Thursday, 25 December 2014

KURUGENZI YA HABARI NA MAWASILIANO KANISA LA FPCT TEGETA KUJA KIVINGINE YAPANGA MIKAKATI KABAMBE

KURUGENZI YA HABARI NA MAWASILIANO FPCT TEGETA  YAJIPANGA UPYA

Kurugenzi ya habari na mawasiliano kanisa la fpct tegeta imesema kuwa wanajipanga kufanya mambo  makubwa kwa kipindi cha mwaka 2015 kwa lengo la kuhakikisha kazi yao inakuwa na ubora zaidi  kwa kutangaza  injili kwa mataifa yote

Akizungumza na mwandishi wetu Mwenyekiti wa idara hiyo bwna Frank Gibebe amesema  lengo lao ni kutangaza neno la Mungu kwa mataifa kupitia mtandao lakini pia kutoa taarifa mbalimbali za kanisa la fpct sambamba na madhehebu mengine huku akisema kwa muda mfupi ambao wamefanya huduma wameona mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na watu mbalimbali kuamua kumpa Yesu maisha baada ya kuona shuhuda mbalimbali ambazo zimekuwa zikitokea katika kanisa la fpct tegeta na kwa makanisa mengine
              Mlezi wa kurugenzi ya habari na mawasiliano fpct tegeta bwn Kakete shephan

‘’unajua mwanzo wakati tunaanza watu wengi waliona kama tunapoteza muda lakini kiukweli mpaka hivi sasa kuna mafanikio mengi tumeyaona na lengo letu ni kuja na maono mapya kwa mwaka ujao ili tuweze kufikia malengo ,namshukuru sana mchungaji wetu wa kanisa la fpct tegeta mch. Joram J. Ntaseha kwa ushirikiano mkubwa kwa idara hii ambayo imezaa matunda katika kanisa kwa muda wa miezi minne tu tangu kuanza kazi tunaamini mwakani kuna mavuno makubwa zaidi” Alisema Gibebe

Aidha alisema anafurahishwa na askofu wa kanisa la fpct jimbo la pwani na Dar es salaam askofu Revert Kamonongo ambaye ameonyesha kuitambua idara hiyo ya habari na mawasiliano na mara kadhaa amekuwa akiifanyia maombezi huku akiwatia moyo kuendelea mbele na kuitangaza kazi ya Mungu kwenye mtandao huku akisema kuwa watu wengi wanapatikana huko hasa vijana
                      Mwenyekiti kurugenzi ya habari na mawasiliano bwn Frank Gibebe
                                            mwenyekiti msaidizi  Hossein Gabriel

Kwa upande mwingine mwenyekiti msaidizi bwana hossein Gabriel amesema wanamshukuru Mungu kwa sababu kila siku wamekuwa wakiona mabadiliko katika idara yao hivyo kuwataka watu mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha injili inasonga kote ulimwenguni


Kurugenzi ya  la Habari na Mawasiliano Fpct Tegeta inaongozwa na Frank Gibebe kama mwenyekiti, Hossein Gabriel Mwenyekiti msaidizi, Gabilo Hosea Mhasibu , na Rasmi leo imemtangaza mtumishi wa Mungu Kakete Shephan ambaye anaishi nchini kanada kuwa mlezi wa idara hiyo
                                Mhasibu kurugenzi ya habari na mawasiliano  Gabilo Hosea

                  mwandishi wa habari kurugenzi ya habari na mawasiliano Happiness Mosha

Askofu wa jimbo la pwani kanisa la fpct ..akofu REVERT KAMONONGO akiwafanyia maombi maalum      viongozi wa idara ya habari na mawasilino kanisa la fpct Tegeta

No comments:

Post a Comment