Monday, 8 December 2014

MAJIBU YALIYO TOLEWA NA MWANASHERIA WA ZITTO BAADA YA KUSHUKIWA NA YEYE ALIKULA PESA ZA ESCROW

Ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow ambapo watumbalimbali wakiwemo Mawaziri,wabunge,watumishi wa uma na viongozi wa dini naowlionekana kukumbwa na sakata hilo la ulaji wa pesa hizo.

           Wakati kikao cha Bunge kilipokua kiendelea katika bunge hilo kuna baadhi ya shutuma zili ibuka zikimtuhumu Mwkt wa kamati ya PAC mhe Zitto Kabwe kwamba na yeye ni miongoni mwa watuhumiwa waliokula pesa hizo.
   
Sasa haya ni majibu yaliyo tolewa na Mwanasheria wa Mbunge Zitto, Bw Msando Alberto akijibu tuhuma hizo zilizo ibuliwa na Mbunge Lusinde kwamba Zitto alipokea milioni kumi zilizo toka kwenye akaunti hiyo';-

 1/ Sijapokea pesa yoyote kutoka kwa IPTL/PAP na kumpa mh Zitto.
2/ Hizi ni habari za kuzusha tu kwamba Zitto alipokea pesa yoyote.
3/ Ikiwa ni kweli jambo hilo nawataka IPTL/PAP waje waseme ikiwa ni kweli walinipa pesa ili ni mpelekee Mh Zitto azifanyie nini? na kwa nini walizitoa?
4/ Kwa nini hawakuomba nihojiwe kuuhusu hizo pesa?
 
Hoja ya msingi inabaki na maswali haya kwamba Hizo pesa ni za nani? na Je tumeibiwa au la?

No comments:

Post a Comment