Wednesday, 29 October 2014

ZAMBIA YAPATA PIGO, RAIS WA NCHI HIYO BWANA MICHAEL SATA AFARIKI DUNIA.

HAYATI; MICHAEL  SATA
Familia ya Bwana SATA na Taifa la ZAMBIA vimekumbwa na kanzia nzito ya kumpoteza Raisi wao kipenzi. Umauti huo umemfika leo wakati akiwa katika hosptal ya Londoni huko nchini Wingereza amabokoalikua akiendelea kupatiwa matibabu(ugonjwa bado haujatangazwa)                                  Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 alizaliwa mwaka 1937 katika mji wa MPIKA.        Hayati SATA aliingia madarakani septemba 2011baada ya kumshinda aliye kuwa raisi wa nchihiyo Bwana LUPIA BANDA.                                                                                                                       Akiwa madarakani alionekana kuwa ni mtu mwenye kujituma na kuchapa kazi zaidi huku akionesha nia yake ya dhati juu ya kupambana na masuala ya rushwa na kuleta usawa kwenye mambo ya ustawi wa kijamii. Akiwa katika harakati za kisiasa na kijamii alikua ni mtumiaji/mvutaji wa sigara halihiyo ilimfanya awe na sauti ya kukwaluza, Katika uongozi wake hakuwahi kuwa na rafki wa kudumu. Ufanisi wake wa kazi ulimfanya kuwa maarufu na hatimae akawa Gavana wa jimbo la LUSAKA kabla ya kuwa rais.                                                                                                                Hayati SATA amefariki dunia akiwa chini ya uangalizi makini wa madaktari ambao walikua wakijituma kwa juhudi zao ilikuunusuru uhai wa Bwana SATA hata hivyo haikuwezekana..                            Bwana SATA ni raisi wa pili wa Zambia kufariki akiwa madarakani.                                      
HAYATI;  MICHAEL SATA   enzi za uhai wake.

No comments:

Post a Comment