Neno la Mungu linasema ajitengea na wenzake hutaka matakwa yake mwenywe. Lakini kwa upande huohuo ni heri kuwa na uoja kuliko kujitenga. Hayo ni maneno yaliyo semwa na mwenyeki wa idara ya akina mama wa Kanisa la FPCT TEGETA MACHINJIONI Mrs Revina Majoro, jumapili ya jana wakati walipokua na hafra fupi ya kutianamoyo na kupongezana baada ya kuombeana kwa muda wa zaidi ya wiki tatu ndani ya idara hiyo.
Nduguzangu waumini na akina mama kwa ujumla ni kwa muda wa takribani wiki tatu tumekua na zoezi la kuombeana kila mwana idara akimuombea mwenzake, tuliandika majina ya wana idara nakisha tukayaweka kwenye kikapu kila mtu akawa anakuja kuchagua karatsi lenye jina,kila aliye chukua jina hilo basi alienda kuliombea/kumwomea mwenzake ili Mungu aweze kumjibumahitajiyake, kama Ndoa,afya,masomo,familia nk,tumemwona Mungu akijbu sana maombi yetu hata kabla ya kuhitimisha wiki hizi za maombi,na sasa leo ndiyo hitimisho la maombi yetu na Sasa kila mmojawetu ameandaa zawadi ya kumpongeza mwenzake. Alisema Mrs Majoro akifafanua zaidi.
Angalia na Tazama Picha namna jinsi Hafra fupi ilivyo kua siku ya janaa.
No comments:
Post a Comment