Friday, 8 May 2015

MAANDALIZI JUMAPILI YA MGUSO SEASON 2 YAKO HATUA ZA MWISHO

 Kamati ya maandalizi,tamasha na sherehe katika kanisa la fpct tegeta jijini Dar es salaam imesema tayari maandalizi ya ibada ya sifa na kuabudu ijulikanayo kama Jumapili ya baraka na Mguso wa kipekee Season 2 yamekamilika kwa asilimia 80 huku na asilimia 20 zilizobakia ni maandalizi madogodogo.

  Akizungumza na Blog hii Katibu wa Kamati Exauds Wiston Alisema tayari wamefanikiwa kwenye hatua kubwa upande wa maandalizi hasa upande wa waimbaji ambapo tayari mwimbaji kutoka USA Fidel Murwa tayari ameshawasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma siku hiyo,na mwimbaji mwingine kutoka kenya Denis Lisoni atawasili nchini siku ya kesho majira ya Saa nane mchana.

 Exauds Alisema waimbaji wengine kutoka Tanzania kama Gabilo Hosea na Kepha Jackson tayari wako kwenye maandalizi kuelekea siku hiyo,huku Nuru kwaya,jerusalem kwaya,The hope singers,na The best of Jesus choir ni miongoni mwa kwaya zitakazohudumu katika siku hiyo.

 Aidha kiongozi huyo alisema kikundi cha sifa na kuabudu kutoka kanisa la fpct tegeta kiko tayari kwa huduma siku hiyo huku akiwaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kwenye ibada hiyo ya sifa na kuabudu kwani Mungu wa majeshi atakutana na uhitaji wa kila mmoja

No comments:

Post a Comment