Monday, 22 December 2014

MWALIMU ATIWA NGUVUNI AKIDAIWA KUMNYONGA MTOTO AKIWA GESTI.

Jeshi la Polisi wilayani Mbogwe mkoani Geita lina mshilikia mwalimu mmoja wa shule ya msingi Kasandalala mwl Laideth Costantine mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumuua mwanae wa kiume kwa kumnyonga akiwa kwenye nyumba ya wageni (Gesti)
   
 Tukio hilo limetokea jumamosi tarehe 20/12/2014 usku.
         Pia kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema sasa tunamshikilia mtuhumiwa sasa uthibitisho na ushahidi wa vipimo vya taktari vinaeleza wazi kuwa mtoto huyo aluwawa kwa kunyongwa,Mtu wa mwisho aliye kuwa na mtoto huyo ni mama yake mzazi.''Alisema kamanda Konyo''

 Hata hivyo baadhi ya majirani wamemseme, mwalimu huyo amekua na tabia za ajabu saaana ambazo zilikua zikiendelea kuishangaza jamii.

  Kwa upande mwingne mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya Mbogwe mkoani Geita ndg Cosmas Kilosa amethibitisha juu ya mauaji hayo kwamba mtoto huyo aliuwawa kwa kunyongwa.

No comments:

Post a Comment