Wednesday, 8 July 2015

MAMBO YAMEPAMBA MOTO, FPCT BOKO YAZIDI KUCHANJA MBUGA SASA.

Hili ni kanisa la kipentekoste linaloitwa FPCT BOKO (FREEPENTECOSTELCHURCH OF TANZANIA- BOKO) linalochungwa na mtumishi wa Mungu Mchungaji na Mwinjilisti anaye tumiwa na Mungu kwa viwango vya juu isivyo kawaida Mch: ELIJAH MTISHIBI na kamati nzima ya uongozi wa kanisa hilo.
      Ni hatua ambayo inaendelea kumpa Mungu utukufu kwani kanisa hilo linazidi kusonga mbele zaidi ni takribani miezi sita(6) na wiki kadhaa tangu kanisa hilo lianzishwe,Lakin  huwezi kuamini na utabaki unamshangaa Mungu kwa kazi na matendo yake anayoyafanya ndani ya kanisa hilo.
   Kwakipindi hicho chote tangu kanisa lianzishwe watu wenye shida na mahitaji mbalimbali wameendelea kupokea majibu yao huku wagonjwa wenye magonjwa sugu wameendelea pia kufunguliwa siku hadi siku huku idadi wa waumini ikiongezeka kwa kasi.
   Hayo na mengine mengi ni vitu ambavyo vinaendelea kumpa Mungu utukufu kila uchwao.
       Karibu uungune na watumishi wa Mungu katika kanisa la FPCT BOKO kwa maombi na maombezi,matatizo mbalimbali ya kiroho na ya kimwili pia karibu uonane na watumishi wa Mungu watakusaidia.
 
    Jinsi ya kufika:-
        Kama watokea MWENGE,AFRICANA,MBUYUNI,TEGETA na kwingineko  panda magari yaendayo Bunju au Bagamoyo Pia kama watokea Bagamoyo,Bunju panda gari za Mwenge au Tegeta shuka kituo cha BOKO KWA MPEMBA,ikiwa umetoka mwenge usivuke lakini kama watokea Bagamoyo vuka utaona kibarabara ya vumbi,tembea mbele nusu km utakutana na kibao kinachoelekeza kanisa lilipo hapo utakua umefika.
Mchungaji Mtishibi kushoto akiwa na Mwimbaji Masanja Mkandamizaji. 

Mch Mtishibi Akiwa  madhabahuni akifundisha. 

Moja ya sehemu ya waumini wa Kanisa la FPCT BOKO wakiwa madhabahuni wakimsifu Mungu.

Picha ikionesha moja ya mkutano aliowahi kuhubili mtumishi wa Mungu Mch ELIJAH MTISHIBI. Katika mkutano huo watu wengi walifunguliwa, Sifa na utukufu  kwa Mungu. 

Mch   ELIJAH MTISHIBI

Mchungaji ELIJAH MTISHIBI akiwa katika picha ya furaha sana

Baadhi ya waumini pia wakiwa katika sifa.


Moja ya team ya vijana washilika wa kanisa la fpct Tegeta  Ni team inayofanya kazi kwa pamoja na ushirikiano wa karibu na kanisa la FPCT BOKO. 

No comments:

Post a Comment