Friday, 30 January 2015

JICHO LA MBALI WIKI HII :MAHOJIANO NA JENNIFER MGENDI

JICHO LA MBALI WIKI HII NA JENNIFER MGENDI

 

Akiwa tayari na albamu zisizopungua tano kibindoni, Jennifer Mgendi(pichani) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa injili au kwa kiingereza Gospel nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na umaarufu mkubwa kutokana na kazi yake hiyo ya uimbaji na kumtukuza mola. 
Lakini tofauti moja kubwa ya Jennifer na wanamuziki wengine wa muziki wa injili ni kwamba yeye pia ni mtunzi mzuri wa hadithi za filamu.Baadhi ya filamu alizowahi kutunga ni kama vile Pigo la FarajaJoto la Roho na Teke la Mama. 

Alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 1995.Albam yake ya kwanza iliitwa ‘Nini?’. Baada ya hapo alitoka tena na albamu zake zilizokwenda kwa majina ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu Nakupenda’,'Nikiona Fahari’ na ya hivi karibuni zaidi inayoitwa Mchimba Mashimo. 

Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde. Katika mahojiano haya,Jennifer anakupa kwa undani kuhusu historia yake kimuziki na kibinafsi. Ni kweli kwamba muziki wa injili wa leo ni wa “kidunia” zaidi ya “kiroho”? Anasemaje kuhusiana na hoja hiyo? Je Jennifer anaongeleaje tofauti za muziki wa injili na ule wa Bongo Fleva?Unakubaliana naye? 

Nini mipango yake kwa mwaka huu wa 2009 na ana ushauri gani kwa vijana?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; 


FTBLOG: Karibu Jennifer ndani ya FPCTTEGETA  BLOG. bwana asifiwe?
JM:Amen…
FTBLOG:Kwa kifupi tu unaweza kutueleza historia ya maisha yako?
JM:Nilizaliwa miaka karibu 37 iliyopita hapa hapa jijini Dar es Salaam katika familia ya watoto watatu nikiwa nimetanguliwa na kaka wawili. Nimepata elimu yangu katika mikoa ya Dar es salaam na Tanga. Nilianza uimbaji rasmi mwaka 1995 na hapo katikati nilifanya kazi kadhaa za kuajiriwa kama Ualimu na Ukutubi lakini tangu mwaka 2007 niliacha kazi za kuajiriwa na mpaka hivi leo ninafanya shughuli zangu binafsi.
FTBLOG:Mara nyingi wasanii huwa wanaanza kwa kufuata mfano wa mtu,watu au kitu fulani.Kwa upande wako nini kilikushawishi uingie kwenye muziki wa injili.Je kwenye muziki wa injili ndiko ulikoanzia au ulianzia kwingine halafu ndio ukahamia kwenye injili?
JM:Watu wengi walikuwa wakinivutia sana na kunihamasisha kwa habari ya uimbaji lakini miaka hiyo nilivutiwa zaidi na Jim Reeves na Yvonne Chakachaka ambao walikuwa wananivutia sana.
Nimeanza moja kwa moja kuimba muziki huu wa injili kwa sababu tayari injili (ambayo ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye) ilikuwa imebadilisha maisha yangu. Kwa hiyo sina mwingine wa kumwimbia zaidi ya huyo mwenye Injili yaani Yesu Kristo.
FTBLOG:Kwa faida ya wale ambao hawajafuatilia kwa ukaribu kazi zako,mpaka hivi sasa umeshatoa albamu ngapi,zinapatikana wapi na wewe kama msanii wa muziki wa injili unafanyia wapi kazi zako?
JM:Mpaka sasa nina albam tano za kusikiliza ambazo ni Nini?,Ukarimu WakeNikiona FahariYesu Nakupenda na Mchimba Mashimo. Pia nina video za nyimbo ambazo ni Yesu Nakupenda na Mchimba Mashimo. Hali kadhalika nina matoleo ya filamu ambayo ni Joto la Roho, Pigo la Faraja na Teke la Mama. Sina sehemu maalum ninayofanyia shughuli zangu kwani shughuli zangu sio za kukaa sehemu moja.
FTBLOG:Kumekuwepo na ukosoaji kwamba ninyi waimbaji wa muziki wa injili wa kizazi hiki mnapoteza kabisa uhalisia wa muziki huo.Wanaosema hivyo wanasema kwamba muziki wenu hauna vionjo vya “kiroho” bali umejaa vionjo vya “kidunia” kutokea kwenye midundo yake na wakati mwingine hata kwenye mashairi au ujumbe uliomo.Unasemaje kuhusu ukosoaji huo?
JM:Unajua ndugu yangu siwezi kukanusha wala kukubaliana na hoja yao hiyo. Inawezekana ni kweli wanavyosema na hii inatokea zaidi pale waimbaji tunapokosa kiasi. Hata hivyo “kiroho” kwa mtu mmoja kwa mwingine chaweza kuwa ni “kidunia”.
Kuna watu wengine hata kupiga makofi tu wakati unaimba kwao ni “kidunia”. La muhimu ni kwamba mradi mashairi na ujumbe unampa Mungu sifa na utukufu, binafsi sioni ubaya wowote wa nyimbo za injili kuwa na “midundo” na wala sijawahi kusoma kwenye biblia sehemu inayokataza kupiga midundo sanasana nimesoma Zaburi ikisema “….pigeni kwa ustadi…”.
Kuhusu ujumbe wa kidunia kwa kweli mimi sijasikia mwimbaji wa nyimbo za injili akiimba nyimbo za kidunia maneno yote tunayoimba yamo kwenye biblia au angalau hayapingani na mafundisho ya msingi ya biblia.
FTBLOG: Mara kwa mara kumekuwepo watu ambao aidha wanajaribu kukufananisha na waimbaji wengine wa muziki wa injili kama Rose Mhando,Bahati Bukuku na wengineo.Wengine wamethubutu hata kuwapambanisha.Je uhusiano wako na wanamuziki wengine wa injili ukoje?Mnajiona kama washindani au washirika katika Bwana?
JM:Ni kweli mara zingine wanafanya hivyo lakini nadhani kimsingi tunatofautiana na kila mmoja ana uimbaji wake kwa kadiri ya kipawa au kipaji alichopewa na Bwana. Ila la kufurahisha ni kwamba hatuna tabia ya kushindana kwani kila mmoja kapewa karama kivyake na kubwa zaidi ni kwamba tunatambua kuwa wote lengo letu ni moja, yaani kuujenga ufalme wa Mungu hapa duniani. Kwa hiyo huwa tunashirikiana sio jukwaani tu bali mara nyingine hata katika mambo ya kawaida ya maisha.
FTBLOG: Kwa muda sasa umekuwa mwanamuziki.Unadhani ni mambo gani matatu ya msingi ambayo umejifunza kutokana na kazi yako ya muziki na ambayo unadhani usingeyajua kama usingekuwa mwanamuziki?
JM:1. Nimejifunza nchi yangu na kuifahamu zaidi kwani nimesafiri sana katika mikoa na wilaya nyingi ambazo nisingefika kama sio muziki.
2. Nimejifunza mambo mengi sana yaliyonijenga kiroho kutokana na kualikwa kuhudhuria mikutano, semina na makongamano ya kiroho.
3.Nimejifunza kuishi aina fulani ya maisha yenye kiasi fulani cha nidhamu kutokana na nafasi yangu katika jamii, maisha ambayo pengine nisingekuwa maarufu nisingeishi hivyo.

Sunday, 25 January 2015

IBADANI LEO >SOMO; UMOJA WA NDUNGU KATIKA KANISA

Umoja ni ushirika,ushikamano na uungamano unaofanya kazi pamoja ili kuinua na kuunda jambo flani
     Umoja katika kanisa ni mhimu saana kwani ni kitu kinacho lijenga na kulikuza au kuliongeza.
 Ili kanisa liendelee kukua lazima liwe na umoja.
 Zaburi 133;1-2 Tazama ilivyo vema na kupendeza ndugu wakae pamoja kwa umoja, inaendelea
    Mwimbaji wa Zaburi hii ana ufananisha UMOJA WA NDUGU na MAFUTA  yashukayo ndevuni mwa Haruni na katika pindo vazi la kikuhani.
 
Maswali ya kujiuliza;-
Ni ndugugani hao?
     Ni wale wafanyao mapenzi ya Mungu jamii ya watu watendao mema kama Yesu mwenyewe alivyo sema, Marko 3;31-35

Ni mafutagani hayo? na yanaumhimu gani?
 Ni mafuta ya yaliyo kuwa yakitumika kuwabariki wafalme katika Taifa la Israel kwa kusud maalum kama makuhani Kutoka 30;30.
    Haruni na wanawe walitiwa mafuta ili kutakaswa kuwa makuhani  2,Samweli 2;4
    Malikia - Esta2;12.
 Kutakaswa vitu vyote mbavyo vinakua tayari katika kanisa ni mandarizi ya kuunda Umoja unao kubalika ktika kanisa na ndyo maana mpaka Hekalu lilitakaswa ili kuweka wakfu umoja.

Kwa nini tunaufananisha umoja huu na mafuta yashukayo ndevuni na katika pindo la vazi la Haruni?
  Haruni ndiye likuwa Kuhani wa kwanza katka Taifa la Israel.
  Mungu mwenyewe ndiye aliye mchagua Haruni kupitia Musa ili awe msemaji na kuliongoza Taifa la Israel.

    Sasa Mungu anapoona kanisa linakuwa kwa Umoja na upendo wa kweli na undugu unaongezeka basi yeye BWANA anafurahia sana kama alivyo uweka umoja huo katika ukuhani wa Haruni.Roho mtakatifu aliwekwa wakfu kwa Haruni ili aendelee kuuwasha umoja.

                 Kwanini Tuwe na UMOJA katika kanisa/Faida za UMOJA

1/Kwa kuwa umoja ni mhimu sana katika kanisa ndiyo maana Yesu Kristo alituombea Umoja ili tuwe wamoja kama yeye na Mungu walivyo na umoja, Yohana 17;11.

2/Hapatakuwa na mhitaji katika kanisa. kwani vitu vyote vitafanyika kwa umoja na kusaidia mwingine ambaye hana ili kumuinua kama waivyo fanya kanisa la Kwanza. Matendo ya mitume 2;44-47
.
3/BWANA atazidi kuliongeza kanisa kimwili na Kiroho katika mambo yoote.

4/Upendo wa ndugu utadumu zaidi na zaidi kwani agizo kuu ni Upendo na wala hapatakuwa na chuki katika Kanisa. 1Yohana 2;9-11.
                                   Mwalim,,  NATHAN  VICENT -FPCT TEGETA(MACHINJIONI)

  Mungu alituagiza Umoja na kupendana katika kanisa,Chuki,masengenyo,na kutokujaliana havitakuwapo ilikumtunza Roho mtakatifu ni lazimakuachakutenda Dhambi na kuendelea kuomba misimamo ya kimwili Bila Roho mtakatifu havita saidia kulikuza kanisa. Mungu ameagiza umoja ili kumtambulisha mwenyewe katika Dunia,.
Ubinafsi na kujipenda wenyewe vinaweza kulivunja au kuligawa kanisa.
     Epuka ubinafsi katika Kanisa maana ni chachu ya kuvuruga umoja na kuligawa kanisa. Simama katika mwito wa kweli na ahadi yake kama alivyo ahidi. Watumishi na watuwoote chukua hadhali katika jambo lolote linalo weza kuvunja umoja wa huduma au kanisa.
Simama katika kweli ili Mungu aone uaminifu  wako wa kulinda na kutunza Umoja kaika kanisa au kundi watu wote tunawajibu na haki ya kuulinda umoja wa Roho ktika katika kanisa usipotee. Mungu akubaliki saana uwe na Tafakuri njema Roho mtakatifu akusaidie. Ameeni.
                              By Mwl NATHAN VICENT-FPCT TEGETA.
  

Saturday, 24 January 2015

NEWS:: HIZI NDIO SURA MPYA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


Haya ndio majina ya mawaziri wapya kwenye baraza jipya la Mh Raisi prof Jakaya Mrisho Kikwete kumbe prof Muhongo alikuwa ameshafahamu ukweli ndio maana akajiuzulu mapema< wapya walioingia ni Anne Kilango Malecela na ndugu Charles mwijage....
WALIOTEULIWA
1. George Simbachawene- Waziri Nishati
2.Mary Nagu-Waziri wa Nchi mawasiliano na Uratibu
3.Christopher Chiza-Waziri uwezeshaji na Uwekezaji
4.Halson Mwakyembe-Ushirikiano wa afrika mashariki
5.Lukuvi-Ardhi Nyumba na Makazi
6.Steven Wasira-Kilimo chakula na Ushirika
7.Samwel Sitta -Wizara ya Uchukuzi
8.Jenista Muhagama-Sera na uratibu wa Bunge
MAWAZIRI KAMILI
Simbachawene - Nishati na Madini
Nagu - Mahusiano na urt
Mwakyembe - Afrika Mashariki
William Lukuvi - Ardhi, Nyumba na Makazi
Stephen Wassira - Kilimo
Samwel Sitta - Uchukuzi
Jenista Mhagama - WM SUB
MANAIBU WAZIRI WALIOTEULIWA
S. Masele - Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano
Angela Kairuki - Ardhi na Makazi
Ummy Mwalimu - Katiba na Sheria
Anne Kilango - Elimu
J. Mwijage - Nishati na Madini
Baraza limetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi
 Ombeni Semfue .

Monday, 19 January 2015

TAZAMA PICHA NAMNA JUMAPILI YA BARAKA NA MGUSO WA KIPEKEE ILIVYOTIKISA FPCT TEGETA

Siku ya jumapili ya tarehe 18/01/2015 ilikuwa ni siku ambayo kulikuwa na ibada maalum ya sifa na kuabudu kanisa la fpct tegeta hakika ilikuwa ya kipekee sana ...ibada hii iliandaliwa na idara ya vijana kanisa la fpct tegeta
                           praise& worship team fpct tegeta wakimwadhimisha Mungu
 waimbaji wa nyimbo za injili Kutoka kulia ni Gazuko junior na Crispin  Challe wakiteta jambo kabla                                                           ya kupanda kwenye stage
                                        hapa ilikuwa ni zamu ya kumuabudu mungu



 kutoka kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa idara ya vijana kanisa la fpct Tanzania  akiwa pamoja na           viongozi wa idara ya vijana mission ya msanga na hapa alikuwa anatoa neno kwa vijana
                 kutoka kulia ni mwimbaji Gabilo Hosea akiteta jambo na Baba Ima

                                    sifa na kuabudu mwanzo mwisho
              Mc modo Hossein Gabriel ndiye alikuwa kiongozi wa ibada hiyo maalum
                             kijana Daniel akifanya ufundi kwenye upande huu
                                    Bwana shuka na nguvu zako ututembelee
                                            mch Joram Jeremiah (fpct tegeta)

Wednesday, 14 January 2015

ASKARI MAGEREZA ALIYE NG'ARA KATIKA MCHEZO WA RIADHA NA KUPANDISHWA CHEO

Ni baada ya askari CPL. Catherina Lange  wa gereza kuu mkoani Arusha kulitumikia jeshi la magereza kwa muda mrefu huku akiwa ni mmoja kati ya wakimbiaji wa kimataifa kutoka katika timu za majeshi ya magereza ya hapa nchini Tanzania,. Askari huyo amekua akishiliki mashindano mbalimbali ya riadha ya kimataifa huku akinyakua vikombe vingi vya mashindano ya kimataifa na kitaifa na kulitangaza Taifa na kuliletea sifa jeshi la Magereza.

unnamed1
Kamishna wa Jeshi la magereza JOHN C, MINJA akimvisha cheo cha Sajin wa Magereza  askari  Catherina Lange,.
unnamed2
Kamishina jenelali J, C, Minja akimpogeza askali Cathelini baada ya kumvisha cheo cha Sajin. 
unnamed6

 Jeshi la magereza makao makuu kwakutambua na kuona umhimu wa mchango huo wa Cpl Catherina Lange, Ametunukiwa kupandishwa cheo cha Sajin sawa na askali mwana Riadha wa kimataifa. Cheo hicho amepandishwa na Kamishina jenelali wa jeshi la magereza  John Casmir Minja, katika makaoofisi za makao makuu ya jeshi la Magereza jijini Dar es salaam jana..  

Tuesday, 13 January 2015

HIVI NDIVYO UWANJA WA SOKA WA KAITABA-BUKOBA MJINI UNAVYO ENDELEA KUJENGWA KWA KASI

Taswira mpya ya uwanja wa soka wa Kaitaba mjini Bukoba unavyo  onekana.

TIZAMA PICHA ZA MWIMBAJI PEACE MULU(ombea adui yako)ALIVYO UMIA KWENYE AJALI SIKU 4 ZILIZOPITA.

Akiwa katika harakati za kurekodi albamu ya video mwimbaji Nguri nchini Kenya Peace Mulu ndipo masahibu haya yalimkuta baada ya kupata ajali mbaya na sasa amelazwa katika hosptali ya KENYATA nchini humo, huku akisubilia kufanyiwa upasuaji wa Mguu wake ulio vunjika.. 
Wadau,wapenzi na watu wote kwa ujumla tuendelee kumuombea kwa Mungu ili amponye haraka na kumpunguzia maumivu ya mwili,, Endelea kuomba juu ya mwimbaji huyu.  
Mungu akubariki
Sehemu ya  uso ya mwimbaji PEACE MULU iliyo jeruhika.

Picha ya mguu wa pili wa mwimbaji Peace Mulu alivyo umia
Miguu  miwili ya mwimbaji PEACE MULU ilivyo umia hasa mguu wakushoto uliumiazaidi mpaka mfupa wa paja lake ulivunjika,.

Sunday, 11 January 2015

RIDHIWANI AANZA KUTEMA CHECHE KWA VITENDO..

Mbunge wa Chalinze mhe, Ridhiwani Kikwete (katikati)akikabidhi mganga mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Dr Mastidia Rutaihwa, gari jipya la wagonjwa kwa ajili ya kituo cha afya cha Chalinze wakati alipokua na mkutano wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Chalinze  Mh Ridhiwani Kikwete aanza kutekeleza moja ya ahadizake alizo ziahidi wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi uliopita mwaka jana..

SHEHENA YA BIDHAA FEKI ZA TEKETEZWA- ZANZIBAR

unnamed1r
Watumishi wa idara ya mamlaka ya chakula na dawa nchini Zanzibar wakijiandaa kuteketeza baahi ya bidhaa zilizo kutwa zikiwa hazina ubora.
Oparesheni ya kutokomeza bidhaa zote zilizopo madukani ambazo zimepita muda wake  na kuangamiza bidhaa zote amabazo hazina ubora kwa afya ya binadamu, mamlaka ya chakula na dawa nchini Zanzibar imeanza kwakutembelea duka kwa duka kuhakikisha ubora wa bidhaa zilizopo kama zinaubora, na kuziteketeza bidhaa zote zisizo na ubora. Mamlaka hiyo mpaka sasa imebaini idadikubwa ya bidhaa zilizo isha mudawake na hazina ubora wa matumizi kwa afya ya binadamu.

Saturday, 10 January 2015

UPATIKANAJI WA NISHATI YA UMEME,DAWA YA MAUAJI YA VIKONGWE ASEMA MKUU WA WILAYA

Kauli  hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Vijijini, Anna Rosse Nyamubiambapo , wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini (REA) ambapo amesema katika mkoa wa shinyanga kumekua kukigubikwa na matukio mbalimbali ya mauaji ya vikongwe wakidhaniwa ni wachawi kwavile tu  macho yao ni mekundu kumbe si sahihi wanachofanyiwa..

Ameendelea kusema kuwa upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika utawasadia vikongwe kupika kwa njia za kisasa kabisa kwa kuepuka matumizi ya majiko ya kuni ambayo huwafanya machoyao kuwa mekundu kwa sababu ya moshi wa kuni.

unnamed1r
MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI  BI ANNA ROSSE NYAMUBI(Aliyeshika kipaza sauti) akiimba wimbo wakufurahia kwenye uzinduzi wa mradihuo,hakucheza pekeyake yupo na ananchi wengine.
unnamed2r
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA  SOSPETER MUHONGO AKIWAHUTUBIA WANANCHI WAKATI WA UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI(REA)
 Pamoja na hayo waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amewataka wananchi kujiadhali na vishoka sambamba na wale wote wanao tumia umeme kinyume na taratibu za kisheria''Wanachi tunayo nafasi haki na wajibu wa kuwafichua wote wanaohujumu mali zetu wenyewe kwani tunawafahamu kabisa kwani tunakulanao,tunaishinao pia ni nduguzetu"alisema Waziri Muhongo wakati akizindua rasmi mradi huo..

Thursday, 8 January 2015

HII SI YA KUKOSA NI JUMAPILI YA KIPEKEE NJOO UKUTANE NA MJIBU YAKO

NJOONI TUMSIFU NA KULITUKUZA JINA LAKE MAANA YEYE NDIYE ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI ....NJOO UPATE MSINGI IMARA KATIKA SIKU MUHIMU ....LAZIMA MUNGU ATAZUNGUMZA NA WEWE HAKIKA HII SI YA KUKOSA WAPENDWA

Tuesday, 6 January 2015

NAMNA YA KUMSIFU NA KUMWABUDU MUNGU IPASAVYO



Moja ya sababu ya watu kutomsifu na kumwabudu Mungu ipasavyo, ni kutokujua namna ya kufanya sifa na kuabudu. Mambo/Pointi zifuatazo zitakusaidia kukuwezesha kujua namna ya kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu. Unapokuwa umetenga muda wa kusifu na kuabudu, au unapokuwa katika muda wako wa maombi, tumia ufahamu wako juu ya mambo uliyojifunza kuhusu Mungu, yanayomstahilisha kusfiwa na kuabudiwa. Kwa mfano:-


                                A: MSIFU MUNGU KWA YALE MAMBO YANAYOMSTAHILISHA
1)      Mtukuze Mungu kwa Sifa zake za kipekee ( Sifa zake za Ki-Mungu).
Mweleze jinsi alivyo Mtakatifu, Wa milele, Mwenye nguvu zote, Mwenye akili na ufahamu wote, n.k

2)      Mtukuze Mungu kwa Tabia zake.
Mweleze jinsi alivyo mwenye Upendo mwingi usiopimika, jinsi alivyo na huruma nyingi, jinsi alivyo mwaminifu na wa kweli. Msimulie habari ulizozisikia na ulizozisoma juu ya tabia zake kwetu.

3)      Mtukuze Mungu kwa Matendo yake makuu.
Mweleze jinsi unavyohusudu kazi mbalimbali za mikono yake, uumbaji wake, na matendo yake makuu. Msimulie jinsi unavyokubali ubora wa kazi zake na ukuu wa matendo yake. Msimulie unavyothamini matendo yake makuu kutoka katika biblia au katika shuhuda ulizozisikia katika maisha ya sasa ya kila siku.

4)      Mtukuze Mungu kwa Baraka na Fadhili zake.
Msifu na kumshukuru kwa fadhili na baraka mbalimbali ulizopata kutoka kwake. Kwa zawadi ya uhai, afya njema, uponyaji, ulinzi, chakula, kazi, elimu, fedha, mali, mifugo, mashamba, biashara, n.k. Yako mambo mengi sana, Mungu amekutendea, usiyoweza kumaliza kuelezea. Msifu kwa hayo.
5)      Mtukuze Mungu kwa Ahadi zake nzuri kwetu.
Pia unaweza kumsifu Mungu kwa ahadi zake mbalimbali alizotupa. Ukampamba kwa jinsi alivyokusudia kutubariki, kutuinua, kutulinda, kutushindia, kututetea, kutuwezesha, kutusaidia, n.k.

                                   B:                    MSIFU MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa za Mungu, Tabia za Mungu au Matendo ya Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El-Shaddai. Ni neno lenye majina mawili ndani yake. El’  maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana itokanayo na neno ‘Shad’ yaani Titi (Ziwa) la mama anyonyeshaye.

Kutokana na ukweli kwamba, titi/ziwa la mama anyonyeshaye, linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa ya mama yake, humpa mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna vitamini, protini, wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto anachohitaji. Maziwa ya mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo, Waisraeli wanapomwita Mungu El-Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama ziwa linavyo mtosheleza mtoto, vivyo hivyo, Mungu ni ‘Mtoshelezi’ kwetu. Halleluyah!

Hivyo, kila jina la Mungu, linabeba aidha Sifa yake au Tabia yake au Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi anasema “… Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu … Mpeni Bwana utukufu kwa jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” (Zab 29:1-2) Msifuni Bwana kwakuwa Bwana ni mwema, Liimbieni Jina lake, kwakuwa lapendeza.(Zab 135:3). Unaweza kumsifu Bwana kwa majina yake. Yafuatayo ni baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya Kiebrania, yatakayokusaidia kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu.


                                                                  

                                  -         

TANZANIA BEI YA MAFUTA YASHUKA, EWURA YATAJA BEI MPYA

Mamlaka ya udhibiti wa nishati,maji na mafuta(ewura) imetangaza kushusha kwa bei za mafuta kuanzia kesho (januari 07/2015) kwa nchi nzima. Akizungumza na wanahabari leo ofsini kwake, mkurugenzimkuu  wa mamlaka ya Udhibiti wa nishati,maji na mafuta, bwana Felix Ngamlagosi, jijini Daresalaam,
Sasa amevitaja viwango hivyo vipya vya bei za mafta  kuwa  vitaanza kutumika rasm kesho;-

Bei ya petrol,
      Bei ya petrol kwa lita moja itauzwa kwa tsh,1955 hii nikutokana na kushuka kwa asilimia 6 kwa sawa na tsh 311 upungufu iliyo pungua kutoka kwa bei ya awali.

Bei ya Dizeli
   Pia lita moja ya dizeli itauzwa kwa Tsh,1845 amabapo asilimia zilizo shuka ni 13 sawa na tsh244 zilizopungua kutoka bei ya awali.

Bei ya mafuta ya taa,
 Mwisho mafuta ya taa nayo yatauzwa kwa tsh1833 lita moja.

Baada ya kuvita viwango hivyo vya bei mpya bw Ngamlagosi amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kuomba au kudai risiti ya malipo mara tu wanapo nunua mafuta kila wakati..
Mkurugenzi mkuu wa EWURA Bw, Felix  Ngamlagosi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake alipokua akitaja na kutoa maelezo juu ya kushuka kwa  bei ya mafuta hapa nchini.

Monday, 5 January 2015

RAISI KIKWETE AMWAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Raisi Dr Jakaya Kikwete akimwapisha mwanasheria mkuu wa selikali George Mcheche katika ikulu ya Raisi ambapo ndipo hafla fupi ya kumpongeza ilifanyika.

Ikiwa ni muda mfupi kupita tangu aliye kuwa mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrick Werema ajiudhulu kufuatia sakata la upotevu wa zaidi ya bilioni miatatu kutoka kwenye akaunti ya tegeta Escrow sasa Raisi wa jamhuli ya muugano wa Tanzania Dr Jakaya Mlisho Kikwete amemteua Mwanasheria mwingine atakaye vaa kiatu cha Werema.
      Raisi Kikwete amemteua Georg Mcheche kuwa mwanashelia mkuu wa Tanzania.
Raisi Dr Jakaya Kikwete akisaini mara baada ya kumwapisha mwanasheria mkuu Tanzania  George Mcheche ikulu.
  

Sunday, 4 January 2015

NDANI YA YESU HAKUNA MZEE BI MAGRET AENDELEA KUMTUMIKIA MUNGU KWENYE HUDUMA YA UIMBAJI

Huu ndio msemo unaweza kuutumia kuwa ndani ya Yesu hakuna mzee hii ni baba ya bi Magreti wa kanisa la fpct tegeta kuonyesha uwezo mkubwa akiwa madhabauni anamwimbia Bwana wa majeshi sauti yake husikika kama kijana lakini kumbe umri umesogea hii imekuwa baraka kubwa katika kanisa la fpct kwani watu wengi ndani ya kanisa hilo wamekuwa wakipata darasa kwa bibi hasa waimbaji inatia moyo sana
                                                   bi magreti akiongoza nyimbo za wokovu





Friday, 2 January 2015

HIVI NDIVYO MJI WA MOROGORO ULIVYO PATA SURUBA YA MVUA

Sehem ya soko la Morogoro ilivyo jaa maji huku wakazi wa mji huo na wafanya biashara wakitaabika . 

Kufuatia mvua zinazo endelea nchini hivi ndivyo wafan
ya biashara wa soko la Mjini Morogoro walipata taabu na kushindwa kufanya biashara kabisa kwenye soko hilo kufuatia mvuakubwa zilizo nyesha na kupelekujaa kwa mto Kikundi kupoteza uelekeo wa kutiririsha maji na kisha kuya tiririsha maji yake katika mji wa Morogoro..