Thursday, 6 November 2014

MUNGU TUEPUSHE NA HAYA ...AJALI MBAYA YATOKEA MOROGORO TISA WAFARIKI DUNIA

WATU TISA WAFARIKI NA AJALI YA GARI HUKO MOROGORO
Zaidi ya watu tisa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya baada ya Basi la Super Aljabir linalofanya safari zake kati ya Morogoro  kugongana na Treni maeneo ya kiberenge karibu na Ifakara Morogoro jioni hii .Ajali hiyo imetokea wakati basi likijaribu kuwahi kuvuka reli kabla ya treni kupita


   TAARIFA ZAIDI ITAKUIJIA HIVI PUNDE

MATOKEO DARASA LA SABA WASICHANA WAFANYA VIZURI ZAIDI YA WAVULANA


NUSU WAFAULU MATOKEO YA DARASA LA SABA
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 yakionyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanafunzi waliofanya mtihani huo Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde yanaonyesha kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi ya wavulana, huku ufaulu kwa jumla ukiwa umeongezeka kwa asilimia 6.38 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Katika matokeo hayo Shule ya Twibhoki iliyopo mkoani Mara iliibuka ya kwanza kitaifa kati ya shule 15,867 zilizofanya mtihani huo ikifuatiwa na Mugini, Peacland na Alliance zote za mkoani Mwanza.

Shule ya tano ni Kwema ya Shinyanga ikifuatiwa na St Severine ya Kagera, Rocken Hill ya Shinyanga, Tusiime ya Dar es Salaam, Imani ya Kilimanjaro na iliyoshika nafasi ya 10 ni Palikas ya Shinyanga.

MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUFIKA KWENYE MAOMBI


MUNGU AKUBARIKI SANA ULIYEHUDHURIA KWENYE MAOMBI                                                     Mungu awabariki watu wote ambao walijitokeza kwenye maombi ya siku tatu hapa kanisani fpct tegeta yaliyofanyika kuanzia siku ya jumatatu na kuhitimisha siku ya jana jumatano, maombi yalikuwa na lengo la kuwaombea wagonjwa wote wanaoteswa na magonjwa mbalimbli hakika naamini kupitia maombi haya Mungu amewafungua Zilikuwa ni siku tatu za kufunguliwa na aliyehudhuria maombi lazima atakuwa amekutana na kitu cha tofauti kabisa  Mimi kama mchungaji wa kanisa la fpct tegeta nawashukuru sana wale wote waliochukua muda wao na kuja kujumuika pamoja katika maombi haya Mungu wa mbinguni awabariki sana.
Mchungaji wa kanisa la fpct tegeta, Joram Jeremiah Ntaseha 

Wednesday, 5 November 2014

MAMBO YA KUFANYA BAADA YA MTU KUAMUA KUOKOKA

YESU APEWE SIFA
  • Sijui kama wewe umewahi kusikia au kushuhudia,lakini mimi nimeshawahi kushuhudia watu wengi waliochukua uamuzi wa kuokoka wakiacha maisha mazuri ya wokovu ndani ya Yesu na kurudia maisha yao ya zamani.Wengine walishaanza hata kumtumikia Mungu kwa huduma mbalimbali lakini wakarudi nyuma.Ni dhahiri kabisa kuwa si mapenzi ya Mungu mtu wake aamue kuokoka halafu arudi tena nyuma.Kiu ya Mungu ni kuona watu wake wanokoka na wakishaokoka waendelee kusonga mbele kwenye maisha ya wokovu mpaka siku ya kufa kwao au mpaka siku Bwana Yesu atakaporudi mara ya pili kama bado watakuwa hai.


    Ni vyema basi wewe ambaye umeamua kuokoka kufahamu baadhi ya mambo yatakayokusadia ili udumu katika wokovu maisha yako yote.

    Baadhi ya mambo yawafanyayo watu wa Mungu kurudi nyuma katika maisha ya wokovu:

    Kutokusoma Neno la Mungu(Biblia) kwa bidii.
  •  
  

Kutokuwa waombaji wa bidii.


  • Kutokuwa na ushirika na waliokoka wengine


  • Kutokupata watumishi wa kuwalea kiroho na kuwatia moyo
  • .

    Kuona aibu kukiri wokovu wao mbele ya wanadamu.


    Mambo ya Kufanya Baada Ya Kuokoka:

    1. Soma Neno la Mungu kwa bidii sana kila siku,mara nyingi iwezekanavyo.Mara baada ya kuokoka wewe ni mtoto mchanga kiroho,Biblia inasema utumie maziwa yasiyoghushiwa(Non-diluted milk)ya kiroho ambayo ni Neno La Mungu(1Petro2:2).Neno la Mungu litakujengea ndani yako nguvu za Mungu za kukuwezesha kudumu katika wokovu siku zote.Ni muhimu basi ujiwekee ratiba yako ya kusoma Biblia yako kila siku na kuhudhuria mikutano na semina za Neno la Mungu wetu.

    2. Kuwa muombaji kwa bidii,Baada ya kuokoka sasa unatakiwa uwe mwombaji sana.Biblia inasema wazi kwenye Yakobo 5:16b:"....Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana kama akiomba kwa bidii",Kinachotakiwa sii kuomba tuu,bali kuomba kwa bidii.Ukimwomba Mungu anasikia na atakujibu maombi yako sawasawa na mapenzi yake.

    3. Acha dhambi;ndugu mpendwa,baada ya kuokoka sasa unatakiwa KUACHA kila dhambi uliyokuwa unaifanya kabla ya kuokoka,unatakiwa uanze maisha mapya kabisa ya kumtukuza Mungu.Ukishaokoka Mungu anakusamehe dhambi zako zote nawe sasa usifanye dhambi tena.Muombe Mungu akupe nguvu zake ile usifanye dhambi tena,hii inawezekana kabisa.

    4. Kuwa na Ushirika na watu wengine waliookoka,ni wazi kuwa watu walio karibu sana na mtu wana uwezo mkubwa sana wa kumbadilisha mtu huyo mawazo yake.Hivyo basi baada ya kuokoka nawe ni muhimu sana ukawa na uhusiano wa karibu sana na watu wengine ambao wameshaokoka,hao watakushauri namna ya kudumu na kukua katika wokovu,watakujibu na maswali ambayo unaweza kuwa nayo.Hata kama watu walijua kama wewe hujaokoka,wafahamishe kuwa umeokoka na kuwa unataka uwe karibu nao.

    5. Kuwa karibu na watumishi mbalimbali wa Mungu,uwaeleze juu ya uamuzi wako wa kuokoka,waombe wakuombee maana ni Kazi waliyopewa na Mungu.Usiwaogope watumishi wa Mungu bali jenga nao urafiki wa karibu sana.Hudhuria Fellowships,mikutano ya Injili na Semina za Neno La Mungu mara kwa mara.

    6. Wafahamishe wenzako kuwa sasa Umeokoka,Ni muhimu sana kuwafahamisha na wengine uamuzi wako wa kuokoka.Hii itakusaidia kwani wakishafahamu kuwa umeokoka hawatakushirikisha tena mambo ambayo ni mabaya(yawe maneno,maandishi,picha au hata matendo)hii itakusadia wewe kukua haraka sana kiroho.

    7. Usife moyo,Ndugu,katika maisha ya wokovu hatutakiwi kuvunjika moyo.Mara baada ya kuokoka inawezekana shetani akataka kukutisha tamaa ya kudumu katika wokovu(kumbuka!shetani hajafurahi kuona wewe umeokoka)ili umrudie yeye.Anaweza akakuletea watu wa kukukashifu ili uacha wokovu au kukushauri uache wokovu au akatumia mbinu zozote zile zikiwemo majaribu mbalimbali.Watu wengi wanafikiri wakiokoka basi ndio haukuna tena majaribu(magumu),mpendwa kuokoka sio mwisho wa majaribu bali ni mwanzo wa majaribu lakini na USHINDI JUU.(Warumi 8:28,37)Unapaswa kufahamu kuwa hakuna jaribu limpatalo mwanadamu Mungu asipotoa njia ya kushinda,kwenye kila jaribu kuna msaada wa Mungu wa kukusaidia,Ukikutana na majaribu hayo wewe dumu kwenye maombi na usirudi nyuma kamwe.

    Hayo ni baadhi tuu ya Mambo ambayo ninapenda uwe nayo unaipoianza safari hii ya wokovu


NYAYO NCHINI KENYA NDANI YA JICHO LA MBALI

Je, wajua nini maana ya NYAYO? na unapo taja neneo Nyayo kwa wakazi wa nchini kenya una maanisha ni

Na unajua ni kwa nni sehemu ya hapo pichani palitwa Nyayo? kwa hayo na mengine Meeng usikose juma mosi hii katika  JICHO LA MBALI.. Ndani ya blog hii

Tuesday, 4 November 2014

JICHO LA MBALI ..SARAH K. ASEMA ALIKATISHWA TAMAA WAKATI WA KUANZA HUDUMA AKIAMBIWA SAUTI YAKE NI YA KIUME NA SI YA UIMBAJI

SARAH K ni muimbaji anayegusa watu wengi hasa kutokana na nyimbo anazoziimba, lakini ni wachache sana wanaofahamu historia ya muimbaji huyo.
Muimbaji huyo aliyezaliwa miaka 42 iliyopita, ameolewa na mchungaji japo kabla ya kuanza huduma ya uimbaji, alishafanya jitihada nyingi maishani ikiwemo kuuza mbogamboga ili mradi maisha yasonge.
Makala haya yanaangazia maisha na mapito magumu aliyoyapitia muimbaji huyo kabla ya kuinuliwa na Mungu.
                                            Mwimbaji wa nyimbo za injili Sarah K

Kabla ya kuanza huduma ya uimbaji, Sara ambaye jina lake kamili ni Sarah Kiriare alikuwa akikusanya fedha kidogokidogo ili apate kuingia studio, ambapo alikuja kufanikiwa na kutoa albamu kwa lugha yake ya asili.

Mbali ya changamoto mbalimbali alizowahi kupitia ikiwemo kukatishwa tamaa na baadhi ya rafiki zake tena wa karibu, ikiwemo kudai kwamba sauti yake haifanani na uimbaji na kwamba ni kama vile anaongea na si kuimba na pia wengine wakisema sauti yake ni ya kiume, jambo ambalo kwa kweli lilimhuzunisha sana, lakini yote hayo hayakumzuia kusonga mbele.

Pamoja na kudharauliwa na kuonekana hafai kwa baadhi ya waimbaji ambao kwa namna moja au nyingine amewafanya kujulikana mbele ya jamii, pia ni jambo ambalo Sarah anaguswa nalo moja kwa moja.



Sarah anasema kuwa suala la kudharauliwa lilikuwa likimliza na kuamua kumlilia Mungu hadi kufikia hapo alipo; ni matokeo ya kusema jambo linamlomsumbua kwa Mungu wake, mathalan msanii mmoja aliyewezeshwa kupitia Sarah, na kisha baada ya hapo maneno yakaanza, ikiwamo kudai kuwa Sarah si lolote wala si chochote kwa maana hajawika kama ambavyo muimbaji huyo aliyewezeshwa kutoka anavyowika.
                                  Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Kenya Sarah K.

Muimbaji huyo ameshawahi kuuza nyanya, magunia, kutembea kwa mguu kwa kukosa nauli, kuimba kwa kukopa pesa ya studio na albamu haitoki kutokana na kuwa na deni kubwa, kutembeza kanda mguu kwa mguu.
“Niseme tu nimeshapitia maisha magumu; nimeshauza nyanya, nimeuza sukuma, nimeuza mangurunya, nimetembea mguu yaani kwa miguu bila ya kupata hela ya kwenda na gari.

“Nimeanza kuimba kwa kukopa pesa; naomba pesa za studio; naenda halafu siuzi kwa hivyo nadaiwa hizo fedha sijui nizitoe wapi.
Nimeshalia, nimeshatembeza kanda zangu zikiwa mfukoni nikipeleka kwa wenye maduka yaani mambo yalikuwa magumu mpaka mahali Mungu akanifikisha nasema asante.”

Sarah K ameolewa na ana watoto watatu na anasema kuwa yeye ni Mkenya; anaeleza sababu za watu wengi kulia akiimba nyimbo zake: “Nimeshaona hivyo tena mara nyingi nikienda kwenye kanisa ambako ninakwenda kuhudumu, ninajikuta hata mimi mwenyewe nalia, kanisa pia hata watu wengi wanalia nadhani kwa sababu wanapata mguso ambao pengine kuna mambo walishapitia, pengine wamekata tamaa yaani ile basi kama vile wanaona Mungu amewasahau lakini niwaambie kuwa Mungu anatuambia tusishughulike sisi wenyewe tusije tukafichaficha au tukajifanya hatutaki kuyataja, tumwambie waziwazi ndivyo ninavyoomba yaani nikulisema linalonitatiza,” anasema.

Sarah K aliyeanza huduma ya uimbaji mwaka 1991 ambapo alitumia lugha yake ya asili na kufanikiwa kutoa albamu tatu kwa lugha yake.

“Nina albamu kama tatu hivi za kilugha halafu mwaka wa 2000 ndio nilitoa albamu ya kwanza iliyokuwa inaitwa Wamtumainio Bwana na Mwimbieni Bwana nyimbo kama hizo. Halafu mwaka 2003 ndio nikatoa albamu ya Milele Daima na ndani yake ndio kuna wimbo ‘Nasema Asante’.

“Hivyo ukijumlisha zote za Kiswahili na Kiingereza ni Wamtumainio, Milele Daima, Adonai, Testimony na nyingine; na sasa nina Liseme na nimetoa albumu nyingine mpya ya sita ambayo ni mpya.

“Hiyo ina siku kadhaa sasa kwa hivyo za Kiswahili ni sita na za kilugha kama tatu hivi,” anasema.
Muimbaji huyo anasali katika kanisa la Anglikana ambapo mume wake ni mchungaji na anasema: “Ombi langu ni kwamba namwamini Mungu nitaendelea katika huduma yangu ya uimbaji hata kama nitakuwa na miaka 80 hata kama nitakuwa na miaka 90.

“Nitaendelea kumwimbia Mungu na kuwa mnyenyekevu na mtiifu mbele zake sio mbele za watu tu.
“Katika utunzi wangu ninamhusisha Mungu zaidi ya mimi mwenyewe ninavyojiona “Siwezi kusema ooh kwa sababu nina albumu tisa au 10; yaani nina ujuzi kabisa wa utunzi kwa hivyo simhitaji Roho Mtakatifu na simhitaji Mungu-siwezi kumsahau Mungu.
“Ninawajenga watu mioyo yao; nitakuwa nawainua watu mioyo yao ambao ni wadhaifu kwenye maeneo ambayo Roho Mtakatifu ananipa watasikia wameinuka na kuwa na matarajio kwamba Mungu yupo na ataendelea kuwatendea makuu-ni mengi tu wacha niachie hapo kwanza.”

Muimbaji huyo anawataka wasanii wachanga wasife moyo na wafuatilie ndoto zao na maono yao kwa sababu kuna mambo mengi ambayo yanaweza kupotosha uimbaji wao.

“Mambo mengi huja kwa mtindo kwamba umefika kumbe bado hujafika; nitakutolea mifano miwili: hili linaweza kuzungumziwa kwa urefu sana katika uimbaji, inaweza ikaja ukiwa mchanga halafu Mungu akakupa kibali sana mbele ya watu kwa wimbo wako kupendwa na ukauzwa sana.

“Sasa hapo kikwazo kimoja kinaweza kukufanya ukarudi nyuma; ni zile hela utakazozipata kutoka kwenye uimbaji ule zinaweza kukutikisa ukarudi nyuma ukakosa kufuatilia yale maono yako uliyokuwa nayo au ahadi ulizoweka mbele za Mungu.

“Unajua kuna ahadi zile uliweka wakati uko chini kabisa ukamwambia Mungu, ‘Utakaponivusha, utakaponibariki nitafanya mambo kadhaa’; kwa hivyo unajikuta umesahau.
La pili ni ile umaarufu wakati wimbo wako ume-‘hit’ ukajulikana sana kuna ule umaarufu unaoupata kila mtu anakuita Sarah K, Sarah K kila mtu anaongea juu yako redio zote zinakutaja; kwa hiyo hiyo umaarufu ukishaingia ndani yako na ukaukubali kwamba wewe ni maarufu ndipo kiburi kitaanza kujiinua.

“Ni vema kuendelea kuwa mnyenyekevu tu daima na umshukuru Mungu.


KWA TUKIO LOLOTE LA KIINJILI TANGAZA NA FPCT TEGETA BLOG ILI UWEZE KUFIKIA WATU WENGI ZAIDI

EMAIL YETU NI ...fpcttegeta@gmail.com
NAMBA ZA SIMU NI...0768061291 Na 0752040012 Au 0765187090

Hii ni kwa matukio yote ya kutangaza neno la Mungu kuanzia mikutano ya injili matamasha mbalimbali, uzinduzi wa albamu za choir mbalimbali na waimbaji binafsi  Lengo ni kuhakikisha injili inasambaa kote ulimwenguni