Tuesday, 2 September 2014
Monday, 1 September 2014
MACHOZI YA FURAHA...... MIAKA KUMI NA NNE NDANI YA NDOA BILA MTOTO LAKINI MUNGU KASIKIA KILIO CHANGU SASA NIMEPATA MTOTO
ACHA NIMSHUKURU MUNGU SIO MCHEZO KUKAAA MIAKA KUMI NA NNE
NDANI YA NDOA BILA KUPATA MTOTO Jumapili
ya tarehe ya 31.8.2014 ilikuwa siku ya furaha na shangwe katika kanisa la fpct
tegeta kwa Mama huyu ambae alikaa miaka
kumi na nne katika ndo yake yeye na mume wake bila kupata mtoto lakini baada ya
kusubiri kwa kipindi hicho chote ndipo
Mungu aliposikia kilio chao na kujibu uhitaji wao wa muda mrefu na sasa
wamepata mtoto
kutoka kulia mama Ana na Mme wake wakimshukuru mungu Ilikuwa ni siku ya machozi kwa
mama huyu pamoja na mme wake hasa pale
Walipokuwa wanamshukuru Mungu katika kanisa la fpct Tegeta baada ya kupitia
kipindi cha mapito, majaribu,na vishawishi vya kila namna katika kipindi chote
cha miaka minne ambacho walikuwa wakimlilia Mungu ili aweze kukutana na uhitaji
wao. Familia
hii wakati inamshukuru Mungu kiukweli karibu kanisa zima hakuna ambaye hakutoa
machozi hasa baada ya kuusikiliza ushuhuda mama huyo wakati wakielezea namna
ambavyo walimuomba Mungu ikafikia hatua ambayo walionekana kuchoka kusubiri na ndipo
Mwanamke aliamua kuchukua jukumu la kwenda kwa mganga wa kienyeji na Mungu kumuweka pembeni, Anasema alipofika kwa
Mganga, mganga alimwambia tatizo lake limepata ufumbuzi ila alitakiwa kutoa
shilingi laki sita na kuku mmoja baada ya hapo alitakiwa kwenda makabulini yeye
pamoja na mganga ili aweze kuambiwa masharti ya kufanya. Aliendelea
kushuhudia kuwa baada ya kufika makabulini mganga alimwambia kuna shimo kubwa
ambalo alitakiwa kuingia ndani ya shimo hilo Mwanamke huyo alionekana kuwa na uoga
hasa alipotakiwa kuingia Ndani shimo lakini kingine kilichomuogopesha ni
makabuli yaliyokowa yamezunguka katika mazingira hayo halafu ilikuwa ni usiku
usiku wa manane. Anasema kwa kuwa alikuwa ana hamu ya kupata mtoto aliamua kuingia ndani ya shimo hilo na ndipo mganga alimwambia kuna joka kubwa litakuja kwenye shimo ili liweze fanya mapenzi na mama huyo baada ya kusikia hivyo alipiga kelele na kuanza kuyakataa masharti hayo lakini mganga alimwambia kwa vyovyote vile ni lazima afuate masharti hayo na tofauti na hapo hatopata mtoto milele. Hakika kilikuwa kipindi kigumu sana aliendelea kushuhudia na kusema baada yakuyagomea masharti ya mganga, mganga alipotea kusikojulikana huku yeye akiwa ndani ya shimo na kuanza kupiga kelele ili Mungu amsaidie na ndipo alipofanikiwa kutoka ndani ya shimo huku laki sita zake pamoja na kuku mganga akiwa ametokomea navyo, anasema ilipofika asubuhi alianza kujilaumu na kumuomba Mungu msamaha kwa yote aliyoyafanya. Baada ya kuona Mambo yamekuwa magumu ndipo familia hii iliweza kuhudhuria katika ibada moja kanisa la fpct tegeta na wakakutana na mtumishi wa Mungu Mch. Joram Jeremiah na ndipo mtumishi wa Mungu alipochukua hatua ya kuiombea familia hii huku akiwaomba kulitumaini jina la Mungu kwani mwaka kesho lazima watapata mtoto[yani mwaka huu 2014] kumbuka haya yote yalikuwa yanatokea mwaka jana mwaka 2013.
mch.Joram Jeremiah Ntaseha[fpct tegeta] Hata hivyo baada ya maombi ya mtumishi wa Mungu , na familia hii kusubiri kwa miaka kumi nan nne ndipo mwezi wa nane mwaka huu Mungu aliweza kujibu uhitaji wao na kufanikiwa kupata mtoto wa kike jina lake akiitwa ANA kiukweli kumbe Mungu anajibu kila hitaji kwa wakati wake ungana na familia hii kumshukuru Mungu.
Sunday, 31 August 2014
SOMO LA LEO KATIKA IBADA YA PILI KANISA LA FPCT TEGETA ...MUNGU ANAJIVUNIA MWENYE HAKI
JUMAPILI Tar 31/08/2014 IBADA YA PILI SOMO LA LEO MUNGU ANA JIVUNIA MWENYE HAKI{KUISHI MAISHA YENYE HAKI}.
Mwl.Evaline G.Manase
. AYUBU 1;1-6 Palikua na mtu mmoja ktk Nchi ya USI jina lake aliitwa AYUBU alikua ni mtu aliye mcha MUNGU sana na kuwa ni mtu mkamilifu mmbele za Mungu.,Anapo tokea mtu mwenye haki duniani Mungu hujivunia saana,lakin upande wa pili shetani nae huchukia saana na kuendelea kufuatilia maisha ya mwenye haki huyo AYUBU 3;3-10 ,Shetani huwashitaki wenye haki mbele za MUNGU Shetani huwatumia watu/vitu vya karibu saana kukujaribu,mke,watoto,mali,majiran wanaweza kuwa jaribu.. ,Kwa nn huwashitki? huwashitaki ili kumdhihaki Mungu. shetanii ana uwezo sawa na malaika kwa hiyo huiona mioyo ya wanadamu na kutamani Mtu mwenye haki aangamie.. Mungu humruhusu shetani amjaribu mwenye haki wake. kwa nn MUNGU hukubari ajaribiwe ? ,1/Mungu ajivunie 2/shetani aabike 3/ushuhuda uwepo. 4/watu waokolewe 5/ tuendelee kumtumaini.. ,Mungu alimtumia Ayubu kumsimangia shetan kwa kua alikwisha kumwona ni mwenye haki. M aisha ya watakatifu yana chunguzwa na kuwindwa saana ili aweze kurudi nyuma. simama katika UKamilifu hatakama kuna mapto,taabu.mateso,na dhiki mbali mbali unazo pitia wew simama tu ktka hali ya utakatifu utashinda. Simama tu endelea kudai haki yako mbele za Mungu kam Ayubu alivyo simama. Hakutenda dhambi hatakma alipt katka Magumu.. usi lalamike mbele za Mungu si mama na BWANA naye ata kushindia Mwachie YESU kila kitu chako yeye ni mshindi ugumu wowote yeye ni msindi..Mungu ni mwema saana hawezi kumuacha mwenye haki wake afe. Jikaze,jivute simama IMARA atakushindia na wew utarudishiwa mara saba...Mungu akutie nguvu na akuinue ktka maisha yako yoote na uwe mshindi..MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI AAMEEEEE'''''' BY MW EVELIN G. MANASE FPCT -TEGETA
Mwl.Evaline G.Manase
. AYUBU 1;1-6 Palikua na mtu mmoja ktk Nchi ya USI jina lake aliitwa AYUBU alikua ni mtu aliye mcha MUNGU sana na kuwa ni mtu mkamilifu mmbele za Mungu.,Anapo tokea mtu mwenye haki duniani Mungu hujivunia saana,lakin upande wa pili shetani nae huchukia saana na kuendelea kufuatilia maisha ya mwenye haki huyo AYUBU 3;3-10 ,Shetani huwashitaki wenye haki mbele za MUNGU Shetani huwatumia watu/vitu vya karibu saana kukujaribu,mke,watoto,mali,majiran wanaweza kuwa jaribu.. ,Kwa nn huwashitki? huwashitaki ili kumdhihaki Mungu. shetanii ana uwezo sawa na malaika kwa hiyo huiona mioyo ya wanadamu na kutamani Mtu mwenye haki aangamie.. Mungu humruhusu shetani amjaribu mwenye haki wake. kwa nn MUNGU hukubari ajaribiwe ? ,1/Mungu ajivunie 2/shetani aabike 3/ushuhuda uwepo. 4/watu waokolewe 5/ tuendelee kumtumaini.. ,Mungu alimtumia Ayubu kumsimangia shetan kwa kua alikwisha kumwona ni mwenye haki. M aisha ya watakatifu yana chunguzwa na kuwindwa saana ili aweze kurudi nyuma. simama katika UKamilifu hatakama kuna mapto,taabu.mateso,na dhiki mbali mbali unazo pitia wew simama tu ktka hali ya utakatifu utashinda. Simama tu endelea kudai haki yako mbele za Mungu kam Ayubu alivyo simama. Hakutenda dhambi hatakma alipt katka Magumu.. usi lalamike mbele za Mungu si mama na BWANA naye ata kushindia Mwachie YESU kila kitu chako yeye ni mshindi ugumu wowote yeye ni msindi..Mungu ni mwema saana hawezi kumuacha mwenye haki wake afe. Jikaze,jivute simama IMARA atakushindia na wew utarudishiwa mara saba...Mungu akutie nguvu na akuinue ktka maisha yako yoote na uwe mshindi..MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI AAMEEEEE'''''' BY MW EVELIN G. MANASE FPCT -TEGETA
Saturday, 30 August 2014
HILI NDIO TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA
JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA
TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU MCHAKATO WA
KATIBA
Sisi, wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania,
tuliokutana tarehe 27 hadi 28 Agosti, 2014, Dar es salaam , tumepata fursa ya
kutafakari, kujadili na kujielimisha kwa kina yaliyomo katika Rasimu ya pili ya
Katiba na mjadala unaoendelea katika Bunge Maalum la Katiba.
Baada ya mjadala wa kina, tunatoa tamko letu kama ifuatavyo:
- Tunaipongeza
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilikusanya Maoni ya
WANANCHI kuhusu mabadiliko hayo na kutuletea Rasimu yenye maoni mengi ya
Watanzania bila kujali dini zao, upande wa Muungano walikotoka, hali zao
za kimaisha, jinsi na kabila.
- Pia
tunaipongeza Tume kwa kuandaa nyaraka na kumbukumbu mbalimbali kama
Randama, Nyaraka zenye maoni ya wananchi, picha, tafiti mbalimbali na hata
orodha ya watu walioshiriki kutoa maoni katika Tume. Tume pia iliweza
kuandaa Tovuti iliyokuwa na kumbukumbu za Tume na Maoni yote yaliyotolewa.
Kazi hii ni ushahidi kuwa Tume iliandaa Rasimu kwa weledi na kwa mujibu wa
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuzingatia maoni ya WANANCHI.
- Tume
imedhihirisha kuwa, ilitenda KIZALENDO na, kwa mantiki hiyo, wajumbe wote
bila kujali vyama vyao, dini zao na upande wa Muungano walikotoka,
waliweza kujadili kwa uwazi na kweli na mwisho wakaridhiana katika kila
Ibara iliyopendekezwa. Hili linatufundisha kuwa Katiba ni MARIDHIANO na si jambo la
maslahi ya kisiasa, bali ni suala la maslahi ya WANANCHI.
- Tunaamini
kuwa kila Mjumbe wa Kamati ya kukusanya maoni ya WANANCHI aliheshimu kiapo
chake na hivyo kufanya kazi waliyokabidhiwa kwa uaminifu na uadilifu na ya
kwamba hawakushawishiwa au kupokea rushwa kutoka kwa kundi, dini au chama
chochote cha siasa wakati wa zoezi hili.
Baada ya Tume kuwasilisha Rasimu kwenye Bunge Maalum la
Katiba, Taifa likaanza kushuhudia “uasi wote na uovu wa wanadamu wapingao
kweli kwa uovu” (Warumi 1:18). Katika mijadala ya Bunge Maalum la
Katiba (BMK) yakaanza kujitokeza mambo mengi yasiyo ya maslahi kwa WANANCHI, na
ukiukwaji wa sheria na kanuni. Mambo kadhaa yanadhihirisha hili:
- Tovuti
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilifungwa bila sababu za msingi kutolewa
wakati mchakato unaendelea. Hali hii imefanya zile nyaraka na kumbukumbu
zilizoandaliwa kwa ajili ya rejea na kuwezesha mjadala wa Rasimu ya Katiba
kuendelea katika mwanga na ufahamu wa nyaraka hizo kutowezekana kabisa.
Kwa sababu hiyo, tumeona Bunge Maalumu la Katiba likiendelea kupotosha
takwimu na taarifa mbalimbali ambazo WANANCHI hawawezi kuzipata kwa ajili
ya kuoanisha baina ya kinachojadiliwa Bungeni na kilichomo katika Rasimu na
viambatanisho vyake vyote. Tunajiuliza jambo hili limefanywa na nani na
kwa maslahi ya nani?
- Bunge
la Katiba limeshindwa kusimamia Kanuni kama ambavyo zilipendekezwa na
kuridhiwa na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Kushindwa huku kusimamia
kanuni kumesababisha vurugu ndani ya Bunge Maalumu na kumekwamisha
matarajio ya wananchi kupata Katiba bora ya nchi yetu.
Matumizi ya ubabe na wingi wa Wabunge wa Chama Tawala (CCM), badala ya
Kanuni za Bunge na maridhiano, kumefanya mchakato wa Katiba kuhodhiwa na
Chama Tawala dhidi ya maslahi ya WANANCHI.
- Mijadala
katika Bunge Maalumu la Katiba imekuwa ya kejeli, matusi, vitisho, ubabe
na kupuuza hata kupotosha maoni yaliyotolewa na Wananchi kwa Tume. Hali
hii imelifanya Bunge Maalumu la Katiba kupuuzwa na hivyo kupoteza heshima
na hadhi yake. Matokeo yake baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wakaamua
kususia vikao vya bunge na wengine kuendelea, bila kukumbuka kuwa KATIBA
NI MATOKEO YA TENDO LA MARIDHIANO NA SI SUALA LA MASLAHI YA KIKUNDI CHA
WATU WACHACHE.
- Hatua
iliyofikiwa ni dhahiri, Mjadala wa BMK unaoendelea umeondoa kwa kiasi
kikubwa maoni yaliyotolewa na wananchi kuhusu muundo wa Muungano,
kupunguza mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge, ukomo
wa ubunge, n.k., na kuwezesha maoni na maslahi ya Chama Tawala kwa uongozi
wa kikundi cha wanasiasa wachache wasio na uaminifu na uadilifu wa kutosha
kuwekwa kama mapendekezo ya Katiba mpya kwa nia ya
kulinda maslahi binafsi au ya makundi na kuhalalisha ukiukwaji mkubwa wa
sheria, kanuni na maadili ya uongozi bora.
Baada ya kujadili na kuona haya na mengine mengi, Jukwaa la
Wakristo Tanzania lina maoni yafuatayo;
1. Kwamba Serikali (Wizara ya Katiba na Sheria) irudishe
tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na nyaraka zake zote kwa ajili ya wananchi
kuendelea kuona kazi waliyoifanya, kujifunza na kujadili Rasimu ya Katiba kwa
uwazi.
2. Kwamba maoni ya wananchi hayawezi kufutwa na kudharauliwa
na Chama Tawala. Hivyo basi, Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea lijadili na
kuboresha tu maoni yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na sio kufanya mabadiliko
katika Katiba ya mwaka 1977.
3. Kwamba mchakato wa Katiba usimamishwe ili kupisha
majadiliano, maelewano na maridhiano muafaka, uchaguzi mkuu na wa serikali za
mitaa. Na mabadiliko ya Katiba ya 15 ya mwaka 1977 yafanyike kuwezesha chaguzi
kufanyika kwa uwazi na haki. Pia, kuweka kifungu kitakacholinda Rasimu ya pili
na kumtaka kiongozi ajaye kuendelea na mchakato wa Katiba.
4. Kwamba baada ya Bunge Maalum la Katiba kuanza shughuli
zake tena, Mwenyekiti wa Bunge hilo afanye kazi kwa mujibu wa kanuni na Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba badala ya kutumia ubabe na kiburi cha wingi wa wajumbe
wa Chama cha Mapinduzi katika Bunge la Katiba.
5. Kwamba wananchi waendelee kusoma na kujadili maoni
yaliyoko katika Rasimu ya pili ya Katiba, na kufuatilia kitakachokuwa
kinajadiliwa kwenye Bunge la Katiba ili kuwawezesha kupiga kura ya maoni wakiwa
na uelewa wa kutosha kabisa kuhusu ni nini kipo kwenye “Katiba
inayopendekezwa”. Wananchi pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa nia ya
kuwawezesha kupiga kura ya maoni.
6. Kwamba tunaomba Tume ya Mabadiliko ya Katiba ihuishwe na
kupewa mamlaka kisheria ili kuiwezesha kujibu maswali yanayojitokeza na kutoa
ufafanuzi kwa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa jumla hadi Katiba Mpya
itakapokamilika na kukabidhiwa rasmi.
Jukwaa la Wakristo Tanzania na Watanzania wote wanaoitakia
nchi yao mema, tunakuomba Mheshimiwa Rais kwamba AMANI ya nchi yetu sasa imo
mikononi mwako hasa katika kipindi hiki cha kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Tunakuomba uahirishe mchakato unaoendelea ili uepushe ishara za aina mbalimbali
za kuanzisha sintofahamu nchini mwetu na hali yoyote inayoweza kuathiri vibaya
mshikamano, umoja na amani ya Taifa letu.
Ifahamike kuwa WANANCHI wa Tanzania wako juu ya Wajumbe wa
Chama cha Mapinduzi. Kwa mantiki hiyo, tunakuomba uepushe WANANCHI wa Tanzania
kuhamasishwa kukikataa Chama cha Mapinduzi kwa kuwa tu Chama hicho kimeyapuuza
na kimekataa Maoni yao waliyotoa kwa dhati baada ya kuaswa na kuhimizwa kufanya
hivyo na viongozi wa nchi.
“Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao,
Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye yasiyowapasa. Wamejawa na
udhalimu wa kila namna, uovu na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya,
wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye
kutabakari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio
na ufahamu, wenyekuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; si
hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”. (Rejea Warumi 1: 28-32)
IKUMBUKWE KUWA RASIMU YA PILI YA KATIBA NI WARAKA HALALI
NA RASMI NA NDIYO MAWAZO YA WATANZANIA NA TUNAHIMIZA KUWA KATIBA NI YA WANANCHI
NA INAHITAJI MARIDHIANO NA SIO UBABE.
Thursday, 28 August 2014
HATARI MTANDAO WA DINI YA SHETANI WAJITANGAZA AFRIKA MASHARIKI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtandao
mmoja nchini Kenya unaoendesha shughuli zake nchini Kenya kuanzia Februari 23
mwaka jana, umetoa tangazo linalowataka watu kujiunga na dini inayomwabudu
Shetani, ikiwa wazi kwamba imekuwa ikiwaingiza Watanzania katika mtandao wake.
Kupitia mtandao huo ambao kwa hekima blog hii linauhifadhi, dini hiyo imetoa tangazo lenye mvuto wa aina yake ikijinadi kwamba ina uwezo wa kumpatia mtu atakayetimiza masharti ya kujiunga nayo kiasi cha shilingi milioni 50.
Kupitia mtandao huo ambao kwa hekima blog hii linauhifadhi, dini hiyo imetoa tangazo lenye mvuto wa aina yake ikijinadi kwamba ina uwezo wa kumpatia mtu atakayetimiza masharti ya kujiunga nayo kiasi cha shilingi milioni 50.
“You can join and get sh.50 Milion”, sehemu ya tangazo la dini hiyo linaeleza
kwa lugha ya Kiingereza, likimaanisha kwamba atakayefanikiwa kujiunga atapatiwa
shilingi milioni 50 za Kenya.
Tangazo la dini hiyo likiwa na nembo yake yenye umbo la duara na alama ya nyota katikati linaeleza jinsi dini hiyo iliyojisheheneza nchini Kenya na kufanikiwa kuwapata wafuasi kutoka Tanzania kuanzia Februari 23 tangu mwaka 2013.
Tangazo la dini hiyo likiwa na nembo yake yenye umbo la duara na alama ya nyota katikati linaeleza jinsi dini hiyo iliyojisheheneza nchini Kenya na kufanikiwa kuwapata wafuasi kutoka Tanzania kuanzia Februari 23 tangu mwaka 2013.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, nchi ya Kenya yenyewe iliwahi kushangazwa na jinsi ambavyo dini hiyo imepenya na nchini humo na kupata mafanikio.
“…took the country by storm which raised the question of how well organized the secret societies associated with devil worshipping are in Africa”, linaeleza tangazo hilo kwa Kiingereza likimaanisha jinsi ambavyo dini hiyo ya siri inayojihusisha na ibada za kishetani barani Afrika ilivyowahi kuifanya Kenya namna ilivyoweza kujiendesha nchi humo.
Gazeti moja la kila siku linalochapishwa nchini humo, likizungumzia dini hiyo katika moja ya makala zake lilieleza kuwa jumuiya za siri za Waabudu Shetani nchini Kenya huundwa na Wakenya wanaopendelea jambo hilo.
Aidha ililiweka wazi kuwepo kwa mtandao unaotoa mahubiri na pia kuonesha ibada za kishetani huku pia zikijitangazia watu wajiunga na dini hiyo.
Gazeti hilo liloandika kwamba kwamba mtandao huo huwataka watu wanaotaka kujiunga wanapaswa kuuza nafsi zao.
Gazeti hilo linalochapishwa kila siku Jijini Nairibi nchini Kenya, lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa watu waliojiunga na dini hiyo aliyekataa kutaja jina lake,ambapo alibainisha kwamba ni kweli kiasi kikubwa cha fedha hutolewa kwa mtu anayejiunga nao.
Alisema mtu huyo hupatiwa kiasi hicho cha fedha baada ya kutumiza masharti muhimu na kukubaliwa uanawachama kwa vigezo maalumu ambayo sio kila mtu anaweza kuvitimiza.
Fomu maalumu ya kwa mtu anayejiunga na dini hiyo, inamtaka akubali kuuza nafsi yake kwanza.
Pamoja mambo mengine mengi, fomu hiyo inaeleza kwamba mtu anayeuza nafsi yake ni lazima akubali kujitoa kikamilifu na kuitumikia dini hiyo kwa milile hata katika kifo.
Aidha fomu hiyo inamtaka mtu anayejiunga kujaza fomu kwa hiyari yake na kuwa na uelewa wa anachokifanya anachokifanya, ikiwemo mambo yatakayomtokea ikiwa itaachana na dini hiyo.
Uwepo watu wanaodaiwa kumwabudu shetani sio jambo geni kusikia nchini Kenya na Tanzania, ukiacha mataifa ya Marekani na Ulaya ambayo ni kitu cha kawaida, lakini suala la dini hiyo kujitangaza na kuelekeza nguvu zake nchini Tanzania ni suala linalopaswa kuchukuliwa tahadhari.
Akizungumza na fpct blog mmoja wa wachungaji waandamizi anayechunga kanisa moja kubwa Jijini Dar es Salaam, alisema tangu zama za kale wafuasi wa Shetani walikuwepo na watu hivyo kinachotakiwa ni kwa wachaMungu kulitambua hivyo na kushika nafasi zao katika kuhubiri Injili na kuwavuta watu kwa Yesu ili waepuke hila za shetani katika kuwateka na hatimaye kuwaangamiza.
Kwa sharti la kutotajwa jina lake mtandaoni, alisema kuwa waabudu shetani wako wengi ulimwenguni, wakitumia hata huduma na imani tata zinazojitangaza kuwa za Kikristo.
Alisema ndio maana katika mataifa ya barani Ulaya na Marekani ni jambo la kawaida kukuta mtu anasoma Biblia ya Kishetani akiamini kwamba ndiye mungu wake anayepaswa kumwabudu.
“Jambo hilo linamaanisha kwamba waabudu Shetani wapo na ndio maana hata
wamechapisha Biblia zao.Kwa kweli dunia ipo katika nyakati za mwisho
zilizotabiriwa katika Biblia, hivyo umakini unahitajika sana”, alisema
Mchungaji huyo.
Monday, 25 August 2014
TAZAMA PICHA NAMNA SHEREHE ZA KUWASIMIKA NA KUWABARIKI WACHUNGAJI NA WAZEE WA KANISA ZILIVYOFANA JANA KATIKA KANISA LA FPCT MISSION YA MSANGA
Watu walikuwa wengi si mchezo
lazima upitie hapa ndo uingie kanisani
kulia ni mchungaji Joram Jeremiah Ntaseha wa fpct tegeta na mzee wa kanisa Kaponda wa msasani
mchungaji Joram Jeremiah Ntaseha
Roho mtakatifu nae alichukua nafasi yake
mtumishi wa Mungu aliyekuwa mwalimu wa semina katika zoezi la kuwabariki wachungaji
askofu Revert Kamonongo akifatilia kwa umakini mambo yalivyokuwa yanaendelea
kumsifu Mungu ilikuwa nzuri sana
ASKOFU Revert Kamonongo akiteta jambo na viongozi wa makao makuu fpct
lazima upitie hapa ndo uingie kanisani
kulia ni mchungaji Joram Jeremiah Ntaseha wa fpct tegeta na mzee wa kanisa Kaponda wa msasani
mchungaji Joram Jeremiah Ntaseha
Roho mtakatifu nae alichukua nafasi yake
mtumishi wa Mungu aliyekuwa mwalimu wa semina katika zoezi la kuwabariki wachungaji
askofu Revert Kamonongo akifatilia kwa umakini mambo yalivyokuwa yanaendelea
kumsifu Mungu ilikuwa nzuri sana
ASKOFU Revert Kamonongo akiteta jambo na viongozi wa makao makuu fpct
Saturday, 23 August 2014
JICHO LA MBALI
HII NDIO HISTORIA YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI REBECCA MALOPE
REBECCA Malope wengi akijulikana kama Malkia wa
muziki wa injili Afrika amezaliwa 1968 katika kijiji cha Lekazi karibu na mji
wa Nelsprut, Mpumalanga.
Historia ya mwimbaji huyo ambayo si nzuri kimaisha kwani
Malope hakuendelea sana katika elimu na ni mambo machache sana yanafahamika
kuhusiana na enzi za utoto wako.
Akiwa katika umri mdogo Malope alipata ugonjwa uliopelekea
kutoweza kutembea na madaktari walidhani asingeweza kutembea tena katika maisha
yake .
Familia yake ilikuwa masikini sana na ndipo yeye na dada
yake Cynthia waliamua kukimbilia katika jiji la Johannesburg kitongoji cha Evaton
kwa ajili ya kutafuta kazi kujikimu na maisha.
Mwaka 1986 Malope akiwa na miaka 21 alishirika kwenye
mashindano ya kutafuta vipaji vya uimbaji yaliyojulikana kama ‘Shell Road to
Fame’ lakini hakufanikiwa kufika mbali.
Malope hakukata tamaa ndipo mwaka uliofuata alishiriki tena
na kuibuka mshindi na wimbo wa ‘Shine on’ ushindi huo ulimsogeza mbali sana
kimuziki na ndipo alipokutanishwa na muandaaji mashuhuri Sizwe Zako na akapata
meneja wake wa kwanza akijulikana kwa jina la Peter Tladi.
Albamu yake ya kwanza ilikuwa na nyimbo za kidunia, albamu
hiyo ambayo haikufanya vizuri sokoni na ndipo alipoamua kujiingiza moja kwa
moja kwenye muziki wa injili.
Alipata ushirikiano mkubwa sana kutoka radio mbalimbali kwa
nyimbo zake za injili kitu ambacho hakikuwa kawaida sana Afrika Kusini.
Mwaka 1990 Rebecca alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa
kike wa Afrika Kusini,na mwaka 1993 ilikadiriwa watu zaidi ya milioni moja
walimpigia kura kama mwanamuziki bora wa kike kwenye Coca Cola Full Blast Music
Award Music Show na alishinda kwa mwaka huo na 1994 pia. Kwenye mauzo, Album
zake zote kumi za kwanza ziliingia kwenye hadhi ya dhahabu.
Katika kipindi chote nakala zaidi ya milioni 2 zilikuwa
zimeshauzwa sokoni.Mwaka 1995 kwenye CD yake ya Shwele Baba nakala zadi ya
milioni moja ziliuzwa ndani ya wiki tatu toka uzinduzi wake na hii iliweka
rekodi ya aina yake katika historia ya soko la muziki Africa kusini.
Mwaka 1996 haukuwa mwaka mzuri kwa Rebecca kwani alimpoteza
baba yake mzazi, kaka yake na dada yake. Wote walifariki katika mazingira ya
kutatanisha wakifuatana.
Lakini hili halikumfanya Rebecca kukata tamaa na kuacha
huduma bali alisonga mbele na kazi hiyo akijipa moyo na kuamini ni mpango
kutoka kwa Mungu mwenyewe na hataacha kumtumikia.
Rebecca anasema siri ya mafanikio yake ni kujituma, kuwa na
malengo na kufanya kazi kwa bidii akimshirikisha Mungu hayo ndiyo yaliyomfanya
kutawazwa Malkia wa muziki wa injili Afrika huku wengi wakimfananisha na
marehemu Brenda Fassie.
Kati ya mwaka 1995 na 2004 Rebecca amezunguka ulimwenguni
akiwa na bendi ya Pure Magic akimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.
Mwaka 2003 Malope alitunukiwa udaktari wa heshima kutoka
chuo kikuu cha Natal kwa mchango wake mkubwa kwa jamii na muziki nchini Afrika
kusini, na Desemba mwaka huo huo alishinda tuzo ya Kora kwa upande wa
mwanamuziki bora wa Injili.
Katika wanamuziki ambao alishirikiana nao kwa karibu sana na
wamekuwa na mchango mkubwa kwake ni pamoja na marehemu Vuyo Mokoena.
Mwaka 2004 Malope alianzisha kipindi chake katika runinga
kikiitwa ‘Gospel time’ ambacho kinafanya vizuri sana.
Mwaka huu februari 25 Malope amerekodi nyimbo za live katika
jiji la Pretoria hiyo ikiwa ni albamu ya 32.
Baadhi ya Tuzo ambazo Dkt. Rebecca Malope amewahi kutunikiwa
ni 1994 mwimbaji bora, 1997 albamu bora sokoni iliyoitwa Uzube Nam, 1998
muimbaji bora wa nyimbo za injili Afrika na albamu bora katika mauzo iliyoitwa
Angingedwa.
Nyingine ni 1999 muimbaji bora wa kike na muimbaji bora wa
injili Afrika kupitia albamu ya Somlandela, 2002 msanii bora wa nyimbo za
injili akishinda na wimbo wa Sabel Uyabizwa, 2003 msanii bora Afrika kupitia
wimbo wake wa Iyahamba Lenqola na 2004 msanii bora wa mwaka kwa wimbo wake
Hlala Nami.
Huyo ndiyo Rebecca Malope ambaye ni kipenzi cha Rais wa
kwanza wa frika Kusini Nelson Mandela na rais wa sasa Jacob Zuma ambaye
amepitia tabu na changamoto nyingi katika maisha.
Subscribe to:
Posts (Atom)



