Wednesday, 24 December 2014

MCHUNGAJI JORAM J. NTASEHA... ASEMA WATU WASHEREKEE SIKUKUU YA KUZALIWA BWANA YESU KWA KUMSHUKURU MUNGU

Mchungaji wa kanisa la fpct tegeta jijini Dar es Salaam mch.Joram jeremiah ntaseha amesema ni vizuri watu wakaitumia vizuri siku ya ukumbusho wa kuzaliwa bwana yesu kristo wakiwa magotini kwa kurudisha shukrani kwa Mungu kwa kumleta mkombozi ambaye ndiye aliyejitoa msalabani kwaajili ya dhambi za wanadamu

Akizungumza mapema hii leo ofisini kwake mch.Ntaseha amesema watu wengi wamejisahau na kuuitumia vibaya siku ya kuzaliwa bwana Yesu huku wengine wakithubutu kufanya vitendo viovu kwa kukesha kwenye madisko kukesha kwenye kumbi za Starehe na kufanya ukahaba jambo ambalo linamchukiza mwenyezi Mungu
"ukija kanisani kwangu watakwambia kabisa kuwa nimewaambia waitumie siku hii kumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu na waendelee  kuyatafakari matendo yake makuu na kujiuliza maswali je ni kweli watu wanaishi maisha matakatifu tena katika kipindi hiki cha siku za mwisho huyu mkombozi aliyezaliwa amekuja kwaajili ya dhambi zako wewe uliyeanguka hivyo ni vyema ukaitumia siku hii kulia mbele za Mungu na kumueleza mahitaji yako kwasababu mkombozi anazaliwa ''Alisema mch.Ntaseha
mchungaji Joram Jeremiah Ntaseha

No comments:

Post a Comment