Sunday, 2 November 2014

HUU NI WAKATI WA WAKRISTO KUMUOMBA MUNGU, MTANDAO WA NDOA ZA JINSIA MOJA WAZIDI KUSHIKA KASI

MTANDAO WA NDOA ZA JINSIA MOJA WAZIDI KUSHIKA KASI, MASHOGA NA WASAGAJI KUASILI WATOTO, UFARANSA NAYO YAFUATA NJIA Kadri siku zinavyoenda, dalili za kiama nazo zinazidi. Sentesi hii inatokana na mchakato wa serikali ya Ufaransa kuandaa muswada ambao unaweza kuwa sheria wiki hii - sheria itakayowafanya watu wa jinsia moja (wanaume kwa wanaume, na wanawake kwa wanawake) wapate haki ya kuoana na kuasili watoto. Sheria hii ikianza, Ufaransa itakuwa taifa la 12 kuruhusu ndoa za jinsia moja, ikiwa imetanguliwa na nchi za Scandinavia; Denmark iliyoruhusu mwaka 2012, Norway (2008), Sweden (2009) na Iceland (2010), pia kuna Uholanzi (2001), Ubeljiji (2003), Spain, na Canada zilizoruhusu mwaka 2005, pamoja na Ureno (2010), huku nchi pekee ya kiafrika iliyoruhusu ndoa hizi ikiwa ni Afrika Kusini mnamo mwaka 2006. (Tanzania nayo ina wafadhili kadha wa kadha kutoka mataifa haya, aidha Serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali) Sheria kwa upande wa Marekani, inazuia serikali kuu kutambua ndoa za jinsia moja, lakini baadhi ya mataifa yake kama Connecticut, Iowa, Massachusetts, New Hampshire, New York na Vermon, pamoja na wilaya ya Columbia na maeneo mawili ya wamarekani wa asili, huku Mexico City ikitambua ndoa hizo, lakini kwa baadhi ya maeneo yake tu. Kwa mantiki hiyo, watu wa jinsia moja wanaweza kuonana, na kuasili mtoto katika nchio yoyote inyotambua sheria hizi, ikiwemo Brazil na Uingereza. Ufaransa ndiyo itakuwa nchi kubwa kiuchumi na kwa idadi ya watu kupitisha sheria hii, ambayo imo katika sera ya Rais Francois Hollande, ambapo tayari kuna watu wameonesha kufurahishwa na jambo hili linaoitwa sheria ya "ndoa kwa wote", ingawa baadhi ya watu wameonesha upoinzani katika taifa hili la kikatoliki kitamaduni Je, mataifa madogo yanayotegemea nchi zilioendelea ili kukuza uchumi wao zitaweza kuhimili mikiki ya matakwa ya wafadhili? Maombi yatatuepusha na mengi, na kutuokoa na mbinu za adui mwovu shetani.

SOMO LA LEO : JUMAPILI IBADA YA ASUBUHI TAR 02/10/2014; KUMTAKA MUNGU NA NGUVU ZAKE

Nini maana ya Nguvu? Ni uweza wa kutawala/kumtawala adui. Nguvu ni matokeo ya mapigano juu ya watu Au vitu.Zipo nguvu za aina mbalimbali nguvu za mwili na nguvu za Roho katika maisha ya Kiroho tunahitaji nguvu ya Mungu ili kuweza kushinda Majaribu ya shetani. Watu wengi wapo kanisani lakini hawana uwezo wa kushinda misukosuko na majaribu ya shetani. FAIDAKUU YA KUWA NA NGUVU ZA MUNGU Nikuwa na uwezo mkuu wa kushinda majaribu dhidi ya mwovu ibirisi. Mitume na manabii walikua na nguvu za Mungu ndyo maana waliweza kushinda majaribu ZABURI 105:4-5. Mkristo yeyote anapokua ameokaoka na kutubu akazipokea nguvu za MUNGU anakuwa imara na hawezi kuteteleka. Mkristo huyohuyo anapotenda dhambi basi nguvu za Mungu hutoweka. Yapomambo mbalimbali yanayp mfanya mkristo kupoteza nguvu za Mungu mabo kama;- 1/Kutokusamehe Mathayo18:21-35 2/Mahusiano mabaya kati ya mume na mke au mahusiano mabaya ya kifamilia 1Petro1:3, 3:7 3/Mahusiano mabaya kati ya mtu na mtu,mtu na jirani yake na mawazo mabaya ndani ya moyo wa mtu yanaweza kusababisha mtu kurudi nyuma kiroho na hatimae kufia dhambini. Ili kuweza kuzipata na kuishi katika nguvu za Mungu ni ;- 1/Kusoma NENO LA MUNGU na kuliishia kama linavyo elekeza YOSHUA 1;8 2/Kuliweka NENO moyoni mwako ZABURI 119;11.,105 Mpendwa wangu neema ya MUNGU ni ya peke sana na ndyo maana tumepewa nguvu yaziada ya kushida majaribu na vikwazo vyote vya Shetani,katika Dunia hii zipo nguvu nyingi sana,waganga,wachawi,wasomi,na watu mashuhuli wote wana nguvu lakini bado nguvu zao haziwezi kumsaidia mtu mwingine,wala haziwezi kukupa tumainila kuishi baada ya kufa. Nguvu za MUNGU wetu aliye mtuma YESU KRISTO aje duniani kwa ajili yetu,akayafanya yaliyo makuu na baadae akatuachia ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye ngao na msaada kwetu Huyu ndiye NGUVU yetu ya kweli ambaye hutupa kushinda mambo yote yanayo tusonga. Kama hujampokea YESU KRISTO kuwa BWANA na mwokozi wa Maisha yako ni wakati wako sasa wa kumpa maisha yako ili uzipate NGUVU ZA MUNGU WETU aliye hai. Mali na pesa zako havitakusaidiaa.. Muda ni sasa wa kumpokea YESU ili awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yako ayabadilishe na uwe kiumbe kipya. Chukua hatua sasa ili uwe miongoni mwa watu wenye NGUVU ZA MUNGU ndani ya Miyo yao.. MUNGU akubariki na aendelee kusema na wewe katika maisha yako yote ya kila siku. Barikwa saana.. BY MWINJLIST JACOB LUKAS-FPCT TEGETA DSM TANZANIA..

Wednesday, 29 October 2014

ZAMBIA YAPATA PIGO, RAIS WA NCHI HIYO BWANA MICHAEL SATA AFARIKI DUNIA.

HAYATI; MICHAEL  SATA
Familia ya Bwana SATA na Taifa la ZAMBIA vimekumbwa na kanzia nzito ya kumpoteza Raisi wao kipenzi. Umauti huo umemfika leo wakati akiwa katika hosptal ya Londoni huko nchini Wingereza amabokoalikua akiendelea kupatiwa matibabu(ugonjwa bado haujatangazwa)                                  Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 alizaliwa mwaka 1937 katika mji wa MPIKA.        Hayati SATA aliingia madarakani septemba 2011baada ya kumshinda aliye kuwa raisi wa nchihiyo Bwana LUPIA BANDA.                                                                                                                       Akiwa madarakani alionekana kuwa ni mtu mwenye kujituma na kuchapa kazi zaidi huku akionesha nia yake ya dhati juu ya kupambana na masuala ya rushwa na kuleta usawa kwenye mambo ya ustawi wa kijamii. Akiwa katika harakati za kisiasa na kijamii alikua ni mtumiaji/mvutaji wa sigara halihiyo ilimfanya awe na sauti ya kukwaluza, Katika uongozi wake hakuwahi kuwa na rafki wa kudumu. Ufanisi wake wa kazi ulimfanya kuwa maarufu na hatimae akawa Gavana wa jimbo la LUSAKA kabla ya kuwa rais.                                                                                                                Hayati SATA amefariki dunia akiwa chini ya uangalizi makini wa madaktari ambao walikua wakijituma kwa juhudi zao ilikuunusuru uhai wa Bwana SATA hata hivyo haikuwezekana..                            Bwana SATA ni raisi wa pili wa Zambia kufariki akiwa madarakani.                                      
HAYATI;  MICHAEL SATA   enzi za uhai wake.

Sunday, 26 October 2014

IBADA YA PILI KANISA LA FPCT TEGETA INAENDELEA

Asante BWANA YESU kwa kutupatia mtoto wa kiume YEFTA.. Hayo ni meno ya BW&BI ALEX. F. MASABHO wakisimama katika madhabahu wakimshukuru Mungu kwa baraka hiyoo. Kanisa la FPCT TEGETA MACHINJIONI


Friday, 24 October 2014

TALII NA BWANA, FPCT TANDALE TANESCO DSM PALIKUA MOTOO,,,,,

                                                                                                                                                                   Nina mshukuru sana Mungu kwakua ameendelea kuwa na mimi,pamoja na kanisa kwa ujumla kwani MUNGU amekuwa ndiye kiongozi mkuu katika uanzishaji wa huduma yake. Tulianza kwa wakati mgumu sana lakini BWANA hakuweza kutuacha na sasa tunaendelea kukua na kuongezeka siku hadi siku, Alisema Mch Misigaro                                                                                                                                                                                                                                                                                                                  

Wednesday, 15 October 2014

MKESHA MKUBWA WA VIJANA KUOMBEA TAIFA LA TANZANIA

MKESHA MKUBWA WA VIJANA PRISHI YA TEGETA KANISA LA FPCT

  idara ya vijana kanisa la fpct parishi ya tegeta wameeandaa mkesha mkubwa wa vijana ambao utawakutanisha vijana wote wa jiji la Dar es salaam kumuabudu Mungu na kulitukuza jina la jehova shama katika mkesha huo
                                       baadhi ya vijana wa kanisa la fpct tegeta

                                kwaya ya jerusalemu kutoka tageta watatoa huduma siku hiyo

 Akizungumza na fpct tegeta blog mwenyekiti wa idara ya vijana kanisa la fpct parishi ya tegeta bwana Frank Gibebe amesema mkesha huo utafanyika katika kanisa la fpct madale jijini Dar es salaam siku ya ijumaa tarehe 31/10/2014 kuanzia saa mbili za usiku mpaka saa kumi na mbili alfajili ambapo amesema lengo la kufanya mkesha huo ni kutaka kuwakutanisha vijana kutoka makanisa tofauti na kujumuika pamoja kuliadhimisha jina la bwana yesu

  Gibebe amesema katika mkesha huo watakuwa na maombi ya kuliombea taifa la Tanzania na mchakato mzima wa katiba mpya pamoja na kuwaombea viongozi wa taifa huku akidai kuwa watafanya maombi maalum kuwaombea viongozi wapya wa kanisa la fpct kitaifa pamoja na kuombea mahitaji mbali mbali ya vijana katika nyanja mbalimbali.

 Aidha kiongozi huyo amesema idara hiyo imearika kwaya mbali mbali pamoja na waimbaji binafsi ambao watatoa huduma katika mkesha huo na kuongeza kuwa vijana wameandaa michezo mbalimbali kama maigizo ,vichekesho na ngonjera kwa lengo la kuhakikisha mkesha huo unakuwa wa tofauti na wa aina yake.
                          Frank Gibebe  mwenyekit idara ya vijana kanisa la fpct parish ya tegeta

   Hata hivyo amewaomba vijana kutoka maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam kuhudhuria katika mkesha huo huku akisema itakuwa siku ya kipekee na ya tofauti kwa sababu tunataka kutumia nguvu Mungu alizotupa sisi kama vijana kupambana na ibilisi na kuvunja ngome zote za shetani katika nchi yetu ya Tanzania hivyo naomba vijana wajitokeze kwa wingi na Mungu wa mbinguni atawabariki

Saturday, 11 October 2014

SIKILIZA MAF5 RADIO KUPITIA www.maf5radio.com KILA SIKU KWA VIPINDI MOTO MOTO

KWA HABARI ,MATUKIO KATIKA ANGA LA KITAIFA KIMATAIFA , HABARI ZA KIBIASHARA MICHEZO NA BURUDANI SIKILIZA KIPINDI CHA SAFARI KUU KILA SIKU SAA 11:00 JIONI- 1:00 USIKU KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA www.maf5radio.com