Friday, 24 July 2015

ROHO WA MUNGU ATEMBEA KATIKA IBADA YA SIFA NA KUABUDU FPCT BOKO

Mkesha wa ibada ya kusifu na kuabudu uliofanyika katika kanisa la FPCT BOKO linaloongozwa na Mch ELIJAH MTISHIBI nje kidogo ya jiji la Dar es salaam Tanzania. Hakika ulikua ni mkesha wa baraka sana. fuatilia picha
Mchungaji Elijah Mtishibi (wa kwanza kushoto) na mkalimani wake Gabilo Hossea wakati akifundisha somo maalumu kwenye mkesha huo kueleza jinsi ambavyo Mungu anaweza kumuinua mtu  bila ya kujali vile mtu mwenyewe alivyo kwani Mungu anavyo mtazama mtu ni tofauti sana na anavyomuwazia. Usikate tamaa wala kujidhalau Mungu yupo kwaajili ya watakatifu.










Mchungaji Elijah akifanya maombezi


Mtume Moses akiendelea kufanya maombi


Mtume Moses akifanya maombi na maembezi kwa moja ya watu walikuwapo kwa mkesha huo



John Gabriel akiongoza  sifa

Mzee  wa kanisa la FPCT Boko Samweli Mtiana akimwinulia Mungu sifa katika sifa na kuabudu.

Mchungji Elijah Mtishibi akifundisha kwa mifano hapa alaikua akielezea jinsi ambavyo Mungu anaweza kumuinua mtu na kumweka mahala pa juu sana kuliko amabavyo inavyoweza kutegemewa. Licha watu kukuksema na kukuona vibaya wewe usikate tamaa ipo siku Mungu atakuinua.

Mwimbaji Gabilo Hossea  akimwimbia Mungu .

Mwinjilisti Hezron Mwanafunzi wa Yesu akiwa anaimba







Mkesha huu uliandaliwa na Uongozi wa idara ya vijana kanisa la Fpct Parishi ya Tegeta chini ya Mwenyekiti wake Frank Charles Gibebe na vijana kutoka sehemu mbalimbali kuhudhulia

No comments:

Post a Comment