Sunday, 2 November 2014

SOMO LA LEO : JUMAPILI IBADA YA ASUBUHI TAR 02/10/2014; KUMTAKA MUNGU NA NGUVU ZAKE

Nini maana ya Nguvu? Ni uweza wa kutawala/kumtawala adui. Nguvu ni matokeo ya mapigano juu ya watu Au vitu.Zipo nguvu za aina mbalimbali nguvu za mwili na nguvu za Roho katika maisha ya Kiroho tunahitaji nguvu ya Mungu ili kuweza kushinda Majaribu ya shetani. Watu wengi wapo kanisani lakini hawana uwezo wa kushinda misukosuko na majaribu ya shetani. FAIDAKUU YA KUWA NA NGUVU ZA MUNGU Nikuwa na uwezo mkuu wa kushinda majaribu dhidi ya mwovu ibirisi. Mitume na manabii walikua na nguvu za Mungu ndyo maana waliweza kushinda majaribu ZABURI 105:4-5. Mkristo yeyote anapokua ameokaoka na kutubu akazipokea nguvu za MUNGU anakuwa imara na hawezi kuteteleka. Mkristo huyohuyo anapotenda dhambi basi nguvu za Mungu hutoweka. Yapomambo mbalimbali yanayp mfanya mkristo kupoteza nguvu za Mungu mabo kama;- 1/Kutokusamehe Mathayo18:21-35 2/Mahusiano mabaya kati ya mume na mke au mahusiano mabaya ya kifamilia 1Petro1:3, 3:7 3/Mahusiano mabaya kati ya mtu na mtu,mtu na jirani yake na mawazo mabaya ndani ya moyo wa mtu yanaweza kusababisha mtu kurudi nyuma kiroho na hatimae kufia dhambini. Ili kuweza kuzipata na kuishi katika nguvu za Mungu ni ;- 1/Kusoma NENO LA MUNGU na kuliishia kama linavyo elekeza YOSHUA 1;8 2/Kuliweka NENO moyoni mwako ZABURI 119;11.,105 Mpendwa wangu neema ya MUNGU ni ya peke sana na ndyo maana tumepewa nguvu yaziada ya kushida majaribu na vikwazo vyote vya Shetani,katika Dunia hii zipo nguvu nyingi sana,waganga,wachawi,wasomi,na watu mashuhuli wote wana nguvu lakini bado nguvu zao haziwezi kumsaidia mtu mwingine,wala haziwezi kukupa tumainila kuishi baada ya kufa. Nguvu za MUNGU wetu aliye mtuma YESU KRISTO aje duniani kwa ajili yetu,akayafanya yaliyo makuu na baadae akatuachia ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye ngao na msaada kwetu Huyu ndiye NGUVU yetu ya kweli ambaye hutupa kushinda mambo yote yanayo tusonga. Kama hujampokea YESU KRISTO kuwa BWANA na mwokozi wa Maisha yako ni wakati wako sasa wa kumpa maisha yako ili uzipate NGUVU ZA MUNGU WETU aliye hai. Mali na pesa zako havitakusaidiaa.. Muda ni sasa wa kumpokea YESU ili awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yako ayabadilishe na uwe kiumbe kipya. Chukua hatua sasa ili uwe miongoni mwa watu wenye NGUVU ZA MUNGU ndani ya Miyo yao.. MUNGU akubariki na aendelee kusema na wewe katika maisha yako yote ya kila siku. Barikwa saana.. BY MWINJLIST JACOB LUKAS-FPCT TEGETA DSM TANZANIA..

No comments:

Post a Comment