Watu hao ambao wamesema wamesafiri kwa njia ya ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza, wamesema walipewa amri na wakubwa wao wanaoishi chini ya maji ili kufika kanisani kuwachukua watu hao ambao hata hivyo hawakuwataja ili wakauliwe kwa njia ya kichawi na kufanywa kafara na mazindiko katika shughuli zao.Wakiwa kanisani hapo walikamatwa nawachungaji wa kanisa hilo ambao walifika asubuhi kama ilivyoada yao kwa ajili ya kufanya maombi na kujitakasa kwa ajili ya ibada. Ingawa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo,kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna kipengele kinachotambua uchawi,hivyo hakuna kesi inayowakabili.dawa ni kuendelea kupiga maombi zaidi ili Mungu aendelee kuwafichua na kuwaponya ili waache tabia ambazo zimekuwa zikinyanyasa na kudidimiza hali za watanzania ambao hawajasimama katika neno.
Wakifanyiwa mahojiano,huku wakitazamwa na watu
mbalimbali waliokusanyika jumapili alfajiri.
|
vifaa vyao vya kazi
Watu
wa usalama pamoja na wananchi wakiwa wamewazunguka wachawi hao.
Mchungaji Diana Bandele na nabii Abigaili Zumaridi wote
wa kanisa la Ufunuo ndio waliowakamata watu hao majira ya alfajiri walipofika
kwa maandalizi ya ibada.
|
No comments:
Post a Comment