Sunday, 28 December 2014

UKUAJI WA KANISA NI MAOMBI.(KWA NINI KANISA LIWE NA MAOMBI?) BY ASKOFU KAMONONGO

Katika maisha ya ya Ukristo zipo nguzo ambazo zinamfanya mkristo aweze kusimama na kuendelea mbele zaidi katika maisha ya kiroho.

1/ Maombi yana beba huduma.
     Ili mkristo awe na mafanikio makubwa kiroho lazima awe na maombi ya kufunga na kuomba ili kusonga mbele,kwani katika dunia hii tnayo ishi kuna vikwazo vingisana ambavyo vinaiwinda huduma yako na kuiangusha. usipokua makini utaanguka na hatimae kuibisha huduma yako.
   Ili uendelee kumwona Mungu katika huduma na maisha yako lazima ujiwekee Muda zuri wa kumwomba Mungu ali akusaidie. Maombi yana

2/ Maombi ni kipimo cha Kiroho. { Wakolosai 1;9-11}
     Maombi ndiyo yana lipima kanisa na waumini katika ukuaji wake.
Kanisa linalo kua nilile linalo omba na washilika wake kuombeana. Waumini au kundi la watu linapo kuasanyika na kuombeana kwa pamoja ndipo hekima na maarifa ya Mbinguni huongezeka. kupata ufaham na mawazo ya kujenga ufalme wa Mungu vinapatikana katika maombi..

3/ Maombi Huimalisha Huduma za watumishi na Viongozi wa kanisa.
             Katika urimwengu wa kiroho mtu wa Mungu anawindwa kuliko kitu chochote,ili shetani aweze kulipga kanisa lazima aanze na kiongozi au mtu anaye onekana kuwa na nafasi ya juu katika huduma. Sasa kwa mazingira hayo vita hiyo imehamia katika katika urimwengu wa mwili,mapigano mengine si ya kiroho tu yanaweza kutumwa mwilini Magonjwa,Umasikini na mambomengine kama hayo hufanya huduma kudhoofka. ili kushinda lazima tuombe.

4/ Maombi hushusha nguvu ya Mungu.
   Ili huduma au kanisa liwe na Nguvu ya Mungu yaani miujiza na kalama mbalimbali ziweze kutembea lazima kuomba.
Mungu husema nasi kwa nji ya maombi. Mkristo anapochukua muda mrefu bila kuomba razima atakufa kiroho,kristo au mwamini anafananishwa na mtoto anae nyonya maziwa ya wa mama kila siku, mtoto asiponyonya lazima ata dumaa. Ndiposa yampasa mkristo ndani ya Kanisa aombe ili kuishusha Nguvu ya Mungu inayoendelea kuzaa na kutunza Nguvu ya Mungu.

                  ;-Kadri upatavyo mafanikio ya kimwili usi sahau maombi.

           Urimwenguni mwanadamu anapita,maisha yetu ni mafupi saana lakini tumaini lipo katika ufalme wa Mungu kwamba baada ya maisha haya ya kawaida yapo maisha mengine ambayo tumeahidiwa kuishi milele. Lakini kabla ya kufka katika mji huo lazima tujitenge na dhambi. Mungu ametupatia Roho mtakaifu ambaye anatufanya kuomba na kushinda dhambi. Jitahidi kuchukua hatua ya kuomba kila iitwapoleo.
ASKOFU WA JIMBO LA PWANI NA MISHENI YA MSANGA (FPCT),REVETY KAMONONGO
       Rudi hatua moja nyuma angalia ni wai ulipo anguka na ukatubu ili uzidi kupata nguvu ya maombi na kuendelea kushinda dhambi.

 MUNGU WA MBINGUNI akubariki na uwe na tafakari njema.

No comments:

Post a Comment