Tuesday, 21 July 2015

HATIMAE ASK, MKUU WA MAKANISA YA FPCT JIMBO LA PWANI ALAMBA SHAHADA YA KWANZA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa , ni msemo unaotumiwa na watu wengi hasa pale linaposubiliwa kwa hamu  jambo flani litokee. Ni ile safari ya miaka 3 ya masomo ya ASKOFU MKUU WA MAKANISA YA FPCT JIMBO LA PWANI ASK, REVERT KAMONONGO, ya kuisaka Shahada ya masomo ya Biblia, zaidi unaweza kuyaita masomo ya Theolojia. Safari hiyo imehitimika salama kabisa katika chuo cha SANJARANDA BIBLE COLLEGE- mkoani SINGIDA .Sherehe hizo zilifanyika jumamosi ya 17/07/2015 katika ukumbi wa chuo hicho na mgeni Rasmi katika mahafari hayo ya 13 alikua ni Bishop STIVEN. Licha ya viongozi na wachungaji ,mbalimbali wanaounda jimbo hilo kuhudhulia pia alikuwaepo mke wa Askofu Mama R . Kamonongo na Mtoto wao mkubwa Charles Revec.

                                 Picha kwa hisani ya Revec media.  Asantesana Revec media kwa ushilikiano wenu mzuri uliopo katiyenu na blog yetu.
Askofu mkuu wa makanisa ya fpct jimbo la Pwani na Zanzibar Ask Kamonongo akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasimi Bioshop STEVEN , kwenye mahafari ya 13 ya wahitimu wa shada ya theolojia katika chuo cha biblia cha  Sanjaranda Mkoani Singida( SANJARANDA BIBLE COLLEGE)

 Askofu Kamonongo akiwa na mke wake wakikata keki ya pongezi kwenye hafla iliyofanyika jioni baada ya sherehe kuu iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanjaranda Bible College.

                                                 Hii ni kwaya ya wahitimu ikiimba

                Ask Kamonongo akiwa na mch Ngenzi wa fpct Msasani (wa kwanza kushoto)
Kwaya ya wahitimu wakitumbuiza aliyeshika microphone ni Ask Kamonongo akiongoza wimbo kwa umahili mkubwa huku akikumbushia enzi hizoo za ujana wake wakati alipokua akiimba Kwaya. 

Akiwa na makamo ASKOFU wa Jimbo la Pwani
Akiwa na Mgeni Rasmi Askofu Stevie Mlenga
Akiwa na Mkuu wa Chuo Rev: John Tuu
Wachungaji misheni ya MsaNGA
Akipokea zawadi mbalimbali kwa watu Sanjaranda
Wakimshukuru Mungu na Mama mchungaji kwa sherehe ya Jioni
Akipokea zawadi ya Taaluma mshindi wa Tatu na zawadi ya Mwanafunzi bora aliyeonyesha Utii na Nidhamu

 ( Picha kwa hisani ya Revec media..   Asante sana Revec media kwa ushilikiano na mahusiano  mazuri yaliopo katiyenu na blog yetu. )

1 comment: