WAIMBAJI WAAMUA KUPAMBANA NA UNENE, MWINGINE ATANGAZA NIA -
Baada ya juhudi za mwimbaji nyota wa muziki wa
injili Afrika ya kusini mwanadada Ntokozo Mbambo wa Mbatha kufanikiwa kupunguza
unene kwa asilimia kubwa mwimbaji mwingine wa kundi la Soweto gospel Choir
mwanadada Sipokazi Nxumalo wa Linda nayeye pia ametangaza hapo jana kuamua
kupunguza unene ili awe sawa na Ntokozo.Sipokazi ambaye anafahamika vyema na wapenzi wa Soweto kutokana na uimbaji wake mahiri ndani ya kundi hilo, ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa facebook akieleza wazi kuvutiwa na waimbaji wenzake ambao anavutiwa na sauti zao kwa jinsi walivyoweka juhudi na sasa matunda yameonekana.
Ntokozo
amewashangaza wengi nchini kwao Afrika ya kusini baada ya kufanya mazoezi na
kujinyima kula vitu vyenye mafuta na hatimaye sasa unene aliokuwa nao awali
umepungua ambapo hata sasa mwanadada huyo anayetarajia kuachia wimbo mpya hivi
karibuni ikiwa maandalizi ya album yake mpya bado anakwenda katika vituo vya
mazoezi (gym) na kula chakula bora ili kulinda mabadiliko yake ya mwili ambayo
wengi hususani wanawake wamempongeza
No comments:
Post a Comment