Sunday, 30 November 2014

SEMINA,SEMINA,SEMINAAAA...

Mch Joram J. Ntaseha-FPCT TEGETA

Mchungaji Joram J. Ntaseha wa kanisa la FPCT TEGETA-Machinjioni kwa kushilikiana na umoja wa akina baba wa kanisa,Wanakukaribisha kwenye semina ya neno la Mungu.Inayo wahusu akina baba wote.
 Semina hiyo itafanyika tar 07/12/2014 saa 8;00 mchana
           .Walimu kutoka nje na ndani ya kanisa hilo watakuwepo.
                     Masomo yatakayo fundishwa ni pamoja na;-
                               1/ Wajibu wa baba/mwanaume katika familia.
                                          2/ Malezi bora kwa watoto huanza kwa baba n.k

Jinsi ya kufika Ukitokea  Bagamoyo,Bunju au Mwenge, shukia Tegeta kwa Ndevu. Uliza mtu yeyote Machinjio ya Tegeta ukifika hapo uliza mtu yeyote kanisa la Fpct tegeta atakuonesha au piga 0765032762
    Chakula na vinywaji vitakuwepo siku hiyo.
         Wababa wooote mnakaribishwa kwene SEMINA hiyo

Saturday, 29 November 2014

HERKOPTA YAANGUKA DAR NA KUUA ASKALI WANNE

Ajali ya herkopta inayosemekena kuwa ni milki ya wizara ya maliasili na utalii imedondoka leo katika eneo la Kipunguni B,Moshi bar Ukonga jijin Daresalaam,.

     Chanzo chetu cha habari kimezungumza na kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Dar es salaam kamanda Suleimani Kova alisema ni ajari mbaya kutokea kwa mwaka huu katika wigo wa usafili wa anga, na alipoulizwa kuhusu chanzo cha ajali hiyo alisema kwa sasa bado hakija julikana bado hivyo taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi na utafiti wa wataalam kukamilika..

Picha ya ajali ya Herkopta ilivyo harbika baada ya kudondoka
Kamanda Kova aktoa maelezo kwa wanahabari.
   Tukio hilo limepelekea kupoteza maisha kwa Askari wanne wajeshi la polisi na Rubani mmoja ,Kamanda Kova mehibitisha kutokea kwa tukio hilo.

HATA SASA MUNGU AMETUSAIDIA

Mungu ni mwema :askofu Revert Kamonongo akiwa na mchungaji Joram jeremia Ntaseha ambaye ni mchungaji wa kanisa la fpct tegeta machinjioni kwenye moja ya ibada za kanisa hilo....askofu Revert Kamonongo alikuwa na huduma ya maombezi ya baraka kanisani hapo
.

TAZAMA PICHA: TUJIKUMBUSHE KIDOGO SHEREHE ZA KUWABARIKI WACHUNGAJI KANISA LA FPCT MISSION YA MSANGA

tujikumbushe kidogo namna sherehe za kuwabariki wazee na wachungaji wa mission ya msanga kanisa la fpct zilivyofana ilikuwa ni tarehe 24/8/2014
                        kushoto ni mchungaji Joram Jeremiah akiwa na Mwl Amri Rubarati
            mchungaji Joram Jeremiah akipongezwa na washirika wake wa kanisa la fpct tegeta
       mzee wa kanisa la fpct tegeta Gabriel Gabo akiwa na mke wake nao waribarikiwa siku hiyo
                         Kushoto ni askofu Revert Kamonongo akiwa na mwalimu wa semina
mwandishi wa habari wa fpct tegeta blog bwn.frank Gibebe akifanya mahojiano na askofu Kamonongo
                          viongozi wa kanisa la fpct mission ya msanga kwenye picha ya pamoja



                                                     watu walikuwa wengi sana

Friday, 28 November 2014

KARIBU SANA KWENYE IBADA ZETU....HAPA FPCT TEGETA

KARIBU SANA KWENYE IBADA ZETU....HAPA FPCT TEGETA MACHINJIONI



   

 JUMANNE SAA KUMI JIONI..........IBADA YA KINA MAMA.

JUMATANO SAA KUMI JIONI .....IBADA YA MAFUNDISHO.

ALHAMISI SAA KUMI JIONI.......MAZOEZI YA KWAYA .

IJUMAA SAA NNE KAMILI ASUBUHI......IBADA YA MAOMBI.

JUMAMOSI SAA KUMI JIONI ....MAZOEZI YA KWAYA.

JUMAMOSI SAA MOJA USIKU .....MAZOEZI YA SIFA NA KUABUDU.

JUMAPILI SAA MOJA ASUBUHI MPAKA SAA NNE....IBADA YA KWANZA.

JUMAPILI SAA NNE ASUBUHI MPAKA SAA SABA MCHANA .... IBADA YA PILI.

JUMAPILI SAA KUMI JIONI .....MAFUNDISHO YA VIJANA.

KARIBUNI SANA TUMUABUDU MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI

Wednesday, 26 November 2014

SOMO LA SIFA NA KUABUDU LINAENDELEA ...SIFA NA IBADA YA MBINGUNI

SOMO:SIFA NA KUABUDUDU
sehemu ya tatu 
SIFA NA IBADA YA MBINGUNI

Katika Sehemu ya pili , tumejifunza maana ya neno la kiingereza la habitat au habitation, jinsi linavyoweza kubadilisha uelewa wetu juu ya sifa na ibada kwa Mungu. tumejifunza kwamba, Habitat – is a special place where living things are found naturally; yaani, habitat ni mahali maalum, viumbe wa asili hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu. Kwahiyo Biblia inaposema katika kitabu cha Zaburi 22:3 kwamba, Mungu ana-inhabit au ameweka kiti chake katika mazingira yaliyo na sifa za Israel (au sifa za watu wake), hii ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake.

Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba, hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Tumejifunza kwamba, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana.


Hii inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mungu ana-inhabit  sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3 inavyosema. Sasa katika sura hii, nimeazimu kukuonyesha jinsi Mungu alivyo serious kuhusu ksifiwa na kuabudiwa. Serious ni neno la kiingereza lenye maana ya kumaanisha sana. Mtu aliye serious, ni mtu asiyetaka utani, uzembe wa mchezo-mchezo katika mambo yake. Na vivyo hivyo, Mungu wetu yuko very serious katika swala la sifa zake na ibada yake, yaani hana utani, wala hataki uzembe wala mchezo mchezo inapokuja katika maswala ya kumsifu na kumtukuza, yuko very very serious. Katika sura hii, nataka nikuonyeshe jinsi ambavyo Mungu anaheshimu sana sifa. Hebu twende mbinguni kidogo, ili nikuonyeshe hii kitu ninasema.


Kwa Mfano wa ibada ya Mbinguni;
Biblia inaeleza kwamba, kule mbinguni, Mungu amejizugushia maelfu na maelfu ya malaika wengi, ambao kazi yao pekee, ni kumsifu na kumwabudu Mungu, usiku na mchana. Ngoja tusome wote;

      Ufunuo 4:9-11, Biblia inasema kwamba, mbinguni kuna viumbe fulani wane, wenye uhai;
    
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. Na hao wenye uhai, wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukurani, yeye aliye hai hata milele na milele, ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
 (Ufu 4:9-11)
  
Katika Ufunuo 5:11-14, Utaona Biblia inasema kwamba,
Kisha nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na  za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa, elfu kumi mara kumi elfu, na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili mwana kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya bahari na vitu vyote vilivyoko ndani yake, nilivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza, una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye mwana kondoo, hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka wakasujudu.
                                                                                         (Ufu 5:11-14)

Mpendwa, hivi ndivyo ambavyo Mungu anathamini sana kusifiwa na kuabudiwa au ibada. Hivi ndivyo ambavyo Mungu anaheshimu sana kusifiwa na kuabudiwa au ibada. Na ndio maana anataka kusifiwa au anaagiza kusifiwa au anaamuru apate kusifiwa. Jamani, Mungu anathamini sana kusifiwa na kuabudiwa; hawa malaika, ni maelfu mengi ya malaika, wanamsifu na kumwabudu Mungu kila siku, tena kwa masaa 24 mfululizo, mchana na usiku, bila kupumzika. Ni maelfu na maelfu ya malaika wengi sana, Mungu amejiwekea huko juu mbinguni, wamekizunguka kiti chake cha enzi, usiku na mchana, wanamwimbia Mungu, wanamsifu Mungu, wanamwabudu mungu, wanamsujudia Mungu na kuanguka mbele zake, ambaye ni muumba wao.

Hawa malaika jamani, ni wengi sana. Hapo mbele nitakuonyesha msatri mmoja unaoeleza hesabu ya kwamba wapo wangapi. Ni hesabu ya kawaida kabisa, unaweza ukajaribu kuipiga ili uweze kujua, hii kwaya tu ya mbinguni, ina malaika waimbaji wangapi; lakini ni malaika wengi sana. Na Biblia inasema kwamba, hawa malaika wapo wa kabila mbili kubwa, wanaitwa Makerubi na Maserafi. Hawa malaika wa kabila hizi mbili, hawana kazi nyingine yoyote ya kufanya, zaidi ya kumsifu na kumwabudu Mungu. Hawa malaika, hawana kazi ya kufua, wala kupika; hawana kazi ya kulinda au kupeleka habari popote. Biblia inasema kwamba, hawaondoki mbele za Mungu, bali kazi yao pekee ni moja tu, yaani kumsifu na kumwabudu Mungu.

Hiyo inatuonyesha kwamba, Mungu yuko very serious’ kuhusu kusifiwa na kuabudiwa, wala hataki mchezo kuhusu kusifiwa na kuabudiwa, kwasabau kusifiwa na kuabudiwa ndiyo biashara muhimu zaidi kwake kuliko kitu kingine chochote. Hebu tusome maandiko matakatifu ya Neno la Mungu kwanza, ili nikuonyeshe hiki ninachosema hapa. Nataka uone mwenyewe jinsi Biblia inavyosema kuhusu sifa na ibada ya mbinguni. Hii itakuonyesha jinsi ambavyo Mungu yuko very very serious’ kuhusu sifa na ibada za viumbe na watu wake.

Jamani, Mungu anathamini sana kusifiwa na kuabudiwa; hawa malaika elfu nyingi, wanamsifu na kumwabudu Mungu kila siku, tena kwa masaa 24 mfululizo, mchana na usiku, bila kupumzika. Ni maelfu na maelfu ya malaika wengi sana, wamewekwa na Mungu huko juu mbinguni, kukizunguka kiti chake cha enzi. Yaani, nikiongea kwa lugha ya kibinadamu, sifa kwa Mungu ni kama maji kwa samaki. Sifa kwa Mungu ni kama ardhi kwa mimea. Sifa kwa Mungu ni kama hewa ‘oxygen’ kwa binadamu. Mungu anaheshimu sana sifa kuliko kitu kingine chochote. Ni kama wewe unavyoheshimu oxygen au kama samaki anavyothamini maji.
Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana; hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mungu ana-inhabit  sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3 inavyosema. Hiyo ndiyo maana ya habitation, a special place for life.

Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit sifa za Israel, ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba, hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote.

Na ndio maana huko mbinguni, Mungu amejizungushia malaika maelfu elfu, Biblia inasema kwamba, ile hesabu ya tu, ya kwaya hii ya mbinguni, elfu kumi, mara elfu kumi, mara elfu, mara elfu. Ni hesabu inayoweza kupigika kabisa. Jaribu; ukishindwa tumia kikokotoo au ‘calculator. Natamani uone jinsi ambavyo Mungu hataki utani inapofika katika maswala ya kusifu na kuabudu. Jaribu kupiga hii hesabu ya idadi yao, ili tuweze kujua, hii kwaya ya mbinguni ina waimbaji wangapi. Hapo utaelewa jinsi Mungu wetu alivyo very serious kuhusu sifa na ibada.

Hesabu ya mbinguni
Kama umefanya hii hesabu kwa usahihi, utakuwa umepata namba yenye masifuri 14. Unajua kuna wengine wenu mikimbia hesabu darasani, basi ngoja nikusaidie, tufanye wote. Biblia inasema kwamba, ile hesabu ya hawa malaika tu, idadi ya kwaya hii ya mbinguni, ni elfu kumi, mara elfu kumi, mara elfu, mara elfu. Hebu tujaribu kufanya Hisabati kidogo, tuipige hii hesabu tuone idadi ya kwaya ya mbinguni, ili uweze kuona jinsi Mungu alivyo serious na ibada. Usiogope, ni hesabu rahisi tu. Haya, twende darasani kidogo. Biblia inasema kwamba, ile hesabu ya hawa malaika tu, idadi ya kwaya hii ya mbinguni, ni elfu kumi, mara elfu kumi, mara elfu, mara elfu. Yaani hivi;

10,000  x  10,000  x  1,000  x  1,000   =  100,000,000,000,000.

Kwa wale mliokimbia hesabu darasani, ukitaka kuifanya hii hesabu ya kuzidisha kwa njia rahisi nay a mkato, unafanya hivi; kwa namba yenye masifuri mengi hivi, wewe yahesabu tu masifuri yooote ujue yako mangapi, halafu, yaweke pembeni. Kwahiyo, katika 
10,000  x  10,000  x  1,000  x  1,000  

Wewe yakusanye masifuri yooote haya, yako 14, kisha uyaweke pembeni, tutayarudishia baadaye. Kwahiyo, ukiondoa masifuri yote haya kutoka katika hesbu yetu, utakuwa umebekiwa na namba zinazoonekana hivi,
                                         1  x  1  x  1  x  1  =  1  

Kwa hiyo, ukizidisha moja na moja, jibu letu ni moja (1). Sasa, tuchukue yake masifuri yetu, tuliyoyaondoa, na tuyapachike au yarudishie, na kuyabandika yote, katika jibu tulilopata. Kumbuka kwamba, tuliondoa masifuri 14. Kwahiyo, tukiyarudisha masifuri yote, na kuyabandika katika hili jibu tulilolipata, basi jawabu letu litakuwa kama hivi.

                                                                                  =   100,000,000,000,000.

Kwahiyo, kama na wewe iliifanya hesabu hii kwa usahihi, ni lazima utakuwa umepata namba yenye masifuri 14. Katika hesabu, hiyo namba inaitwa Trillioni 100. Trillioni 1 ni sawa na Billioni 1,000. Kwahiyo Trillioni 100  ni mafungu 100 yenye Billioni elfu moja moja, kila moja. Hao ni malaika wengi sana jamani. Na Biblia inasema kwamba, hawa malaika Trillioni 100, ni hesabu ya malaika waimbani tu. Hiyo ndiyo idadi ya kwaya ya mbinguni ndugu yangu. Halafu wewe tunakwambia uje kumsifu Mungu, bado unaringa au unajifanya bize (busy). Mungu ana watu bwana. Kusifu ni kwa faida yako pia mpendwa, ohooo! (Nitakufundisha hii baadaye).

Kwahiyo hawa ndio malaika walizungushwa katika kiti cha enzi cha Mungu, ili kumsifu yeye, usiku na mchana, wako Trillion 100. Na kwa taarifa yako, hapo hatujawahesabu na kuwajumkisha wale wa wizara zile nyingine mbili; wale malaika wa wizara ya ulinzi na usalama, malaika wanajeshi, au malaika wa vita, walio chini ya uongozi wa Malika Mkuu Mikaeli; hatujawahesabu hao; na pia watujawahesabu wale malaika wa wizara ya habari na mawasiliano, wale wanaosambaza jumbe za Mungu, chini ya usimamizi wa Malaika Gabrieli; na hao pia hatujawahesabu wala kuwajumlisha katika idadi hii ya Trillioni 100. 
Kwahiyo, hawa malaika Trillion 100, ni malaika waimbaji tu; hawa ndio walio katika wizara ya kusifu na kuabudu, wizara ambayo zamani, ilikuwa chini ya Malaika Lusifa, kabla hajasababisha ule uasi uliotokea mbinguni (kwa sasa, huyu Lusifa, sasa ndiye ibilisi shetani). Lakini zamani, kabla hajaangushwa  na kutupwa huku chini duniani, alikuwa kiongozi wa hii kwaya ya mbinguni. Usome vizuri kitabu cha Ufunuo 12:3-4, 7-12, 27 na Isaya 14:10-16 na Ezekieli 28:11-19 utaiona hiyo. Lakini nadhani hebu tusichanganye masomo; naahidi nitakufundisha vizuri zaidi kipengele hiki, katika kitabu changu kingine cha Vita vya kiroho. Lakini kwa sasa, hebu turudi katika somo letu.

Kwahiyo, hawa malaika Trillioni 100, ni wale ambao ni waimbaji tu; masaa yote 24, hawa hawaondoki mbele za kiti cha enzi; kazi yao moja na ya pekee ni kumsifu na kumwabudu Mungu tu. Hawa malaika, hawana kazi nyingine isipokuwa kumsifu na kumwabudu Mungu; hawana kazi ya kulima, wala kuvuna; hawana kazi ya kufua wala kufagia; hawana kazi ya kulinda pamoja na malaika walinzi wa Mungu walio chini ya malaika Mkuu Mikaeli, wala kazi ya kupeleka barua au ujumbe popote, pamoja na malaika walio chini ya Malaika Gabrieli, hapana! Kazi yao ya pekee ni moja tu, kumsifu, kumtukuza na kumwabudu Mungu tu!

Vitu vyote vimeumbwa, kwa mahitaji na matakwa ya Mungu.
Biblia inasema kwamba, usiku na mchana, malaika hawa huwa mbele za Mungu tu, wakikizunguka kile kiti cha enzi, na kumsifu na kumwabudu Mungu; tena huanguka na kuinuka, huinama na kusujudu, wakisema “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, wewe ndiwe Mungu, uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya ‘mapenzi’ yako, vitu vyote vilikuwako, navyo vikaumbwa.” (Ufunuo 4:11). Maana ya sentensi hii ya mwisho ni kwamba, ‘vitu vyote vimeumbwa na Mungu ili kutimiza ‘mapenzi’ ya Mungu.’ Na kwa shule tuliyojifunza katika sura zilizopita, tumejua sasa ya kwamba, mapenzi’ ya Mungu ya kwanza ni kusifiwa na kuabudiwa.

Tafsiri zingine za Biblia, zinasema kwamba, hayomapenzi’ ya Mungu, si tu kwamba ni ile nia ya Mungu au ni ule mpango wa Mungu, bali pia, hili neno ‘mapenzi’ ya Mungu, pia limemaanisha, ‘mahitaji ya Mungu au ‘matakwa ya Mungu. Na kwa shule tuliyojifunza katika sura zilizopita, tumejua sasa ya kwamba, mahitaji’ ya Mungu ya kwanza ni kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, lugha nyingine ya neno ‘mapenzi’ ni ‘mahitaji’ au ‘matakwa’. Kwahiyo, kwa uelewa huo, tukiuweka huo msamiati mpya katika ule mstari wa Ufunuo 4:11, tunaweza kusema kwamba;
Wale malaika trillion 100, wanazunguka na kumsujudu Mungu wakisema “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, wewe ndiwe Mungu, uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya ‘matakwa’ yako vitu vyote vilikuwako, navyo vikaumbwa.’ Au pia, inaweza kusomeka kwamba ‘… kwasababu ya ‘mahitaji’ yako vitu vyote vilikuwako, navyo vikaumbwa.” (Ufunuo 4:11). Na kwa shule tuliyoipitia, sas tumeshajua, tena kwa hakika ya kwamba, mahitaji ya Mungu ya kwanza ni kusifiwa na kuabudiwa; au kwa lugha nyingine ni tunaweza kusema kwamba, ‘matakwa’ ya Mungu ya kwanza ni kisifiwa na kuabudiwa.

Feni na Air-Condition za Mungu
Hapo juu tulisema kwamba, kama Mungu angekuwa mwanadamu, anayeishi katika nchi yenye joto kali, kwa mfano la kule uarabuni, basi sifa na kuabudu ndivyo vingekuwa hewa yake. Sasa basi, hebu piga picha, katika mazingira kama hayo, kama Mungu angekuwa mwanadamu, ni lazima angehitaji feni za kumpulizia au air-condition ya kumpoozea joto na kumtengenezea hewa safi. Na kama ingekuwa ndio hivyo, sifa na kuabudu ndivyo vingekuwa hewa ya Mungu. Na kama ndivyo, basi wale malaika waliomzunguka Mungu, ndio wangekuwa vyombo maalum vya kumtengenezea Mungu, ile hewa anayoihitaji, yaani sifa na ibada!

Kwa uelewa huu, basi hao malaika Trillion 100, ndio wangekuwa hizo feni za Mungu za kumpulizia ili apate upepo mzuri wenye ubaridi ili kumpooza na joto kali la duniani. Au hao malaika trillion 100, ndio wangekuwa air-condition za Mungu, za kumpulizia hewa saaaaaafi ya ubaridi. Kama mwanadamu anavyoishi kwenye hewa safi, ndivyo ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Halleluyah!  Sasa piga picha, mtu aliyejizungushia feni triliioni 100 anajaribu kukuonyesha nini? Fikiri tu mwenyewe. Kweli, mtu aliyejitundikia air-condition trillion 100 kwenye sebule au ukumbi wake, hivi mtu huyo anajaribu kukwambia nini? Umeweza kukisia, mtu kama huyu anajaribu kutuambia nini sisi tunaomtazama?

Mimi nadhani, mtu wa namna hiyo anajaribu kukwambia kwamba, yuko very very serious kuhusu kupata hiyo hewa yake; yaani hataki mchezo. Basi na kwa Mungu ni hivyo hivyo; Jamani, ndivyo ambavyo Mungu wetu alivyo; Mungu yuko very very serious kuhusu kusifiwa na kuabudiwa, kama maandiko tuliyoyasoma, yalivyotuonyesha kwamba, Mungu wetu anakaa au anaishi katika mazingira ya sifa na ibada. Na hataki utani wala michezo ya hovyo hovyo, juu ya ibada yake. Mimi nadhani ndicho Mungu anachojaribu kutuonyesha na kutuambia; kwamba yuko serious!
Mabomba ya Maji ya Mungu
Nikupe mfano mwingine; piga picha, kama Mungu angekuwa samaki, anayeishi kwenye Bwawa la maji, ni lazima angehitaji mabomba ya kuingiza maji katika bwawa lake. Na kama ingekuwa ndio hivyo, basi hao malaika trillion 100, ndio ambao wangekuwa ni mabomba ya kumuingizia maji katika bwawa lake ili apate maji. Kama samaki anavyoishi kwenye maji, ndivyo ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Halleluyah!

Sasa, piga picha, mtu aliyewekea mabomba trillioni 100,  hivi unadhani anajaribu kukwambia nini? Mimi nadhani, mtu wa namna hiyo anajaribu kukwambia kwamba, yuko very very serious kuhusu kupata hayo maji yake; yaani hataki mchezo. Basi na kwa Mungu ni hivyo hivyo; Jamani, ndivyo ambavyo Mungu wetu alivyo; Mungu yuko very very serious kuhusu kusifiwa na kuabudiwa.

Sasa, kwa mfano huo huo, ni muhimu uelewe kwamba, viumbe wote sisi, tumeumbwa na Mungu duniani, ili tuwe kwake kama vyombo maalum vya kumsifu na kumwabudu yeye Mungu. Kusifu na kuabudu kunatupa sababu na maana ya sisi viumbe kuishi.  Na ndio maana Daudi alipoelewa ufunuo huu, akajiambia mwenyewe, kusema “… Ee nafsi yangu, umsifu Bwana”. Halafu katika mstari wa pili, Daudi anatuambia na sisi wengine kwamba;
Nitamsifu Bwana, muda ninaoishi, nitamwimbia
      Mungu wangu ningali ni hai” (Zaburi 146: 1-2).”

Ufunuo wa Mfalme Daudi.
Na ndio maana, Roho Mtakatifu alipompa Mfalme Daudi ufunuo huu; Kwamba viumbe wote ni vyombo maalum vilivyoumbwa kumsifu na kumwabudu Mungu, Daudi akaandika tena waraka maalum au wimbo maalum kwa viumbe wote, ili kuwaamuru na kuwakumbusha, watenge muda maalum wa kumsifu na kumwabudu Mungu. Mfalme Daudi akaandika waraka huo au wimbo huo katika Zaburi 148.







SAKATA LA TEGETA ESCROWNA VIGOGOWALIOMULIKWA BILA CHENGA

Kamati ya bunge ya hesabu za serikali leo imetoa ripoti yake inayoelezea sakata zima linalo husisha upotevu wa wa ma milioni ya pesa ambapokiasi cha zaidi ya bilioni miatatu zinatwa kuibiwa.
 
Akitoa maelezo na majumuisho mwkt wa kamati hiyo mhe Zitto Kabwe na Makam mwkt mhe DeoFillikunjombe wametoa maelezo na vielelezo tofauti vinavyo elekeza jinsigani pesa hizo zilitumiwa,amabapo vingozi wakuu wa serikali na watumishi wa umma nao wameguswa na kisu hicho.

 Wakitoa maelezo mwkt na makam wake kila mmoja kwa nafasi yake kwa ujumla wazilri mkuu,waziri wa nishati na madini,katibu mkuu wa nishati na madini na mwanasheria mkuu wa serikali wmehusishwa na sakata hilo

Aidha kamati imewataka wale wote wliohuska na tukio hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwemo kuvuliwa nyazifa zao na kufilisiwa malizao. 

Mh Zitto Kbwe
Sakata hilo linaloendelea bungeni linaendelea kuwakumbusha watanzania tukio la Richomond na  EPA mbalo lilipelekea waziri mkuu Lowasa kujiudhulu.

Saturday, 22 November 2014

SOMO LA SIFA NA KUABUDU LINAENDELEA....KWANINI MUNGU ANATAKA KUSIFIWA

SEHEMU YA PILI
KWANINI MUNGU ANATAKA KUSIFIWA
Katika sura iliyopita, tumejifunza kwamba, Mungu anaheshi sana sifa na ibada, na Mungu anataka sana kusifiwa na kuabudiwa. Na kama vile Mfalme Daudi alivyoandika katika Zaburi 22:3 kwamba; “Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.” Hivyo, tumeona kwamba, Mungu ametuumba sisi na viumbe wote, ili tutimize mapenzi yake au matakwa yake au mahitaji yake, amabyo ni kusifiwa na kuabudiwa. Ndio maana Mungu anataka sana kusifiwa na kuabudiwa; yaani sifa na ibada kwa Mungu, ni vitu vya thamani sana na vya umuhimu sana. Kwakweli, Mungu anaheshimu sana sifa na ibada
.

Na tumejifunza kwa maisha ya Mfalme Daudi, jinsi alivyolielewa kusudi hili la Mungu juu ya maisha yake au juu ya maisha yetu sis wanadamu, kwamba tumeumbwa tuwe kama chombo cha kumsifu na kumwabudu Mungu siku zake zote za maisha yake, maadam tunaishi. Hivyo basi katika sura hii, kama nilivyokuahidi, hebu tuchimbe zaidi na tutafute kujua, kwanini Mungu anataka sana kusifiwa. Katika sura hii, nataka tujifunze kwa undani zaidi, sababu inayomfanya Mungu kupenda sana sifa, na hata kuumba viumbe wote ili wawe au ili tuwe, vyombo vyake viteule, vya kumsifu na kumtukuza yeye. Hebu tujifunze kwanini Mungu anaheshimu sana sifa.

Mungu anaishi katika sifa na ibada viumbe na watu wake.
Uuumm … Si watu wengi wanaojua kwanini Mungu anaheshimu sana sifa na kwanini Mungu anapenda sana ibada na sifa. Na hivyo basi, si watu wengi wanaojua kwanini Mungu anataka sana kutukuzwa na tena ameagiza kwamba asifiwe. Kwahiyo, katika kipengele hiki, nataka nikupe ufunuo huo, ili nawe upate kujua, kwanini Mungu aliumba viumbe vyote na alituumba na sisi wanadamu. Nataka na wewe upate ufunuo huu, ili upate kujua sababu inayomfanya Mungu kuheshimu sana sifa na ibada. Katika kipengele hiki, utaelewa jinsi ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake, yaani jinsi Mungu anavyoishi katika sifa na ibada. Hebu tuanzie katika mistari hii, ambayo tumekwisha kuisoma mara kadhaa; Zaburi 22:3 inayosema kwamba;

“Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.”
(Zaburi 22:3)

Ngoja nianze kwa kusema kwamba, Mungu alitumia mstari huu mmoja, kufungua sana macho ya moyo wangu, ili kunipa ufunuo huu ambao ulibadilisha maisha yangu, kama ulivyobadilisha maisha ya Daudi bin Yese. Mstari huu ulileta ufunuo mkubwa sana maishani mwangu, hata kuweza kuelewa jinsi Mungu anavyoheshimu sana sifa na ibada. Niliweza kuelewa kwanini Mungu anapenda sana sifa na ibada. Nami nataka na wewe pia uweze kuelewa jinsi Mungu anavyoheshimu sana sifa na ibada, hata akatuumba na sisi ili tumpe sifa na utukufu. Ni maombi yangu kwamba, Mungu akupe ufunuo huu, afungue macho ya moyo wako pia, ili na wewe uweze kuelewa umuhimu wa sifa na ibada kwa Mungu, na ili na wewe uanze kuwa chombo cha sifa na ibada kwa Mungu. na Mungu akujalie kufanya wito huu kwa uaminifu na bidii.

Maandiko haya katika Zaburi 22:3 yanasema kwamba, ‘Nawe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli (au kwa maana nyingine, ukaaye katika sifa za watu wako).’  Angalia tena vizuri, hilo nenouketiye’. Hilo neno kuketi, halimaanishi tu kukaa, bali linamaanisha pia kuishi. Ni neno la kawaida kabisa tulilolizoea katika lugha za kila siku. Kwa mfano, mtu akiulizwa kuhusu mahali gani anapoishi, mara nyingi huwa tunasema ‘mimi ninakaa mtaa fulani’ au ‘mimi ninakaa kitongoji fulani’. Na hapo huwa tunamaanisha kwamba, tunaishi katika mtaa huo au tunaishi katika kitongoji hicho au eneo hilo, na sio kwamba huo mtaa unaokaa, huwa unaukalia kama vile unavyokalia kiti chako; haapanaaa! Bali huwa tunamaanisha kwamba, huko uliposema  unapokaa ndipo mahali pako au mahali petu pa makazi au maisha; yaani ndipo mahali wewe unapoishi.

Kwa mfano; Mtu anaposema mimi ninakaa Kinondoni, au Temeke au Ilala; au mtu anaposema kwamba ‘mimi nakaa Ubungo au Kariakoo,’  huwa tunajua kabisa ya kwamba, mtu huyo hamaanishi kwamba, Kinondoni ni kiti chake au Ubungo ni kiti chake au huo mtaa alioutaja ni kiti chake cha kukalia; haapanaaa! Bali mtu akisema hivyo, sisi wote tunaelewa, huwa anamaanisha kwamba, yeye anaishi Ubungo au anaishi Kinondoni au anaishi Mbagala au anaishi katika huo mtaa alioutaja. Kwa uelewa huu, huu mstari tuliousoma katika Zaburi 22:3 kwamba Mungu anaketi katika sifa za watu wake, haumaanishi tu kwamba Mungu ameweka kiti chake katika sifa za watu wake, kwa kuziheshimu sana; bali pia mstari huu unaweza kumaanisha kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake.


Kwa dhana hii au kwa uelewa huu, utaanza kuiona sifa na ibada kitofauti. Naamini utaiona sifa na ibada kuwa ni sehemu muhimu sana ya maisha yako na utaiheshimu sana kama vile Mungu anavyoiheshi; kwani Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Na hii ndio sababu kubwa inayomfanya Mungu kupenda sana sifa za watu wake na si hivyo tu, bali hata kutaka sana kufanyiwa sifa na ibada na watu wake. Na ndio maana Mungu anatuamuru sisi wote tulio viumbe wake, kumsifu na kumwabudu yeye kila siku ya maisha yetu; na hii si mpaka iwe siku maalumu ya ibada kama vile Jumapili, No! Bali ni kila siku ya maisha yetu. Narudia tena kusema kwamba, kila siku ya maisha yetu, ni siku ya ibada, na inatakiwa tuichukulie hivyo.

Ni muhimu sana mtu wa Mungu uelewe hilo na upange vizuri ratiba zako kwa kila siku ili uweze kuishi katika kumpendeza Mungu. Usingoje kumwabudu na kumsifu Mungu siku ya Jumapili tu au katika siku maalumu iliyopangwa na kanisa lako ili kukutanika ibadani, haapanaaa! Mungu anataka tuwe tunakutana naye kila siku katika sifa na ibada. Kwahiyo, jenga nidhamu ya kukutana na Mungu kwa sifa na ibada, katika nyumba yako au katika chumba chako au katika mahali popote patulivu, utakapopachagua wewe. Mungu wet anataka tuwe na nidhamu ya kukutana naye ‘kila siku’ katika sifa na ibada. Kama ulikuwa hujui, sasa umejua. Ibada kwa Mungu inatakiwa iwe kiiiiila siku.

Kwahiyo, kama nilivyosema hapo juu, ni muhimu sana mtu wa Mungu uelewe hilo na upange vizuri ratiba zako kwa kila siku ili uweze kuishi katika kumpendeza Mungu. usimalize siku nzima pasipo kupata muda wa kukaa mbele za Mungu na kusema naye juu ya uzuri wake na utukufu wake. Panga ratiba zako vizuri, na uuheshimu muda wa kukaa mbele za Mungu. kama unataka Mungu akuheshimu mtaani au duniani, hebu na wewe mwonyeshe kwamba, unamheshimu kwa muda wako. Narudia tena kusema, hebu usingoje kumwabudu na kumsifu Mungu, siku ya Jumapili tu au katika siku maalumu iliyopangwa na kanisa lako ili kukutanika ibadani, haapanaaa! Fahamu kwamba, Mungu anataka tuwe tunakutana naye ‘kila siku’ katika sifa na ibada. Habari ndio hiyo!

Na Mfalme Daudi alilielewa kusudi hili la Mungu juu ya maisha yake, kwamba yeye ameumbwa awe kama chombo cha kumsifu na kumwabudu Mungu siku zake zote za maisha yake, maadam tu, anaishi. Na Daudi alilitimiza kusudi hili vizuri. Na ndio maana anaandika kwamba; Halleluyah! Ee nafsi yangu, umsifu Bwana. 2 (Nami Daudi) Nitamsifu Bwana, muda ninaoishi, nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.” (Zaburi 146: 1-2)
Sifa na ibada ni kama mahali pa maisha ya Mungu
Kwa wale mnaoweza kusoma Biblia za kiingereza, utaona katika baadhi ya tafsiri za Biblia za kiingereza, mstari huu umeandikwa kwamba ‘Mungu ana inhabit the praises of Israel, yaani Mungu ana-ishi katika sifa za watu wake. Hili neno ku-inhabit linatokana na neno la kiingereza la habitat. Na kwa wale mliosoma biology ya form one (sayansi ya viumbe ya kidato cha kwanza), mtakumbuka kwamba Habitat – is a special place where living things are found naturally. Yaani, ni mahali maalum, viumbe wa hupatikana kuishi kwa asili. Kwa mfano; Siku Nuhu alipofungua mlango wa safina, hakuhitaji kuwaambia wanyama waende wapi na wapi, bali kila mnyama alijua pa kukimbilia; kila mnyama alikimbilia katika mahali pake maalumu pa kuishi, kutokana na ile asili yake, aliyopewa na Mungu. 
Naamini uakumbuka habari za Mzee Nuhu, aliyejenga safina na kuingiza wanyama wote huko ndani. Kisha Mungu akafungulia maji, na dunia ikazamishwa majini kwa muda wa siku zaidi ya arobaini. Siku Nuhu alipotoka katika safina, na akaufungua mlango wa safina, wananyama wote walitoka na kuanza kuimbia, kila mnyama kalilekea katika mahali pake maalum kwa makazi yake, sawa sawa na asili ambayo Mungu amewaumbia. Tunasoma kwamba, Nuhu hakuhitaji kuwaelekeza wanyama mahali pa kwenda, bali kila mmoja, sawa sawa na alivyoumbwa, alivutwa na asili yake kuelekea kule ambako kwa asili, ndiko maisha yake yalipo.

Nuhu hakuhitaji kumwambia samba, chui, fisi, twiga, tembo na nyani waende wapi, bali kila mmoja wao, sawa sawa na alivyoumbwa na Mungu, alivutwa na asili yake kuelekea kule ambako kwa asili, ndiko maisha yake yalipo; kila mmoja alivutwa kwenda katika habitat au habitation yake. Pia, Mzee Nuhu hakuhitaji kumwambia chura, kobe na mamba waende kuishi wapi, bali kila mmoja wao, sawa sawa na alivyoumbwa na Mungu, alivutwa na asili yake, kwenda kuishi kule ambako kwa asili, maisha yake ndipo yalipo; kila mmoja alivutwa kwenda katika habitat au habitation yake.

Wanyama wote walioumbwa kuishi maporini na msituni, walikimbilia huko kwa asili yao, bila kupelekwa. Na ndege wote walioumbwa kuishi maporini na msituni, walikimbilia huko kwa asili yao, bila kupelekwa na mtu. Hiyo ndiyo maana ya habitat ua habitation, ni mahali maalum kwa maisha ya viumbe, kwa asili zao, bila kupelekwa na mtu yeyote.

Lakini pia, Mzee Nuhu hakuhitaji kumwambia mbwa, kuku na njiwa waende wapi, bali kila mmoja, sawa sawa na alivyoumbwa, alikamatwa kubaki pale pale pamoja na familia ya Mzee Nuhu. Kwa asili ya wanyama hawa, Mungu aliwapa kubaki kuishi na binadamu; kwani ndiko ambako kwa asili, ndiko maisha yao yalipo; wameumbwa kuishi na sisi. Na ndio maana, kuna njiwa pori na njiwa wa kawaida. Pia kuna mbuzi pori (swala) na mbuzi wa kawaida. Na mbwa pia, kuna mbwa wa porini (fisi) na kuna mbwa wa kawaida. Hata na paka, kuna paka porini na paka wa kawaida. Wa pori ni waporini, lakini, wa kawaida ni wa nymbani kwa binadamu; wameumbwa kuishi na binadamu. Na wanyama hawa wote wana, wale wa porini na hawa wa kawaida, wana tabia tofauti kabisa. Wa porini hawafugiki, bali wa kawaida, wanafugika; ndivyo Mungu alivyowaumba.

Kwahiyo, siku ile maji ya gharika yalipokauka juu ya uso wa dunia, Mzee Nuhu hakuhitaji kumwambia mbwa na kuku na njiwa waende wapi, bali wanyama wote hawa, sawa sawa na asili yao waliyoumbiwa, asili yao iliwakamata kubaki pale pale, kuishi pamoja na familia ya Mzee Nuhu; kwasababu, kwa asili ya wanyama hawa, Mungu aliwapa kubaki kuishi na binadamu; kwahiyo, ndiko ambako maisha yao yalipo; mbwa, paka, kuku, bata, mbuzi na njiwa (na wanyama wengine wa kawaida ambao sijawataja) wameumbwa na Mungu kuishi na sisi. Kwa lugha ambayo nimekuwa nikiitumia, wanyama hawa, habitat au habitation yao ni pale binadamu alipo. Hiyo ndiyo maana ya habitat au habitation.

Kwahiyo, Habitat – is a special place where living things are found naturally; yaani, habitat ni mahali maalum, viumbe wa asili hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu. Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit sifa za Israel, ina maanisha kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Ngoja niongee kwa mifano ya kibinadamu, ili unielewe vizuri zaidi; maana mwalimu bila mifano, shule haiingii vizuri. Ookeey! Kwa Mfano, kama vile samaki kwa asili yake, anavyoishi katika maji, na ndivyo ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Au, kama vile miti, kwa asili yao iliyoumbiwa na Mungu, inavyoishi katika ardhi au katika udongo, ndivyo  ambavyo Mungu anavyoishi katika sifa na ibada za watu wake; Na kama vile binadamu, kwa asili yetu, tulivyoumbw kuishi katika hewa, ndivyo ambavyo Mungu anavyoishi katika sifa na ibada za watu wake.


Ngoja niongee kwa lugha ya kibinadamu kabisa; Jamani, najaribu kusema hiviii, kama Mungu angekuwa samaki, basi sifa na ibada ndio yangekuwa maji kwa Mungu; Kama Mungu angekuwa mti, basi sifa na ibada ndio ungekuwa udongo kwa Mungu; na kama Mungu angekuwa binadamu, basi hii hewa ya oxygen tunayoivuta, ndio ingekuwa kama sifa na ibada kwake. Jamani, huu ni mfano tu, sijasema kwamba, Mungu wetu ni samaki au ni mti; No! No! No! msije mkanitenga na kanisa. Nimeongea tu kwa lugha ya kibinadamu, ili uweze kuelewa kirahisi uthamani na umuhimu wa sifa na ibada kwa Mungu wetu.

Kwahiyo basi, kutokana na ule mstari tuliousoma katika kitabu cha Zaburi 22:3 unaosema; ‘Nawe U Mtakatifu, Uketiye (au an-inhabit) juu ya sifa za Israeli’. Tumeona kwamba, lile neno ‘unaketi katika sifa za watu wako, lina maana kubwa sana. Tumeona kwamba, katika tafsiri zingine za Biblia, neno hilo linamaanisha ‘unaishi katika sifa za watu wako’. Na kwa kiingereza, Biblia zingine zimesema kwamba, Mungu ana-inhabit sifa za watu wake. Na kama Mungu inhabit au anaishi katika sifa na ibada za watu wake, basi uwe na uhakika kwamba, sifa na ibada kwa Mungu ndio kitu cha thamani kuliko vyote. Kwasababu, kama sifa na ibada ndiyo mazingira ya Mungu ya kuishi (yaani ‘Habitation’ yake), basi hiki ndicho kitu cha maana zaidi na ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu. 

Kwa Mfano wa Samaki;
Piga picha mwenyewe, kitu cha kwanza na cha thamani zaidi kwa maisha ya samaki ni nini? Mimi naamini kwamba maji ndio kitu cha thamani zaidi kwa samaki, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu maji ndio mahali yalipo maisha au habitation/habitat ya samaki. Ukimnyima samaki maji, unamtakia mauti tu. Atakufa! Kwahiyo, hakuna kitu kingine chochote kilicho cha thamani na umuhimu mkubwa kwa samaki kama maji.

Vivyo hivyo kwa Mungu wetu; kwasababu Mungu anaishi katika sifa za watu wake au ana-inhabit  sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3 inavyosema. Hivyo basi, kwa ukweli huu, nakwambia kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana.
Hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mugnu ana-inhabit  sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3 inavyosema. Hiyo ndiyo maana ya habitat au habitation. Habitat – is a special place where living things are found naturally; yaani, habitat ni mahali maalum, viumbe wa asili hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu.

Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit sifa za Israel, ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba, hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote.

Kwa Mfano wa Mimea au Miti;
Hebu jiulize mwenyewe, hiviiii, kitu cha kwanza na cha thamani zaidi kwa miti ni nini? Jiulize tu. Mimi naamini kwamba udongo na maji ndio vitu vya thamani zaidi kwa miti au maua au mimea, kuliko kitu kingine chochote; hii ni kwasababu udongo na maji ndio mahali yalipo maisha au habitation/habitat ya mimea yote. Kwahiyo, hakuna kitu kingine chochote kilicho cha thamani na umuhimu mkubwa kwa miti na maua na mimea kama udongo na maji.

Vivyo hivyo kwa Mungu, kwasababu Mungu anaishi katika sifa za watu wake, basi katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa, kwasababu Mungu anaishi katika sifa na ibada. Kusifiwa na kuabudiwa ndiyo haja yake kubwa. Kama nilivyosema hapo kwanza, huko mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana. Hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote.

Kwa Mfano wa Mtu au Binadamu;
Hebu jiulize tena, hiviiii, katika vitu vyooooote vilivyopo duniani, kitu cha kwanza na cha thamani zaidi kuliko vyote kwa binadamu ni nini? Jiulize tu. Fikiria vizuri kabla ya kujibu. Je ni ardhi? Je ni nyumba? Je ni chakula? Mimi naamini kwamba, kitu cha thamani zaidi katika maisha ya mwanadamu, si chakula, bali ni hewa (yaani oxygen). Hewa ndio vitu vya thamani zaidi kwa mwanadamu, kuliko kitu kingine chochote, kuliko hata chakula. Hii ni kwasababu mahali popote penye hewa ya ‘oxygen’, ndipo mahali yalipo maisha ya mwanadamu wote. Sikiliza, mtu anaweza kukaa dakika 5 bila kula chakula, lakini mtu hawezi kukaa dakika s bila kuvuta hewa; lazima atakufa! Kwahiyo, hewa ndio vitu vya thamani zaidi kwa mwanadamu, kuliko kitu kingine chochote, kuliko hata chakula. Kwahiyo, hakuna kitu kingine chochote kilicho cha thamani na umuhimu mkubwa kwa binadamu, kama hewa.

Kwa Mungu, kitu cha thamaani zaidi kuliko vyote, ni sifa na ibada.
Kwa mifano hiyo yoooooote tuliyoiona hapo juu, basi ni vivyo hivyo na kwa Mungu; kwasababu Mungu anaishi katika sifa za watu wake, basi katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa; iko hivyo kwasababu, Mungu anaishi katika sifa na ibada za watu wake. Kutokana na ule mstari tuliousoma katika kitabu cha Zaburi 22:,3 unasema; ‘Nawe U Mtakatifu, Unaishi  (unaketi) juu ya sifa za Israeli’. Kwa hiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo haja  kubwa zaidi ya Mungu kuliko kitu kingine chochote. Kama nilivyosema hapo kwanza, huko mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana. Hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote. 
Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote. Na ndio maana, hata kule mbinguni, tutakapofika, hatutafanya kitu kingine zaidi ya kumsifu na kumwabudu Bwana; hiyo inaonyesha kwamba, sifa na ibada ndio kitu cha thamani zaidi kwa Mungu, kuliko kitu kingine chochote, kwasababu Mungu anaishi katika sifa na ibada za viumbe wake; au kwa ile lugha yetu tuliyojifunza, Mungu ana-inhabit  sifa za watu wake, kama Zaburi 22:3 inavyosema. Hiyo ndiyo maana ya habitat au habitation. Habitat – is a special place where living things are found naturally; yaani, habitat ni mahali maalum, viumbe wa asili hupatikana kuishi kwa asili zao, pasipo kupelekwa na mtu. Kwahiyo Biblia inaposema Mungu ana-inhabit sifa za Israel, ina maana kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Hivyo basi, kwa ukweli huu, ni muhmu sisi viumbe wake tujue kwamba, hakuna kitu kama sifa na ibada, katika moyo wa Mungu. Kama nilivyosema hapo juu kwamba, katika vitu vyote, hakuna kitu kingine cha thamani kwa Mungu, kama kusifiwa na kuabudiwa. Kwahiyo, kusifiwa na kuabudiwa ndiyo shauku ya Mungu ya kwanza na tena ndio hamu iliyo kubwa zaidi kuliko vyote.








YAFAHAMU KWA UNDANI HAYA-; SILOAM SHIKA NENO TENDA NENO

Ukiwa ni muda wa majuma mchache umepita tangu kifo cha kiongozi mkuu wa kanisa la POOL OF SILOAM nabii Eliya Munuo ali maarufu Adamu wa Pli wa kiazi hichi cha mwisho.
   Yapo mambo mbalimbali yenye utata amabyo yanaendelea kujitokeza na huku kikiwaacha watu wengi wakiwa na hari ya sintofahamu katikavichwavyao na maswaliyaokukosa majibu ya uhakika maana muhusika mwenyewe tayari kisha toweka.

Pamoja na hayo yote yapo mambo ambayo ulikua huyajui/kuyafahmu kuhusiana na kanisa hilo,ndipo sa mwandishi wetu anachukua nafasi hii kukujuza yanayo onekana kuwa yako tofauti na vile ambavyo wengi wamezoea kuyaona au kuyasikia.

Huduma hiyo iliyokuwapo tangu muda lakini imejipatia umaarufu mnamo mwaka wa 2013 ikiwa makao yake makuu yapo Mbezi Beach Makonde jijin Daresalaam Tz Mwanzilishi wa kanisa hilo Eliya Munuo Adam wa pili mungu wa majeshi alipokea mwito wa kumtumikia mungu wa kweli mnamo mwaka 2003 huku akiachana na kazi yake ya uhandisi katika shilika laughavi wa umeme Tanzani Tanesco.

Aliendelea mbele zaidi na kumtumikia Mungu wa majeshi huku misingi mbali mbali ya dini hiyo akiendelea kupanda katika nchi ya Tanzania na duniani kote Adamu wa pili akiwa na mwito tofauti tofauti juu ya imani hiyo huku akiamini imani/madhehebu haya yaliyopo sasa waumini na vingozi wao wamepotoka.

 Kwa muktadha huo sasa yapo mambo mbalimbali ambayo aliyaweka/kuyanzisha na yale yaliyo kuwepo kuyageuza kama Mungu wake alivyo muamuru yafanyike.

KUPINGA JINA BIBLIA TAKATIFU
  Jambo hilo hufanyika tu mara pale ambapo muumini mpya anapokua ameeingia kanisa hilo analazimika kukabidhi Bibilia yake yaani ya Biblia takatifu kwa uongozi wa kanisa hilo na wao huchukua hatua ya kutoa kava ya biblia hiyo na kuweka kava mpya mpya NYEUPE yenye jina la Kitabu cha Bwana.

   KUBADILI SIKU YA KUABUDU    
            Kiongozi huyo alilazimika kubadili siku ya kuabudu kutoka jumapili na kuwa juma nne.

TAREHE KATIKA MWEZI
  Kanisa hilo lina amini kuwa siku za mwezi ni 28 na si 29,30 wala 31
wanaamini kuwa siku ya 28 ni sahihi kabisa na ndyo maana wanawake mzunguko waopia huanzia siku ya 28.Halizaidi zinaendelea mbele zaidi ambapo mnamo mwaka 2008 kanisa hilo lili chapisha kitabu kinachsema mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi,na mwisho wa mwaka si si disemba bari ni Februari.
     
KUBADILI JINA LA AWALI
  Kanisa hilo humtaka muumini mpya anapokua amejiunga na dini hiyo kubadili jinalake la mwanzo na kubatizwa upya na kufuata maagizo ya dini hiyo(ni lazima kubadilisha jina)

  MISIMAMO JUU YA MAADHIMISHO MBALI MBALI
           Kanisa hilo halifungamani na kukubari siku za maadhimisho ya kitaifa kama Siku ya Ukimwi duniani,siku ya kifua kikuu duniani,siku ya wanawake duniani nk.

       KUVAA NGUO NYEUPE
             Watu wote wanalazimika kuvaa nguo nyeupe wakati wa ibada kama ishara ya utakatifu na kumuonesha Mungu Eliya ni mtakaifu na watoto wake ni watakatifu..

           KAULI MBIU/SALAM
              Salamu yao ni Shika neno tenda neno kama ishara ya kuamini uzima upo katika neno kwa lolote hufanyika kwa neno..

Eliya Munuo -katikati pichni.   Shika neno tenda neno
Adamu wa pili  ELIA MUNUO -Shika neno tenda neno
Kwa misimamo hiyo na halihiyo inapelekea baadhi ya waumini wa madhebu mengine kama ya RC,KKKT na MORAVIANI  kulihusisha kanisa hilo na miondoko ya kishetani wakidai kuwa kugeuza kile ulicho kikuta babu zako wanafanya na wewe ukakiita ni upotofu basi moja kwa moja kuna mafungamano ya Kipepo hapo. 

Friday, 21 November 2014

MWIMBAJI NYOTA WA NYIMBO ZA INJILI AFARIKI DUNIA

PIGO KWA TASNIA YA MUZIKI WA INJILI TZ...

Tasnia ya muziki wa injili leo imempoteza mwimbaji wake nyota na mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti Mtoni almaarufu kama Lulu choir kutoka kanisa la Kilutheri, George Bonge Njabili aliyefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

                                                           George enzi za uhai wake

Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema, marehemu George alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam wakati akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda mrefu na mwimbaji huyo kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.

Marehemu George atakumbukwa kwa huduma yake njema ya uimbaji kupitia kwaya ya Lulu ambako aliongoza nyimbo mbalimbali ukiwemo Around the corner Jesus coming, Tazameni Upendo huu, Haleluya na nyingine nyingi huku akiipamba vyema DVD ya kwanza ya kwaya hiyo iliyobebwa na wimbo wa Lulu. Ni takribani miaka mitatu sasa toka aliyekuwa mwalimu mkuu wa kwaya ya Lulu kufariki dunia, kifo ambacho wengi walidhani aliyefariki ni George kiasi kwamba taarifa za kifo chake hii leo kimepokelewa kwa tofauti hasa baadhi ya watu wakidhani alishafariki siku nyingi.

Marehemu George Njabili almaarufu kama George Bonge akiwa na mkewe enzi za uhai wake

SOMO: KWANINI KUSIFU NA KUABUDU


KWANINI KUSIFU NA KUABUDU
utangulizi
Zaburi  100:1-5  
            “1Mfanyieni Bwana shangwe dunia yote; 2Mtumikieni Bwana kwa furaha, njooni mbele zake kwa kuimba; 3Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu, ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake, tu watu wake na Kondoo wa malisho yake. 4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu, mshukuruni lihimidini jina lake5Kwa kuwa Bwana ndiye mwema, rehema zake ni za milele, na uaminifu wake, vizazi na vizazi.

Zaburi 146: 1-2
1Haleluyah. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana. 2Nitamsifu Bwana,
muda ninaoishi,  nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.”

Mtumishi wa Mungu, Mfalme Daudi, anaandika Zaburi hizi kwa ufunuo alioupata, juu ya kusudi la Mungu kwa wanadamu. Mfalme Daudi alipewa kuelewa kwamba, sisi wanadamu wote ni kazi ya mikono ya Mungu, na tumeumbwa ili kumtolea Mungu sifa na ibada, siku zote za maisha yetu. Mfalme Daudi alipopata ufunuo huu na kuelewa jambo hili, akaandika Zaburi hizi tulizozisoma, ili kutufahamisha na kutuhamasisha watu wote, kumsifu na kumwabudu Mungu, kwani ndio wito wetu mkuu. Lakini ukiangalia jinsi wanadamu wengi tunavyoishi, utagundua kwamba, si watu wengi waliopo duniani, wameelewa kitu ambacho Mfalme Daudi alielewa; si watu wengi tunaoishi, tumeelewa kusudi hili la Mungu juu ya Maisha yetu, kwamba sisi wote ni viumbe wa kumsifu na kumwabudu Mungu wetu.

Si watu wengi wanaoelewa kwamba, sisi binadamu ni vyombo maalumu vya kumpa Mungu sifa na ibada. Na ndio maana watu wengi huwa hawana desturi ya kumwabudu Mungu kila siku. Watu wengi angalau wanamwabudu Mungu kwa kiasi katika maisha yao, ni wale wanaomwabudu Mungu mara moja kwa wiki; ni watu ambao huwa wanaosubiri mpaka ifike siku maalum iliyopangwa kwa ajili ya ibada, kwa mfano siku ya Jumapili, ndipo utawaona wana kazana kwenda makanisani kusali.


Lakini laiti kama wangejua kwamba, Mungu anatarajia na anatazamia sana, watu wake tuwe tunakutana naye kila siku katika ibada za binafsi, basi watu wengi zaidi wangekuwa na desturi ya kumwabudu Mungu kila siku katika nyumba zao au vyumbani mwao. Tatizo kubwa la watu wengi ni kutokujua; na ndio maana watu wengi hawapatikani ibadani; hata katika nyumba zao, watu wengi hawana muda wa kukaa mbele za Mungu, ili kumsifu na kumtukuza muumba wao, kila siku baada ya kazi zao kwisha. Bali watu wengi huwa wanaosubiri mpaka ifike siku maalum ya kwenda ibadani, kwa mfano siku ya Jumapili, ndipo utawaona wanajiandaa na kwenda kusali. Hii si sawa. Jamani, kwa wale ambao mlikuwa hamfahamu, basi ni muhimu sana ujue kwamba, sisi binadamu na viumbe wote, ni vyombo maalumu vya kumpa Mungu sifa na ibada kila siku.  Hii ndio sababu ya sisi kuumbwa na kuishi.


Lakini, cha ajabu ni kwamba, watu wengi huwa hawafanyi bidii sana kutenga muda au kutafuta muda wa kukaa mbele za Mungu na kumsifu na kumwabudu yeye. Hali hii inatokana na kutoelewa kwamba, binadamu tumeumbwa kama vyombo maalum vya kumsifu na kumwabudu Mungu, kila siku. Na ndio maana Mfalme Daudi alipewa ufunuo huu na Mungu, ili tuweze kujua kwamba, sisi binadamu wote na viumbe vingine vyoote, ni vyombo maalumu vya kumpa Mungu sifa na ibada kila siku.  Hii ndio sababu ya sisi kuumbwa na kuishi.


Na Mfalme Daudi alijaliwa kulielewa jambo hili, na ndio maana kila wakati alitembea na kinubi chake, akimsifu Mungu wake nyakati zote. Biblia inatuambia kwamba, Daudi alikuwa mchunga mbuzi, kondoo na ng’ombe wa babake; lakini na huko porini nako, Daudi alikuwa akichunga wanyama wake huku akimwimbia Mungu wake kwa furaha, akimpigia na muziki kwa kinubi chake. Daudi alielewa kusudi la Mungu juu ya maisha yake. Pamoja na majukumu mengi aliyokuwa nayo, lakini bado Mfalme Daudi alijitahidi kuishi maisha ya ibada, bila kujali mazingira aliyokuwepo.

Ni muhimu tujue kwamba, Mungu ametuumba sisi na viumbe wote, ili tutimize mapenzi yake au matakwa yake au mahitaji yake, amabyo ni kusifiwa na kuabudiwa. Hii ina maana kwamba, Mungu anataka kusifiwa na Mungu anataka kuabudiwa. Kwa Mungu, sifa na ibada ni vitu vya muhimu sana, Mungu anaheshimu sana sifa na ibada. Na Mfalme Daudi alilielewa kusudi hili la Mungu juu ya maisha yake, kwamba yeye ameumbwa awe kama chombo cha kumsifu na kumwabudu Mungu siku zake zote za maisha yake, maadam anaishi. Na Biblia inasema kwamba Daudi alilitimiza kusudi hili vizuri. Na ndio maana tunaona anaandika katika kitabu cha Zaburi zake kwamba;
1Halleluyah! Ee nafsi yangu, umsifu Bwana. 2 (Nami Daudi) Nitamsifu Bwana, muda ninaoishi, nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.”
                                             Zaburi 146: 1-2

Si watu wengi wanaojua kwanini Mungu anaheshimu sana na anapenda sana ibada na sifa. Na hivyo basi, si watu wengi wanaojua kwanini Mungu anataka na ameagiza kusifiwa. Na ndio maana Mungu amanipa ufunuo huu, ili nikuandikie, ili nawewe uweze kulijua kusudi la Mungu maishani mwako na maishani mwetu sote. Nataka na wewe upate ufunuo huu, ili upate kujua sababu inayomfanya Mungu kuheshimu sana sifa na ibada. Katika kitabu hiki, utaelewa jinsi ambavyo Mungu anaishi katika sifa za watu wake, yaani jinsi Mungu anavyoishi katika sifa na ibada, kama vile Mfalme Daudi anavyoandika katika kitabu cha Zaburi 22:3 kwamba; “Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.”

Kwahiyo, katika sura hii ya kwanza, tumeona kwamba, tatizo kubwa la watu wa Mungu linatokana na kutokujua. Tumeona kwamba, si watu wengi wanaoelewa kwamba, sisi binadamu ni vyombo maalumu vya kumpa Mungu sifa na ibada. Na ndio maana watu wengi huwa hawana desturi ya kumwabudu Mungu kila siku. Na tumeona kwamba, watu wachache ambao angalau wanamwabudu Mungu kwa kiasi katika maisha yao, ni wale wanaomwabudu Mungu mara moja kwa wiki; ni watu ambao huwa wanaosubiri mpaka ifike siku maalum ya ibada, kwa mfano siku ya Jumapili, ndipo utawaona wana kazana kwenda makanisani kusali.

Hii inatokana na kutokujua; na kama watu wanajua hili, basi hawafanyi wanachotakiwa kufanya kwasababu ya uzembe tu na kutokutii. Lakini laiti kama wangejua kwamba, Mungu anatarajia na anatazamia sana, watu wake tuwe tunakutana naye kila siku katika ibada za binafsi, basi watu wengi zaidi wangekuwa na desturi ya kumwabudu Mungu kila siku, huko katika nyumba zao au kule katika vyumba vyao. Kwahiyo tunaweza kusema kwamba, kutokukutana na Mungu mara kwa mara katika ibada, kunatokana na kutokujua (ujinga) na pia, uzembe na kutokutii; ndio maana watu wengi hawapatikani ibadani. Wewe waangalie watu wengi wanavyoishi katika nyumba zao, nakwambia, watu wengi hawana muda wa kukaa mbele za Mungu, ili kumsifu na kumtukuza Mungu wetu. Kila siku baada ya kazi zao kwisha, watu hutumia muda mwingi sana katika kuangalia TV na katika kutembeleana na kupiga soga.
Utakuta watu wanaweza kukaa katika soga na katika TV, kwa masaa mengi. Swala la kumtumikia Mungu kwa sifa na ibada, halipo katika ratiba zao za kila siku. Ibada imekuwa kitu cha mara moja kwa wiki; watu wengi huwa wanaosubiri mpaka ifike siku maalum ya kwenda ibadani, kwa mfano siku ya Jumapili, ndipo utawaona wanajiandaa na kwenda kusali. Jamani, hii si sawa. Kwahiyo, kwa wale ambao mlikuwa hamfahamu, basi nimewaandikia kitabu hiki, tena kwa umuhimu sana, ili ujijue kwamba, wewe ni chombo cha ibada mbele za Mungu. Ni muhimu sana tujue kwamba, sisi binadamu na viumbe wote, ni vyombo maalumu vya kumpa Mungu sifa na ibada kila siku.  Hii ndio sababu ya sisi kuumbwa na kuishi.

Na ndio maana Mfalme Daudi alipewa ufunuo huu na Mungu, ili tuweze kujua kwamba, sisi binadamu wote na viumbe vingine vyoote, ni vyombo maalumu vya kumpa Mungu sifa na ibada kila siku. Jamani, hii ndio sababu kubwa na ya kwanza, kwanini sisi tupo duniani. Na Mfalme Daudi alijaliwa kulielewa jambo hili, na ndio maana kila wakati alitembea na kinubi chake, akimsifu Mungu wake nyakati zote. Pamoja na majukumu mengi aliyokuwa nayo, lakini bado Mfalme Daudi alijitahidi kupata muda wa kumsifu na kumwimbia Mungu.

Jamani, Daudi anatufundisha jambo kubwa sana hapa. Yaani pamoja na majukumu mengi aliyokuwa nayo kama Rais wa nchi, lakini bado Mfalme Daudi alijitahidi kupata muda wa kuishi maisha ya ibada, bila kujali mazingira aliyokuwepo. Najaribu kupiga picha mawazoni kwangu, jinsi Daudi alivyokuwa akizama katika sifa na ibada. Napiga picha jinsi alivyokuwa akitembea huku akiimba. Naweza kuona jinsi Daudi alivyokuwa akiswaga wanyama wake huku akiimba nyimbo za kumsifu Mungu wetu. Naona jinsi ambavyo alikuwa akifua nguo huku midomo yake ikibubujisha sifa. daudi alikuwa akipika chakula huku akimsifu Mungu. Daudi alikuwa akifagia nyumba au banda la kuku au zizi la ngómbe huku akimsifu Mungu.

Na kwa wale mlioko maofisini, hamna jambo la kujitetea, mwenzenu Mfalme Daudi pia, alikuwa akifanya kazi za kuandika huku akimnong’oneza Mungu maneno ya sifa. Jamani, huyu alikuwa Rais wa nchi, tena ni nchi yenye vita nyingi na mapigano makaki, kushoto na kulia, mpaka hivi leo! Sembuse wewe ambaye hata Ukatibu kata hauna! Lakini pamoja na kwama alikuwa kiongozi wa nchi nzima, bado pamoja na ubize (busy) wote aliokuwa nao, na mapigano yote waliyokuwa nayo, bado Mfalme Daudi alijitahidi kupata muda wa kujihudhurisha na kukaa katika uwepo wa Mungu na kumsifu na kumwimbia Mungu wetu. Na kwa saluti kabisa mimi ninampongeza sana kwa kusema, Mheshimiwa Mfalme Daudi alikuwa chombo cha sifa! Jamani, ni muhimu tujue kwamba, Mungu anaishi katika sifa za watu wake. Mungu anaishi katika sifa na ibada, kama vile Mfalme Daudi alivyoandika katika Zaburi 22:3 kwamba; “Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.” Hivyo, Mungu ametuumba sisi na viumbe wote, ili tutimize mapenzi yake au matakwa yake au mahitaji yake, amabyo ni kusifiwa na kuabudiwa. (Hii nitakuelewesha vizuri katika sura inayokuja). Ndio maana Mungu anataka sana kusifiwa na kuabudiwa. Kwa Mungu, sifa na ibada ni vitu vya muhimu sana.

Kwakweli, Mungu anaheshimu sana sifa na ibada. Na Mfalme Daudi alilielewa kusudi hili la Mungu juu ya maisha yake, kwamba yeye ameumbwa awe kama chombo cha kumsifu na kumwabudu Mungu siku zake zote za maisha yake, maadam anaishi. Na Biblia inasema kwamba Daudi alilitimiza kusudi hili vizuri. Mfalme Daudi alijitahidi kupata muda wa kujihudhurisha na kukaa katika uwepo wa Mungu na kumsifu na kumwimbia Mungu wetu. Na kwa saluti nyingine, ninapiga huku nikisema, Mheshimiwa, His Excellency, President, Daudi wa Yese, alikuwa chombo cha sifa mbele za Mungu!      SOMO LITAENDELEA