Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Vijijini, Anna Rosse Nyamubiambapo , wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini (REA) ambapo amesema katika mkoa wa shinyanga kumekua kukigubikwa na matukio mbalimbali ya mauaji ya vikongwe wakidhaniwa ni wachawi kwavile tu macho yao ni mekundu kumbe si sahihi wanachofanyiwa..
Ameendelea kusema kuwa upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika utawasadia vikongwe kupika kwa njia za kisasa kabisa kwa kuepuka matumizi ya majiko ya kuni ambayo huwafanya machoyao kuwa mekundu kwa sababu ya moshi wa kuni.
|
MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI BI ANNA ROSSE NYAMUBI(Aliyeshika kipaza sauti) akiimba wimbo wakufurahia kwenye uzinduzi wa mradihuo,hakucheza pekeyake yupo na ananchi wengine. |
|
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AKIWAHUTUBIA WANANCHI WAKATI WA UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI(REA) |
Pamoja na hayo waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amewataka wananchi kujiadhali na vishoka sambamba na wale wote wanao tumia umeme kinyume na taratibu za kisheria''Wanachi tunayo nafasi haki na wajibu wa kuwafichua wote wanaohujumu mali zetu wenyewe kwani tunawafahamu kabisa kwani tunakulanao,tunaishinao pia ni nduguzetu"alisema Waziri Muhongo wakati akizindua rasmi mradi huo..
No comments:
Post a Comment