Friday, 24 July 2015

ROHO WA MUNGU ATEMBEA KATIKA IBADA YA SIFA NA KUABUDU FPCT BOKO

Mkesha wa ibada ya kusifu na kuabudu uliofanyika katika kanisa la FPCT BOKO linaloongozwa na Mch ELIJAH MTISHIBI nje kidogo ya jiji la Dar es salaam Tanzania. Hakika ulikua ni mkesha wa baraka sana. fuatilia picha
Mchungaji Elijah Mtishibi (wa kwanza kushoto) na mkalimani wake Gabilo Hossea wakati akifundisha somo maalumu kwenye mkesha huo kueleza jinsi ambavyo Mungu anaweza kumuinua mtu  bila ya kujali vile mtu mwenyewe alivyo kwani Mungu anavyo mtazama mtu ni tofauti sana na anavyomuwazia. Usikate tamaa wala kujidhalau Mungu yupo kwaajili ya watakatifu.










Mchungaji Elijah akifanya maombezi


Mtume Moses akiendelea kufanya maombi


Mtume Moses akifanya maombi na maembezi kwa moja ya watu walikuwapo kwa mkesha huo



John Gabriel akiongoza  sifa

Mzee  wa kanisa la FPCT Boko Samweli Mtiana akimwinulia Mungu sifa katika sifa na kuabudu.

Mchungji Elijah Mtishibi akifundisha kwa mifano hapa alaikua akielezea jinsi ambavyo Mungu anaweza kumuinua mtu na kumweka mahala pa juu sana kuliko amabavyo inavyoweza kutegemewa. Licha watu kukuksema na kukuona vibaya wewe usikate tamaa ipo siku Mungu atakuinua.

Mwimbaji Gabilo Hossea  akimwimbia Mungu .

Mwinjilisti Hezron Mwanafunzi wa Yesu akiwa anaimba







Mkesha huu uliandaliwa na Uongozi wa idara ya vijana kanisa la Fpct Parishi ya Tegeta chini ya Mwenyekiti wake Frank Charles Gibebe na vijana kutoka sehemu mbalimbali kuhudhulia

Tuesday, 21 July 2015

POLISI BONGO YAWEKA WAZI MAJINA NA PICHA YA MAJAMBAZI YALIYOVAMIA KITUO CHA POLISI CHA SITAKI SHARI.

Ni msako mkali unao endelea hapa nchini Tanzania wa kuwasaka majambazi walio vamia kituo cha polisi cha Sitaki shari Ukonga Jijini Dar es salaam na kuwauwa askari polisi 4 na askali mmoja wa ulinzi shilikishi. Sasa zoezi hilo limeendelea kwa kasi pia na kuwashirikisha wananchi, Jeshi la polisi limefanikiwa kuwa tia ngvuni majambazi wa 2 na wengine 3 kuwaua kwenye mapigano makali yaliyozuka wakati wa msako huo na kuweza kukamata kiasi cha zaidi ya 160milioni na silaha saba zilizoporwa kituoni hapo,.
     Baada ya kuzungumza na wanadishi wa habari Kamanda Kova aliyaweka wazi majina ya majambazi wengine sugu wanaosakwa na jeshi hilo la polisi.

  Fuatilia na usome  majina na pichazaohapaa.







HATIMAE ASK, MKUU WA MAKANISA YA FPCT JIMBO LA PWANI ALAMBA SHAHADA YA KWANZA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa , ni msemo unaotumiwa na watu wengi hasa pale linaposubiliwa kwa hamu  jambo flani litokee. Ni ile safari ya miaka 3 ya masomo ya ASKOFU MKUU WA MAKANISA YA FPCT JIMBO LA PWANI ASK, REVERT KAMONONGO, ya kuisaka Shahada ya masomo ya Biblia, zaidi unaweza kuyaita masomo ya Theolojia. Safari hiyo imehitimika salama kabisa katika chuo cha SANJARANDA BIBLE COLLEGE- mkoani SINGIDA .Sherehe hizo zilifanyika jumamosi ya 17/07/2015 katika ukumbi wa chuo hicho na mgeni Rasmi katika mahafari hayo ya 13 alikua ni Bishop STIVEN. Licha ya viongozi na wachungaji ,mbalimbali wanaounda jimbo hilo kuhudhulia pia alikuwaepo mke wa Askofu Mama R . Kamonongo na Mtoto wao mkubwa Charles Revec.

                                 Picha kwa hisani ya Revec media.  Asantesana Revec media kwa ushilikiano wenu mzuri uliopo katiyenu na blog yetu.
Askofu mkuu wa makanisa ya fpct jimbo la Pwani na Zanzibar Ask Kamonongo akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasimi Bioshop STEVEN , kwenye mahafari ya 13 ya wahitimu wa shada ya theolojia katika chuo cha biblia cha  Sanjaranda Mkoani Singida( SANJARANDA BIBLE COLLEGE)

 Askofu Kamonongo akiwa na mke wake wakikata keki ya pongezi kwenye hafla iliyofanyika jioni baada ya sherehe kuu iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanjaranda Bible College.

                                                 Hii ni kwaya ya wahitimu ikiimba

                Ask Kamonongo akiwa na mch Ngenzi wa fpct Msasani (wa kwanza kushoto)
Kwaya ya wahitimu wakitumbuiza aliyeshika microphone ni Ask Kamonongo akiongoza wimbo kwa umahili mkubwa huku akikumbushia enzi hizoo za ujana wake wakati alipokua akiimba Kwaya. 

Akiwa na makamo ASKOFU wa Jimbo la Pwani
Akiwa na Mgeni Rasmi Askofu Stevie Mlenga
Akiwa na Mkuu wa Chuo Rev: John Tuu
Wachungaji misheni ya MsaNGA
Akipokea zawadi mbalimbali kwa watu Sanjaranda
Wakimshukuru Mungu na Mama mchungaji kwa sherehe ya Jioni
Akipokea zawadi ya Taaluma mshindi wa Tatu na zawadi ya Mwanafunzi bora aliyeonyesha Utii na Nidhamu

 ( Picha kwa hisani ya Revec media..   Asante sana Revec media kwa ushilikiano na mahusiano  mazuri yaliopo katiyenu na blog yetu. )

Monday, 20 July 2015

HONGERA BABA ASKOFU REVERT KAMONONGO KWA KUHITIMU.

          Kushoto ni Askofu Kamonongo akipongezwa na kijana wake Charles Revert

Monday, 13 July 2015

MAJAMBAZI YATIWA NGUUVUNI MCHANA HUU DAR,

Ni kundi la majambazi linalo kadiliwa kuwa na idadi ya watu nne(4) lililokuwa likipora kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa mtu ambaye hajaweza kutambulika jina kwa Haraka,Ilikua  katika mitaa ya mnara wa saa maeneo ya Stesheni jiji Dara es salaam.  Baada ya polisi (askali kanzu)kuwatilia mashaka watu hao iliwalazimu kuwafuata mjambazi hayo na kuanza kurushiana risasi na wengine kujificha chini ya tex zilizokuwa zimepaki katika eneo hilo. Baada ya mapigano hayo polisi walifanikiwa kuwatia nguvuni wote. 



Wednesday, 8 July 2015

MAMBO YAMEPAMBA MOTO, FPCT BOKO YAZIDI KUCHANJA MBUGA SASA.

Hili ni kanisa la kipentekoste linaloitwa FPCT BOKO (FREEPENTECOSTELCHURCH OF TANZANIA- BOKO) linalochungwa na mtumishi wa Mungu Mchungaji na Mwinjilisti anaye tumiwa na Mungu kwa viwango vya juu isivyo kawaida Mch: ELIJAH MTISHIBI na kamati nzima ya uongozi wa kanisa hilo.
      Ni hatua ambayo inaendelea kumpa Mungu utukufu kwani kanisa hilo linazidi kusonga mbele zaidi ni takribani miezi sita(6) na wiki kadhaa tangu kanisa hilo lianzishwe,Lakin  huwezi kuamini na utabaki unamshangaa Mungu kwa kazi na matendo yake anayoyafanya ndani ya kanisa hilo.
   Kwakipindi hicho chote tangu kanisa lianzishwe watu wenye shida na mahitaji mbalimbali wameendelea kupokea majibu yao huku wagonjwa wenye magonjwa sugu wameendelea pia kufunguliwa siku hadi siku huku idadi wa waumini ikiongezeka kwa kasi.
   Hayo na mengine mengi ni vitu ambavyo vinaendelea kumpa Mungu utukufu kila uchwao.
       Karibu uungune na watumishi wa Mungu katika kanisa la FPCT BOKO kwa maombi na maombezi,matatizo mbalimbali ya kiroho na ya kimwili pia karibu uonane na watumishi wa Mungu watakusaidia.
 
    Jinsi ya kufika:-
        Kama watokea MWENGE,AFRICANA,MBUYUNI,TEGETA na kwingineko  panda magari yaendayo Bunju au Bagamoyo Pia kama watokea Bagamoyo,Bunju panda gari za Mwenge au Tegeta shuka kituo cha BOKO KWA MPEMBA,ikiwa umetoka mwenge usivuke lakini kama watokea Bagamoyo vuka utaona kibarabara ya vumbi,tembea mbele nusu km utakutana na kibao kinachoelekeza kanisa lilipo hapo utakua umefika.
Mchungaji Mtishibi kushoto akiwa na Mwimbaji Masanja Mkandamizaji. 

Mch Mtishibi Akiwa  madhabahuni akifundisha. 

Moja ya sehemu ya waumini wa Kanisa la FPCT BOKO wakiwa madhabahuni wakimsifu Mungu.

Picha ikionesha moja ya mkutano aliowahi kuhubili mtumishi wa Mungu Mch ELIJAH MTISHIBI. Katika mkutano huo watu wengi walifunguliwa, Sifa na utukufu  kwa Mungu. 

Mch   ELIJAH MTISHIBI

Mchungaji ELIJAH MTISHIBI akiwa katika picha ya furaha sana

Baadhi ya waumini pia wakiwa katika sifa.


Moja ya team ya vijana washilika wa kanisa la fpct Tegeta  Ni team inayofanya kazi kwa pamoja na ushirikiano wa karibu na kanisa la FPCT BOKO.