Kauli hiyo imetolewa na Askofu mkuu wa Jimbo la Kigoma Ask Jeremiah Kumenya, alipokuwa katika kanisa la FPCT TEGETA-Machnjioni baada ya Ibada wakati akizungumza na mwandishi wetu pale alipotaka kuskia kauli ya kanisa na kauli ya Askofu akiwa ni kiongozi wa ngazi ya juu katika jimbo hilo Kuhusu sakata la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)nchini Tanzania
Askofu Kumenya alisema , lengo na kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu ni aishi milele na kumuabudu yeye.
Inapotokea mwanadamu amekufa basi awe Kafa kwa kifo cha kawaida ambacho ni mpango wa Mungu kama yeye anavyo penda
Lakini inasikitisha sana siku hizi wapo watu wanapanga njama kabisa za kuwaua Binadamu wenzao ambao wameumbwa na Mungu kama wao.
Akiendelea mbele zaidi Askofu aliongeza kuwa Ikitokea mtu anamuua mwenzake tena kwa ukatili na unyama usio semeka ifahamike moja kwa moja mtu huyo anamkosea Mungu na zaidi hamjui yeye aliye muumba na ambaye pia anayekataza mabaya Hasa kuua" alisema Askofu Kumenya.
Kuhusu watu wanao amini nguvu za giza/waganga ask Kumenya alisema ni Imani potofu kabisa ambazo hazina msaada kwa mtu yeyote aliyeumbwa na Mungu, Kwani haina sababu ya kuamini kwamba kumuua mwenzako na kupata utajili si sahihi. Tamaa ya utajili na uroho wa madaraka visiwe sababu ya kuwakatishia uhai binadamu wenzetu walioumbwa na Mungu kama sisi."
Waganga wote wa kienyeji wanao hamasisha watu kufanya vitendo hivi waache mara moja kwani muda wao wa kufichuliwa na kupewa adhabu akali unakaribia.
Kwa upande wa kanisa na wakristo wote nchini Askofu kumenya alisisitiza sana kuwa waendelee kushikamana kumwomba Mungu kwa kasi na juhudi zaidi, kwani Mungu anasikia kilio cha watu wake, maana Mungu anasema ikiwa watu wake watalia kwa bidii na kumpazia sauti atasikia. Taifa linapopita katika kipindi kigumu kama hiki ambapo watu wanakosa msaada na majibu ya matukio yao jukumu la kanisa ni kumuita Mungu mwenye majibu.
Kanisa halipaswi kumnung'unikia wala kumlaumu mtu yeyote ila tunapaswa kumlilia Mungu atusaidie kutuokoa na roho chafu ya Mauti inayolinyemelea Taifa letu" alisema ask Kumenya.
ASKOFU ; JEREMIAH KUMENYA wa jimbo la Kigoma akiwa madhabahuni katika kanisa la FPCT TEGETA-Machinjion i ,wakati alipokuwa akihibiri, jana.( Picha na mwanahabari wetu Hossien Gabriel) |
Mwisho kabisa Askofu Kumenya alitoa wito kwa wananchi na wasamalia wema wenye mapenzi ya dhati na wanaoumizwa na kukerwa na vitendo hivi kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Mauaji ya walemavu wa Ngozi(Albino) Huku akiisisitiza Serikali na viongozi wote kuhakikisha wana simamia haki na ulinzi kwa kila Raia kwani ni haki yao kulindwa na kupata usalama wakati wowote.
No comments:
Post a Comment