Sunday, 2 November 2014
HUU NI WAKATI WA WAKRISTO KUMUOMBA MUNGU, MTANDAO WA NDOA ZA JINSIA MOJA WAZIDI KUSHIKA KASI
MTANDAO WA NDOA ZA JINSIA MOJA WAZIDI KUSHIKA KASI, MASHOGA NA WASAGAJI KUASILI WATOTO, UFARANSA NAYO YAFUATA NJIA
Kadri siku zinavyoenda, dalili za kiama nazo zinazidi. Sentesi hii inatokana na mchakato wa serikali ya Ufaransa kuandaa muswada ambao unaweza kuwa sheria wiki hii - sheria itakayowafanya watu wa jinsia moja (wanaume kwa wanaume, na wanawake kwa wanawake) wapate haki ya kuoana na kuasili watoto.
Sheria hii ikianza, Ufaransa itakuwa taifa la 12 kuruhusu ndoa za jinsia moja, ikiwa imetanguliwa na nchi za Scandinavia; Denmark iliyoruhusu mwaka 2012, Norway (2008), Sweden (2009) na Iceland (2010), pia kuna Uholanzi (2001), Ubeljiji (2003), Spain, na Canada zilizoruhusu mwaka 2005, pamoja na Ureno (2010), huku nchi pekee ya kiafrika iliyoruhusu ndoa hizi ikiwa ni Afrika Kusini mnamo mwaka 2006. (Tanzania nayo ina wafadhili kadha wa kadha kutoka mataifa haya, aidha Serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali)
Sheria kwa upande wa Marekani, inazuia serikali kuu kutambua ndoa za jinsia moja, lakini baadhi ya mataifa yake kama Connecticut, Iowa, Massachusetts, New Hampshire, New York na Vermon, pamoja na wilaya ya Columbia na maeneo mawili ya wamarekani wa asili, huku Mexico City ikitambua ndoa hizo, lakini kwa baadhi ya maeneo yake tu.
Kwa mantiki hiyo, watu wa jinsia moja wanaweza kuonana, na kuasili mtoto katika nchio yoyote inyotambua sheria hizi, ikiwemo Brazil na Uingereza. Ufaransa ndiyo itakuwa nchi kubwa kiuchumi na kwa idadi ya watu kupitisha sheria hii, ambayo imo katika sera ya Rais Francois Hollande, ambapo tayari kuna watu wameonesha kufurahishwa na jambo hili linaoitwa sheria ya "ndoa kwa wote", ingawa baadhi ya watu wameonesha upoinzani katika taifa hili la kikatoliki kitamaduni
Je, mataifa madogo yanayotegemea nchi zilioendelea ili kukuza uchumi wao zitaweza kuhimili mikiki ya matakwa ya wafadhili? Maombi yatatuepusha na mengi, na kutuokoa na mbinu za adui mwovu shetani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment