NUSU WAFAULU MATOKEO YA DARASA LA SABA
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya
mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 yakionyesha kuwa zaidi ya nusu ya
wanafunzi waliofanya mtihani huo Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk
Charles Msonde yanaonyesha kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi ya wavulana,
huku ufaulu kwa jumla ukiwa umeongezeka kwa asilimia 6.38 ikilinganishwa na
mwaka 2013.
Katika matokeo hayo Shule ya Twibhoki iliyopo mkoani Mara
iliibuka ya kwanza kitaifa kati ya shule 15,867 zilizofanya mtihani huo
ikifuatiwa na Mugini, Peacland na Alliance zote za mkoani Mwanza.
Shule ya tano ni Kwema ya Shinyanga ikifuatiwa na St Severine ya
Kagera, Rocken Hill ya Shinyanga, Tusiime ya Dar es Salaam, Imani ya
Kilimanjaro na iliyoshika nafasi ya 10 ni Palikas ya Shinyanga.
No comments:
Post a Comment