Friday, 22 January 2016

IKIWA BWANA AMETENDA KWANINI TUSIMSHUKURU?

Hili ndilo swali unaweza ukajiuliza sana mala kwa mala pale tu unapokumbuka BWANA alichokifanya katika maisha yako. Lakini pia wapo watu wengi ambao wanasahau sana mambo makubwa Ambayo BWANA mefafanya katika maisha yao.

Sasa basi kwakulijua hilo kwamba Mungu anapswa kushukuliwa kwakila jambo na hatua tuna vuka,Kanisa la FPCT BOKO Kwa ushrika Mkubwa wa kanisa la FPCT TEGETA-Machinjioni,wameandaa ibada kubwa ya sifa na Shukrani kwaajili ya kumshukuru Mungu kwakujibu Mahitaji yao meengi lakini kubwa likiwa ni kwamba Mungu amewawezesha kanisa la FPCT BOKO kwa Mpemba lilipo chini ya Mchungaji ELIJAH MTISHIBI kupata Vyombo vizuri vya na vya kisasa vya muziki..
 
Ibada hiyo itafanyika tar 31/01/2016.Kuanzia saa8:00mchana katika Kanisa la FPCT Boko kwa Mpemba. Wimbaji mbalimbali watakuwepo kumtukuza Mungu kama :- Nuru kwaya,Jerusalem kwaya, Esther Band Kutoka Gongo la Mboto,Kefas Jacksoni, na wengine wengi.

Usikoseeee!!,. Mtaarifu na mwingine,Hakuna kiingiliooo..
ELIJAH MTISHIBI_ -MCHUNGAJI WA KANISA LA FPCT BOKO KWA MPEMBA.
MR $ MRS PASTOR ELIJAH MTISHIBI Waki mwimbia Mungu Moja ya wimbo uliopo katika vitabu vya Nyimba za WOKOVU.

Wednesday, 6 January 2016

TAZAMA PICHA JINSI IBADA YA SIFA NA KUABUDU ILIVYOKUWA NZURI NDANI YA KANISA LA FPCT TEGETA-MACHINJIONI

Ibada ilifanyika tar 03/01/2016 ilikua ni ibada ya sifa na shukrani kwa Mungu kwa kuumaliza mwaka 2015 salama na kumtaka Mungu azidi kuwa nasi katika mwaka 2016. Ibada hii iliandaliwa kwa ushirikiano wa Makanisa mawili ya FPCT BOKO -KWA MPEMBA chini ya MCH ELIJAH MTISHIBI na kanisa la FPCT TEGETA-MACHINJIONI linalo chungwa na Mch J.J. NTASEHA.
Frank Gibebe akiongoaza wimbo wa sifa katika hali ya kuashilia uelekeo wa ushindi na kumtazama Bwana kwa mikono hiyo na watu wote wakimfuata kuamnini kwamba nguvu ya Mungu ipo .Ni kweli hiyo iikua ni moja ya step nzuri iliyokuwa kivutio kwa watu wengi walio kuwapo siku hiyo.
Hawa ni sehem ya waimbaji wa sauti ya pili wakiimba.

Mwl Gabilo Hosea akiongoza moja ya wimbo wa Kuabudu. Nyuma ni kundi zima la sifa na kuabudu.

Wa kwanza mbele kushoto ni mwimbaji Baraka Muna na kushoto ni Gabilo Hosea wakiimba kwa pamoja na kucheza . Kma unavyoona hapo mikono ilikuwa imeshikilia kiuno kwa ishara kwamba kwa Mungu hakuna jeuri.

Kijana John Gabriel/Saranda akiongoza wimba wa kuabudu. 

Kijana Gabriel akipiga drums kwa ubora wa hali ya juu saana. Huyu ni moja ya wapigaji waliowabariki watu wengi sana na kuwavutia sana kutokana na umriwake na upigaji wake wa hali ya juu sana, Kijana huyu ana umri wa mika 12 lakini anapiga drums mithili ya mtu mzima . 

Anaitwa Daniel. Lakini huwa jina lake maarufu ni DANY MA DRUMS. Huyu kijana ni moja ya wapiga drums maarufu sana ndani ya jiji la Dar es salam, alpiga pia siku hiyo kwa ubara na viwango vya hari ya juu sana. 



Wapigaji wa kitaa la Base na Solo naopia walikuwa wakimpigia Mungu kwa ubora wa hali ya juu sana,.