Tuesday, 31 March 2015

ASKOFU GWAJIMA AACHIWA KWA DHAMANA

Askofu Josephat Gwajima wa ufufuo na uzima
Hatimae sakata la Askofu  mkuu Wa kanisa la  ufufuo na uzima la jijin dar es salaam Josephat Gwajima, linaendelea kutoa picha flan machoni pa wa Tanzania na wana dunia kwa ujmla baada ya kuachiliwa nje kwa  dhamana yeye na wachungaji wake 15 waliokua wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa makosa tofauti tofauti likiwemo la kutoa maneno makali kwa Askofu mkuu wa Kanisa Ktoliki Tanzania Ask Pengo na lile la baadhi ya wachungaji  kudaiwa kutaka kumtorosha askofu Gwajima wakati alipokua amelazwa katika hosptali ya TMJ ya Dar es salaam.  Chanzo cha habari kutoka katika kanisa hilo kimeeleza,. 

JUBILEE YA MIAKA 80 KANISA LA FPCT BIGABIRO


Monday, 30 March 2015

IDARA YA UMOJA WA AKINA MAMA FPCT TEGETA WAFANYA SHANGWE NA BONGE LA SAPLAIZ (SUPRISE)

Neno la Mungu linasema ajitengea na wenzake hutaka matakwa yake mwenywe. Lakini kwa upande huohuo ni heri kuwa na uoja kuliko kujitenga. Hayo ni maneno yaliyo semwa na mwenyeki wa idara ya akina mama wa Kanisa la FPCT TEGETA MACHINJIONI Mrs Revina Majoro, jumapili ya jana wakati walipokua na hafra fupi ya kutianamoyo na kupongezana baada ya kuombeana kwa muda wa zaidi ya wiki tatu ndani ya idara hiyo.

Nduguzangu waumini na akina mama kwa ujumla ni kwa muda wa takribani wiki tatu tumekua na zoezi la kuombeana kila mwana idara akimuombea mwenzake, tuliandika majina ya wana idara nakisha tukayaweka kwenye kikapu kila mtu akawa anakuja kuchagua karatsi lenye jina,kila aliye chukua jina hilo basi alienda kuliombea/kumwomea mwenzake ili Mungu aweze kumjibumahitajiyake, kama Ndoa,afya,masomo,familia nk,tumemwona Mungu akijbu sana maombi yetu hata kabla ya kuhitimisha wiki hizi za maombi,na sasa leo ndiyo hitimisho la maombi yetu na Sasa kila mmojawetu ameandaa zawadi ya kumpongeza mwenzake. Alisema Mrs Majoro akifafanua zaidi.

 Angalia  na Tazama Picha  namna jinsi Hafra fupi ilivyo kua siku ya janaa.













 

Wednesday, 11 March 2015

HUIMA..HUDUMA YA INJILI MASHULENI YAZIDI KUSHIKA KASI JIJINI DSM

Kanisa la fpct tegeta jijini Dar es salaam limekuwa na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele lakini moja ya mikakati ni kuhakikisha injili inasambaa mashuleni na hili limeanza kufanikiwa baada ya kuanza kwenye baadhi ya shule za sekondari hapa jijini na jambo hili limekuwa likisimamiwa na mwinjilisti Jackob Lucas ambaye amekuwa akitoa huduma huku nguvu za Mungu zikionekana hasa baada ya wanafunzi wengi kufunguliwa kutoka kwenye nguvu za giza.

 ENDELEA KUTAZAMA PICHA WIKI HII ILIKUWA ZAMU YA Shule ya Sekondari Kisauke


                 wanafunzi wa shule ya sekondari kisauke jijini Dsm wakimuabudu Mungu



                                           EV.Jackob Lucas akifanya maombezi








                                  EV.Jackob Lucas Akifundisha neno la Mungu

Monday, 2 March 2015

WANAOWAUA ALBINO HAWAMJUI MUNGU KABISA;-ASEMA ASKOFU KUMENYA

Kauli hiyo imetolewa na Askofu mkuu wa Jimbo la Kigoma Ask Jeremiah Kumenya, alipokuwa katika kanisa la FPCT TEGETA-Machnjioni baada ya Ibada wakati akizungumza na mwandishi wetu pale alipotaka kuskia kauli ya kanisa na kauli ya Askofu akiwa ni kiongozi wa ngazi ya juu katika jimbo hilo Kuhusu sakata la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)nchini Tanzania

Askofu Kumenya alisema , lengo na kusudi la  Mungu kumuumba mwanadamu ni aishi milele na kumuabudu yeye.
Inapotokea mwanadamu amekufa basi awe Kafa kwa kifo cha kawaida ambacho ni  mpango wa Mungu kama yeye anavyo penda
 Lakini inasikitisha sana siku hizi wapo watu wanapanga njama kabisa za kuwaua Binadamu wenzao ambao wameumbwa na Mungu kama wao. 

Akiendelea mbele zaidi Askofu aliongeza kuwa  Ikitokea mtu anamuua mwenzake tena kwa ukatili na unyama usio semeka ifahamike moja kwa moja mtu huyo anamkosea Mungu na zaidi hamjui yeye aliye muumba na ambaye pia anayekataza mabaya Hasa kuua" alisema Askofu Kumenya.  
        
     Kuhusu watu wanao amini nguvu za giza/waganga ask Kumenya alisema ni Imani potofu kabisa ambazo hazina msaada kwa mtu yeyote aliyeumbwa na Mungu, Kwani haina sababu ya kuamini   kwamba kumuua mwenzako na kupata utajili si sahihi.  Tamaa ya utajili na uroho wa madaraka visiwe sababu ya kuwakatishia uhai binadamu wenzetu walioumbwa  na Mungu kama sisi." 
         Waganga wote wa kienyeji wanao hamasisha watu kufanya vitendo hivi waache mara moja kwani muda wao wa kufichuliwa na kupewa adhabu akali unakaribia.   

Kwa upande wa kanisa na wakristo wote nchini Askofu kumenya alisisitiza sana kuwa waendelee kushikamana kumwomba Mungu kwa kasi na juhudi zaidi, kwani Mungu anasikia kilio cha watu wake, maana Mungu anasema ikiwa watu wake watalia kwa bidii na kumpazia sauti atasikia. Taifa linapopita katika kipindi kigumu kama hiki ambapo watu wanakosa msaada na majibu ya matukio yao jukumu la kanisa ni kumuita Mungu mwenye majibu. 

Kanisa halipaswi kumnung'unikia wala kumlaumu mtu yeyote ila tunapaswa kumlilia Mungu atusaidie kutuokoa na roho chafu ya Mauti inayolinyemelea Taifa letu" alisema ask Kumenya. 
ASKOFU ; JEREMIAH  KUMENYA wa jimbo la Kigoma akiwa madhabahuni katika kanisa la FPCT TEGETA-Machinjion i ,wakati alipokuwa akihibiri, jana.( Picha na mwanahabari wetu Hossien Gabriel)
Mwisho kabisa Askofu Kumenya alitoa wito kwa wananchi na wasamalia wema wenye mapenzi ya dhati na wanaoumizwa na kukerwa na vitendo hivi kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Mauaji ya  walemavu wa Ngozi(Albino) Huku akiisisitiza Serikali na viongozi wote kuhakikisha wana simamia haki na ulinzi kwa kila Raia kwani ni haki yao kulindwa na  kupata usalama wakati wowote.