Monday, 29 June 2015

MSANII WA BONGO MOV STEVE NYERERE AJITOSA,ATANGAZA NIA YA UBUNGE

Ni siku kadhaa zimepita tangu msanii wa maigizo (bongo mov) Wema Sepetu aoneshe nia ya kutaka kuteuliwa na chma cha mapinduzi(ccm)kimptishe ili aweze kugombea ubunge katika jimbo la Singida mjini. Sasa hali hiyo imeamsha ari kwa msanii mwingine tena wa  tasnia hiyo ya maigizo(Bongo mov) Steven Mengele(Steve Nyerere) Amejitosa kutangaza nia kuptia chama cha mapinduzi (CCM) kiweze kumteuwa iliaweze kuipeperusha bendela ya chama hicho katika jimbo la Kinondoni. Msanii huyo ameamua kutangaza nia mwishoni mwa juma lililopita, wakati alipokuwa katika viwanja vya Bwawani Kinondoni akiongea na wananchi akiwahamasisha wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftali la kudumu la wapiga kura,
   Sambamba na hilo Msanii huyo Steven Mengele (Steven Nyerer)  alisema kuwa ikiwa atapewa ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto zinazo wakabili wananchi wa jimbo hilo la Kinondoni.
STEVE NYERERE  Akiwasili kwenye viwanja vya Bwawani kwaajili ya kuzungumza na wananchi
STEVE NYERER akipongezwa kwa uamuzi alio ufanya

 Pamoja na hayo alizitaja baadhi ya kero kuwa ni pamoja na miuondombinu mibovu,Uhaba wa maji,Masoko ya kudumu wamachinga na mama ntilie,Ajira kwa vijana nk. Pia aliwaomba wanachi wasisite kumchagua kwenye uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu, endapo chama chake kitamptisha.Hivyo aka sisitiza kuwa wananchi wa jimbo la Kinondoni wapaswa kuish maisha ya raha na Amani kwakutatuliwa matatizo yao. 

No comments:

Post a Comment