiyo, hakuna kitu kingine chochote kilicho
cha thamani na umuhimu mkubwa kwa binadamu, kama hewa.
Kwa Mungu, kitu cha thamaani zaidi kuliko
vyote, ni sifa na ibada.
Kwa mifano hiyo yoooooote tuliyoiona hapo juu,
basi ni vivyo hivyo na kwa Mungu; kwasababu Mungu anaishi katika sifa za watu
wake, basi katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama
kusifiwa na kuabudiwa; iko hivyo kwasababu, Mungu anaishi katika sifa na ibada
za watu wake. Kutokana na ule mstari tuliousoma katika kitabu cha Zaburi
22:,3 unasema; ‘Nawe U Mtakatifu,
Unaishi (unaketi)
juu ya sifa za Israeli’. Kwa hiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo haja kubwa zaidi ya Mungu kuliko kitu kingine
chochote. Kama nilivyosema hapo kwanza, huko mbinguni, tutakapofika,
hatutafanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana. Hiyo
inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko
kitu kingine chochote.
Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya
Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio
maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya
kumsifu na kumwabudu Bwana; hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha
thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi
katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mungu
ana-inhabit
sifa za watu wake, kama Zaburi
22:3 inavyosema. Hiyo ndiyo maana ya habitat
au habitation. Habitat – is a special place where living things
are found naturally; yaani, habitat
ni mahali maalum, viumbe wa asili
hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu. Kwahiyo
Biblia inaposema Mungu ana-inhabit sifa za Israel, ina maana
kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Hivyo basi, kwa
ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba, hakuna kitu kama sifa na
ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu kwamba, katika vitu
vyote, hakuna kitu kingine cha
thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na
kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi
kuliko vyote.
No comments:
Post a Comment