Kauli ya Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania imeya tengua maneno yaliyosemwa na waziri wa ardhi,nyumba na makazi Profesa Anna Tibaijuka,siku chache zilizopita alipokua akizungumza na wandishi wa habari kwamba kamwe hawezi KUJIUZULU juu ya tuhuma zinazo muandama akilengwa kuwa ni mmoja kati ya watuhumiwa walio kula mabiloni ya pesa za akaunti ya Tegeta Escrow,akitajwa kupokea kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja nukta tano.
Akizungumza na Taifa kwa kupitia wazee wa jiji la Daresalaam leo hii Raisi Dr Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Diamond Jubilee amemuomba waziri Anna Tibaijuka aachie ngazi hiyo ili kumpisha mtu mwingine aendeleee na majukumu hayo.
|
Raisi Dr Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wazee wa Jiji la Daresalaam |
|
Baadhi ya wazee wakimsikiliza kwa Makini Raisi Dr KIKWETE lipokua akizungumza nao. |
No comments:
Post a Comment