Moja ya sababu ya watu kutomsifu na kumwabudu Mungu ipasavyo, ni
kutokujua namna ya kufanya sifa na kuabudu. Mambo/Pointi zifuatazo zitakusaidia
kukuwezesha kujua namna ya kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu. Unapokuwa
umetenga muda wa kusifu na kuabudu, au unapokuwa katika muda wako wa maombi,
tumia ufahamu wako juu ya mambo uliyojifunza kuhusu Mungu, yanayomstahilisha kusfiwa
na kuabudiwa. Kwa mfano:-
A: MSIFU MUNGU KWA YALE MAMBO YANAYOMSTAHILISHA
1)
Mtukuze Mungu kwa Sifa zake za kipekee ( Sifa zake za Ki-Mungu).
Mweleze jinsi alivyo Mtakatifu , Wa
milele, Mwenye nguvu zote, Mwenye akili na ufahamu wote, n.k
2)
Mtukuze Mungu kwa Tabia zake.
Mweleze jinsi alivyo mwenye Upendo mwingi usiopimika,
jinsi alivyo na huruma nyingi, jinsi alivyo mwaminifu na wa kweli. Msimulie
habari ulizozisikia na ulizozisoma juu ya tabia zake kwetu.
3)
Mtukuze Mungu kwa Matendo yake makuu.
Mweleze jinsi unavyohusudu
kazi mbalimbali za mikono yake, uumbaji wake, na matendo yake makuu. Msimulie
jinsi unavyokubali ubora wa kazi zake na ukuu wa matendo yake. Msimulie
unavyothamini matendo yake makuu kutoka katika biblia au katika shuhuda
ulizozisikia katika maisha ya sasa ya kila siku.
4)
Mtukuze Mungu kwa Baraka na Fadhili zake.
Msifu na kumshukuru kwa
fadhili na baraka mbalimbali ulizopata kutoka kwake. Kwa zawadi ya uhai, afya
njema, uponyaji, ulinzi, chakula, kazi, elimu, fedha, mali, mifugo, mashamba,
biashara, n.k. Yako mambo mengi sana, Mungu amekutendea, usiyoweza kumaliza
kuelezea. Msifu kwa hayo.
5)
Mtukuze Mungu kwa Ahadi zake nzuri kwetu.
Pia unaweza kumsifu Mungu kwa ahadi zake mbalimbali
alizotupa. Ukampamba kwa jinsi alivyokusudia kutubariki, kutuinua, kutulinda,
kutushindia, kututetea, kutuwezesha, kutusaidia, n.k.
B: MSIFU
MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa
za Mungu, Tabia za Mungu au Matendo ya Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El-Shaddai.
Ni neno lenye majina mawili ndani yake. ‘El’ maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana itokanayo na
neno ‘Shad’
yaani Titi (Ziwa) la mama
anyonyeshaye.
Kutokana na ukweli kwamba,
titi/ziwa la mama anyonyeshaye, linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa
ya mama yake, humpa mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna
vitamini, protini, wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto
anachohitaji. Maziwa ya mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo,
Waisraeli wanapomwita Mungu El-Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama
ziwa linavyo mtosheleza mtoto, vivyo
hivyo, Mungu ni ‘Mtoshelezi’
kwetu. Halleluyah!
Hivyo, kila jina la Mungu,
linabeba aidha Sifa yake au Tabia yake au Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi
anasema “… Mpeni Bwana, enyi wana wa
Mungu … Mpeni Bwana utukufu kwa jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri
wa utakatifu.” (Zab 29:1-2) Msifuni Bwana kwakuwa Bwana ni mwema, Liimbieni Jina lake, kwakuwa
lapendeza.(Zab 135:3). Unaweza kumsifu Bwana kwa
majina yake. Yafuatayo ni baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya Kiebrania,
yatakayokusaidia kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu.
-
No comments:
Post a Comment