Thursday, 18 December 2014

WAZIRI, TIBAIJUKA KAMWE SIWEZI KUJIUZULU

Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka,Amesema kamwe hataweza kujiudhulu nafasiyake ya uwaziri aliyo nayo kwa sasa,kutokana na Kashf ya Akaunti ya Tegeta Escrow iliyo mkumba baada ya kutajwa yakua na yeye ni miongoni mwa watu walio shiriki kugawana pesa hizo.
   Waziri Tibaijuka alisema kiasi cha zaidi ya bilioni 1.6 kilichotajwa kuwa ni mgao alioupata kutoka kwenye akanti hiyo ni fedha alizo zipata baada ya kuomba kwa muda mrefu ili kuziendeleza shule zake za sekondari ya wasichanaya Kajumulo iliyoko mjini Bukoba na Barbro ilipo jijini Dar es salaam. Hivyo  haoni sababu ya kujiuzulu kwa pesa ambazo yeye anaziona ni za halari kabisa na zilitolewa kwa njia za wazi na sahihi.

Waziri Tibaijuka ameendelea kuzungumza mambo mengi na wanahabari leo katika hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam, na Mwisho akasema ''Naiachia serikali iendelee kufanya uchunguzi ikiwa itabaaini kuwa fedha hizo ni haramu nitazirejesha serikalini alisema waziri Tibaijuka''
1q
Waziri wa  Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Ardhi Profesa Anna Tibaijuka.  

No comments:

Post a Comment