Monday, 20 July 2015
Monday, 13 July 2015
MAJAMBAZI YATIWA NGUUVUNI MCHANA HUU DAR,
Ni kundi la majambazi linalo kadiliwa kuwa na idadi ya watu nne(4) lililokuwa likipora kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa mtu ambaye hajaweza kutambulika jina kwa Haraka,Ilikua katika mitaa ya mnara wa saa maeneo ya Stesheni jiji Dara es salaam. Baada ya polisi (askali kanzu)kuwatilia mashaka watu hao iliwalazimu kuwafuata mjambazi hayo na kuanza kurushiana risasi na wengine kujificha chini ya tex zilizokuwa zimepaki katika eneo hilo. Baada ya mapigano hayo polisi walifanikiwa kuwatia nguvuni wote.
Wednesday, 8 July 2015
MAMBO YAMEPAMBA MOTO, FPCT BOKO YAZIDI KUCHANJA MBUGA SASA.
Hili ni kanisa la kipentekoste linaloitwa FPCT BOKO (FREEPENTECOSTELCHURCH OF TANZANIA- BOKO) linalochungwa na mtumishi wa Mungu Mchungaji na Mwinjilisti anaye tumiwa na Mungu kwa viwango vya juu isivyo kawaida Mch: ELIJAH MTISHIBI na kamati nzima ya uongozi wa kanisa hilo.
Ni hatua ambayo inaendelea kumpa Mungu utukufu kwani kanisa hilo linazidi kusonga mbele zaidi ni takribani miezi sita(6) na wiki kadhaa tangu kanisa hilo lianzishwe,Lakin huwezi kuamini na utabaki unamshangaa Mungu kwa kazi na matendo yake anayoyafanya ndani ya kanisa hilo.
Kwakipindi hicho chote tangu kanisa lianzishwe watu wenye shida na mahitaji mbalimbali wameendelea kupokea majibu yao huku wagonjwa wenye magonjwa sugu wameendelea pia kufunguliwa siku hadi siku huku idadi wa waumini ikiongezeka kwa kasi.
Hayo na mengine mengi ni vitu ambavyo vinaendelea kumpa Mungu utukufu kila uchwao.
Karibu uungune na watumishi wa Mungu katika kanisa la FPCT BOKO kwa maombi na maombezi,matatizo mbalimbali ya kiroho na ya kimwili pia karibu uonane na watumishi wa Mungu watakusaidia.
Jinsi ya kufika:-
Kama watokea MWENGE,AFRICANA,MBUYUNI,TEGETA na kwingineko panda magari yaendayo Bunju au Bagamoyo Pia kama watokea Bagamoyo,Bunju panda gari za Mwenge au Tegeta shuka kituo cha BOKO KWA MPEMBA,ikiwa umetoka mwenge usivuke lakini kama watokea Bagamoyo vuka utaona kibarabara ya vumbi,tembea mbele nusu km utakutana na kibao kinachoelekeza kanisa lilipo hapo utakua umefika.

![]() |
| Mchungaji Mtishibi kushoto akiwa na Mwimbaji Masanja Mkandamizaji. |
![]() |
| Mch Mtishibi Akiwa madhabahuni akifundisha. |
![]() |
| Moja ya sehemu ya waumini wa Kanisa la FPCT BOKO wakiwa madhabahuni wakimsifu Mungu. |
![]() |
| Picha ikionesha moja ya mkutano aliowahi kuhubili mtumishi wa Mungu Mch ELIJAH MTISHIBI. Katika mkutano huo watu wengi walifunguliwa, Sifa na utukufu kwa Mungu. |
![]() |
| Mch ELIJAH MTISHIBI |
![]() |
| Mchungaji ELIJAH MTISHIBI akiwa katika picha ya furaha sana |
![]() |
| Baadhi ya waumini pia wakiwa katika sifa. |
![]() |
| Moja ya team ya vijana washilika wa kanisa la fpct Tegeta Ni team inayofanya kazi kwa pamoja na ushirikiano wa karibu na kanisa la FPCT BOKO. |
Thursday, 2 July 2015
KARIBU USHIRIKI BARAKA ZA MUNGU KATIKA IBADA ZA KANISA LA FPCT TANDALE -TANESCO
Mchungaji JUSTINE MISIGARO wa kanisa la FPCT Tandale- Tanesco Jijini Dar sa salaam, Anawakaribisha watu wote waishio Dar es salaam na maeneo jirani ya mkoa huo, kufika na kuwatembelea katika ibada za kanisani hapo ili kushiriki Baraka za Mungu kwa pamoja,.
Karibu sana pindi upatapo fursa.
Na hiii ni ratiba za ibada katika kanisa hilo.
Jumatano kuanzia saa 10;00 alasiri -12;00 jioni ni Mafundisho ya Biblia na Neno la Mungu.
Injumaa kuanzia saa 10;00 alasiri -12;00 jioni ni maombi na maombezi.
Juma mosi kuanzia saa 08;00 mchana 11;00 Ni ushauri wa kiroho kuonana na mchungaji moja kwa moja. Pia Juma mosi kuanzia saa 10;00 - 01;300 ni mazoezi ya kwaya.
Na jumapili saa 03;15 - saa 07;30 ni Ibada kuu iliyojaa nguvu na matendo makubwa ya Mungu.
Kwa mawasiliano na ushauri wa mambo mbalimbali, wasiliana na mch Misigaro kwa
+255 685 590 048
Karibuni sana.
![]() |
| MCH ; JUSTINE MISIGARO WA KANISA LA FPCT TANDALE-TANESCO AKIWA MADHABAHUNI . |
![]() |
| Mama Mchungaji wa kanisa la FPCT Tandale Tanesco Bi, Rehema Misigaro. |
![]() |
| Hawa ni moja kati ya vijana wa kundi la sifa na kuabdu na msimamizi wa mitambo. |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Monday, 29 June 2015
MSANII WA BONGO MOV STEVE NYERERE AJITOSA,ATANGAZA NIA YA UBUNGE
Ni siku kadhaa zimepita tangu msanii wa maigizo (bongo mov) Wema Sepetu aoneshe nia ya kutaka kuteuliwa na chma cha mapinduzi(ccm)kimptishe ili aweze kugombea ubunge katika jimbo la Singida mjini. Sasa hali hiyo imeamsha ari kwa msanii mwingine tena wa tasnia hiyo ya maigizo(Bongo mov) Steven Mengele(Steve Nyerere) Amejitosa kutangaza nia kuptia chama cha mapinduzi (CCM) kiweze kumteuwa iliaweze kuipeperusha bendela ya chama hicho katika jimbo la Kinondoni. Msanii huyo ameamua kutangaza nia mwishoni mwa juma lililopita, wakati alipokuwa katika viwanja vya Bwawani Kinondoni akiongea na wananchi akiwahamasisha wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftali la kudumu la wapiga kura,
Sambamba na hilo Msanii huyo Steven Mengele (Steven Nyerer) alisema kuwa ikiwa atapewa ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto zinazo wakabili wananchi wa jimbo hilo la Kinondoni.
Pamoja na hayo alizitaja baadhi ya kero kuwa ni pamoja na miuondombinu mibovu,Uhaba wa maji,Masoko ya kudumu wamachinga na mama ntilie,Ajira kwa vijana nk. Pia aliwaomba wanachi wasisite kumchagua kwenye uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu, endapo chama chake kitamptisha.Hivyo aka sisitiza kuwa wananchi wa jimbo la Kinondoni wapaswa kuish maisha ya raha na Amani kwakutatuliwa matatizo yao.
Sambamba na hilo Msanii huyo Steven Mengele (Steven Nyerer) alisema kuwa ikiwa atapewa ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto zinazo wakabili wananchi wa jimbo hilo la Kinondoni.
![]() |
| STEVE NYERERE Akiwasili kwenye viwanja vya Bwawani kwaajili ya kuzungumza na wananchi |
![]() |
| STEVE NYERER akipongezwa kwa uamuzi alio ufanya |
![]() |
HUJAFA HUJAUMBIKA,OMBA YASIKUKUTE
![]() |
![]() |
| Akizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na wandishi wa habari Bi GRACE KAIZA mkazi wa Igoma mjini Mwanza ambaye ameomba kusaidiwa na watu mbalimbali kutokana na tatizo alilonalo la mguu wake kuugua ugonjwa wa kansa(saratani) unao msumbua kwa muda wa miaka kadha sasa tangu aupate ugonjwa huo. Anasema chanzo ilitokea uvimbe kama upele kidogo tu kwenye mguu wake, kadili kilivyo endelea kukua kipele ndivyo kiliendelea kuleta madhala licha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa. Amehangaika kwa muda mrefu akitafuta matibabu ya ugonjwa huo lakini hakuna mafanikio yoyote,hali inayo mlazim sasa kukatwa mguu wake huo. Hivyo ameomba msaada kwa wadau na watu mbalimblali wajitokeze kumchangia pesa ili aweze kukatwa mguu wake na aweze kuunusuru uahai wake,. Kwa yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaombwa kmsaidia kumchangia mchango kwa kuptia M pesa simu No - 0768 264 182 |
Sunday, 21 June 2015
MWIMBAJI MILCA KAKETE AZINDUA ALBAM MBILI MKUPUO NDANI YA VCCT CHURCH-MBEZI
Ilikua ni ibada maalum ya uzinduzi wa album mbili za mwimbaji wa kimataifa Milca Kakete uliofanyika katika kanisa la vcct Mbezi Dare es salaam Tanzania. Mwimbaji huyo alisindikizwa na waimbaji mbalimbali kama vile D.G.C. CHOUR,VOICE AKAPELA,MILIAM LUKINDO na wengine weengi,
Ikumbukwe lengo la mwimbaji huyo Milca kufanya uzinduzi ni kutafuta pesa ambazo zitawasidia watumishi (wachungaji)wanaofanya kazi ya Mungu katika mazingira magumu hasa wale wakao vijijini ili waweze kuwezeshwa katika nyanja mbalimbali za kihuduma, Ambapo kiasi kadhaa cha pesa kiliweza kupatikana ili kusapoti huduma hiyo, Pia mwimbaji huyo ametoa wito kwa watumishi na wadau wote wenye moyo wa kumtumikia Mungu wajitokeze kumuunga mkono ili waweze kuwasaidia watumishi wengine weengi zaidi kwa wakati mmoja,.
Mchungaji Dr Huruma Nkone aliye shikilia mic,Mch Samwe(Katikati) na Mch Safari wate kwa Pmoja wakifanya maombi rasimi kwaajili ya kuziweka wakfu dvd za mwimbaji Milca Kakete ili ziweze kuanza kusikilizwa na kufanyiwa changizo maalum.
Mch Dr Huruma Nkone (kushoto) akiwa nana mkewake.
Wakwanza kushoto ni mch Safari wa kanisa la D P C jijini Dar na Milca Kakete akiteta jambo na mmoja wa marafikizake wa karibu sana waliohudhulia ukumbini
Mama yake mzazi wa Mwimbaji Milca Kakete aki mkumbatia mmoja ya wanafamilia baada ya kutoka jukwaani alipokua akitoa neno la shukrani kwa Mung,Huwezi aminin aliweza kudondosha chozi la furaha kwakitendo alicho kishuhudia,kwani ilikua ni moja ya maombiyake kwa Mungu ampatie japo hata mmoja ya watoto wake atakae weza kuwamrithi wake,kwani na yeye ni mwimbaji wa miaka mingisaana. Licha ya kuwa mzee sasa lakini Bado anamtumikia Mungu kwa Uimbaji.
Mama yake mzazi wa Milca Kakete akitoa shuuda na shukrani.Aliye mshikia Mic ni Mch Samwel
Mwimbaji Milca Kaketi akiwa katika hari ya utulivu akifuatili uimbaji.
Ikumbukwe lengo la mwimbaji huyo Milca kufanya uzinduzi ni kutafuta pesa ambazo zitawasidia watumishi (wachungaji)wanaofanya kazi ya Mungu katika mazingira magumu hasa wale wakao vijijini ili waweze kuwezeshwa katika nyanja mbalimbali za kihuduma, Ambapo kiasi kadhaa cha pesa kiliweza kupatikana ili kusapoti huduma hiyo, Pia mwimbaji huyo ametoa wito kwa watumishi na wadau wote wenye moyo wa kumtumikia Mungu wajitokeze kumuunga mkono ili waweze kuwasaidia watumishi wengine weengi zaidi kwa wakati mmoja,.
Mchungaji Dr Huruma Nkone aliye shikilia mic,Mch Samwe(Katikati) na Mch Safari wate kwa Pmoja wakifanya maombi rasimi kwaajili ya kuziweka wakfu dvd za mwimbaji Milca Kakete ili ziweze kuanza kusikilizwa na kufanyiwa changizo maalum.
Mch Dr Huruma Nkone (kushoto) akiwa nana mkewake.
Mama yake mzazi wa Mwimbaji Milca Kakete aki mkumbatia mmoja ya wanafamilia baada ya kutoka jukwaani alipokua akitoa neno la shukrani kwa Mung,Huwezi aminin aliweza kudondosha chozi la furaha kwakitendo alicho kishuhudia,kwani ilikua ni moja ya maombiyake kwa Mungu ampatie japo hata mmoja ya watoto wake atakae weza kuwamrithi wake,kwani na yeye ni mwimbaji wa miaka mingisaana. Licha ya kuwa mzee sasa lakini Bado anamtumikia Mungu kwa Uimbaji.
Mama yake mzazi wa Milca Kakete akitoa shuuda na shukrani.Aliye mshikia Mic ni Mch Samwel
Mwimbaji Milca Kaketi akiwa katika hari ya utulivu akifuatili uimbaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)