Monday, 29 June 2015

MSANII WA BONGO MOV STEVE NYERERE AJITOSA,ATANGAZA NIA YA UBUNGE

Ni siku kadhaa zimepita tangu msanii wa maigizo (bongo mov) Wema Sepetu aoneshe nia ya kutaka kuteuliwa na chma cha mapinduzi(ccm)kimptishe ili aweze kugombea ubunge katika jimbo la Singida mjini. Sasa hali hiyo imeamsha ari kwa msanii mwingine tena wa  tasnia hiyo ya maigizo(Bongo mov) Steven Mengele(Steve Nyerere) Amejitosa kutangaza nia kuptia chama cha mapinduzi (CCM) kiweze kumteuwa iliaweze kuipeperusha bendela ya chama hicho katika jimbo la Kinondoni. Msanii huyo ameamua kutangaza nia mwishoni mwa juma lililopita, wakati alipokuwa katika viwanja vya Bwawani Kinondoni akiongea na wananchi akiwahamasisha wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftali la kudumu la wapiga kura,
   Sambamba na hilo Msanii huyo Steven Mengele (Steven Nyerer)  alisema kuwa ikiwa atapewa ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto zinazo wakabili wananchi wa jimbo hilo la Kinondoni.
STEVE NYERERE  Akiwasili kwenye viwanja vya Bwawani kwaajili ya kuzungumza na wananchi
STEVE NYERER akipongezwa kwa uamuzi alio ufanya

 Pamoja na hayo alizitaja baadhi ya kero kuwa ni pamoja na miuondombinu mibovu,Uhaba wa maji,Masoko ya kudumu wamachinga na mama ntilie,Ajira kwa vijana nk. Pia aliwaomba wanachi wasisite kumchagua kwenye uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu, endapo chama chake kitamptisha.Hivyo aka sisitiza kuwa wananchi wa jimbo la Kinondoni wapaswa kuish maisha ya raha na Amani kwakutatuliwa matatizo yao. 

HUJAFA HUJAUMBIKA,OMBA YASIKUKUTE


Akizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na wandishi wa habari Bi GRACE KAIZA mkazi wa Igoma mjini Mwanza ambaye ameomba kusaidiwa na watu mbalimbali kutokana na tatizo alilonalo la mguu wake  kuugua ugonjwa wa kansa(saratani) unao msumbua kwa muda wa miaka kadha sasa tangu aupate ugonjwa huo. Anasema chanzo ilitokea uvimbe kama upele kidogo tu kwenye mguu wake, kadili kilivyo endelea kukua kipele ndivyo kiliendelea kuleta madhala  licha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa.  Amehangaika kwa muda mrefu akitafuta matibabu ya ugonjwa huo lakini hakuna mafanikio yoyote,hali inayo mlazim sasa kukatwa mguu wake huo.  Hivyo ameomba msaada kwa wadau na watu mbalimblali wajitokeze kumchangia pesa ili aweze kukatwa mguu wake na aweze kuunusuru uahai wake,.
Kwa yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaombwa kmsaidia kumchangia mchango kwa kuptia M pesa    
simu No - 0768 264 182

Sunday, 21 June 2015

MWIMBAJI MILCA KAKETE AZINDUA ALBAM MBILI MKUPUO NDANI YA VCCT CHURCH-MBEZI

Ilikua ni ibada maalum ya uzinduzi wa album mbili za mwimbaji wa kimataifa Milca Kakete uliofanyika katika kanisa la vcct Mbezi Dare es salaam Tanzania. Mwimbaji huyo alisindikizwa na waimbaji mbalimbali kama vile D.G.C. CHOUR,VOICE AKAPELA,MILIAM LUKINDO na wengine weengi,
  Ikumbukwe lengo la mwimbaji huyo Milca kufanya uzinduzi ni kutafuta pesa ambazo zitawasidia watumishi (wachungaji)wanaofanya kazi ya Mungu katika mazingira  magumu hasa wale wakao vijijini ili waweze kuwezeshwa katika nyanja mbalimbali za kihuduma, Ambapo kiasi kadhaa cha pesa kiliweza kupatikana ili kusapoti huduma hiyo, Pia mwimbaji huyo ametoa wito kwa watumishi na wadau wote wenye moyo wa kumtumikia Mungu wajitokeze kumuunga mkono ili waweze kuwasaidia watumishi wengine weengi zaidi kwa wakati mmoja,.


 Mchungaji Dr Huruma Nkone aliye shikilia mic,Mch Samwe(Katikati) na Mch Safari wate kwa Pmoja wakifanya maombi rasimi kwaajili ya kuziweka wakfu dvd za mwimbaji Milca Kakete ili ziweze kuanza kusikilizwa  na kufanyiwa changizo maalum.
 Mch Dr Huruma Nkone (kushoto) akiwa nana mkewake.

 Wakwanza kushoto ni mch Safari wa kanisa la D P C jijini Dar na Milca Kakete akiteta jambo na mmoja wa marafikizake wa karibu sana waliohudhulia ukumbini
 Mama yake mzazi wa Mwimbaji Milca Kakete aki mkumbatia mmoja ya wanafamilia baada ya kutoka jukwaani alipokua akitoa neno la shukrani kwa Mung,Huwezi aminin aliweza kudondosha chozi la furaha kwakitendo alicho kishuhudia,kwani ilikua ni moja ya maombiyake kwa Mungu ampatie japo hata mmoja ya watoto wake atakae weza kuwamrithi wake,kwani na yeye ni mwimbaji wa miaka mingisaana. Licha ya kuwa mzee sasa lakini Bado anamtumikia Mungu kwa Uimbaji.




 Mama yake mzazi wa Milca Kakete akitoa shuuda na shukrani.Aliye mshikia Mic ni Mch Samwel
 Mwimbaji Milca Kaketi akiwa katika hari ya utulivu akifuatili uimbaji.











Saturday, 20 June 2015

USIJIJIBUU.. NI SEMINA YA VIJANA ILIYOFANYIKA TAR 19/06/2015 KATIKA KANISA LA FPCT TEGETA MACHINJIONI,ANGALIA PICHA HAPAAA..

Ilikua ni siku ya pekee sana ambayo Mungu aliiandaa kwaajili ya kuwahudumia vijana walio hudhulia kwenye semina ya neno la Mungu iliyofanyika jana tar 19/06/2015 katika kanisa la fpct Tegeta- Machinjioni,
 Semina hiyo ilihudhuliwa na vijana kutoka makanisa mbalimbali,waliojitokeza kwa Wingi ili kujifunza neno la Mungu, Hakika Mungu alionekana kwa viwango vingine kabisa na  masomo  yalikua mazuri sana,ambayo yaliwafanya vijana kuuliza maswali mengi na mpaka kufikia wakati wa kukatisha muda wa maswali kwani mpka saa10alfajili bado maswli yalikua yakiulizwa.

    Kipekee sana mwalimu wa semina hiyo Mch ELIJAH MTISHIBI kutoka Tanzania alifundisha masomo mazuri sana na kufafanua kwa undani na kina maandiko katika Biblia huku akielezea mifano mbalimbali,hali iliyo amsha ari kubwa ya vijana kutamani semina iendelee mpka saa1 asubuhi.
Haya ni maombi maalum baada ya mafundisho ya semina

Kushoto ni Bw, Frank Gibebe mwkt wa idara ya vija akiwa mlezi wa Idara Mrs Mussa.

Bubujiko la maombi likiendeleaa vijana wakipata nguvu mpyaa ya maombi. 

Mwal wa semina Mch ELIJAH MTISHIBI akifanya  maombi maalum vijana waliohudhulia semina hiyo.


Mwalim wa semina Mch ELIJAH MTISHIBI mkononi akishilikia karatasi lilioandikwa maswali ya liyo kuwa yakiulizwa na baadhi ya vijana waliokuwa hawana ujasili wa kuuliza moja kwa moja'.

Baadhi ya vijana wakiendelea kumsikiliza mwalimu kwa makinisana na wengine wakiandika baadhi ya pointi mhimu/.

Mwalim wa somo Mch ELIJAH MTISHIBI akiimba wimbo wa kuabudu 

Moja ya kijana aliyeshindwa kujizuia baada ya nguvu ya Mungu kushuka katika maombezi maalum yalifayika kwenye simina hiyo na kuanza kumuita Mungu ili aweze kutenda kitu katika maisha mapya.
Sauti za vijana zikapazwa kwa Mungu

Sunday, 7 June 2015

HIVI NDIVYO SHEREHEYA UZINDUZI WA MATAWI MAPYA ILIVYO FANA

Hii ni katika ibada ya pili ya sherehe ya Uzinduzi wa matawi mawili mapya ya kanisa la FPCT- BOKO na FPCT BUNJU A, Sherehe hiyo imefanyika katika kanisa la FPCT TEGETA MACHINJIONI. Hakika Mungu ni mwema na mwaminifu katika maisha ya watuwake. Watu mbalimbali walihudhuria katika sherehe hiyo sambamba Mch Boazi Muyengo kutoka Bagamoyo aliye muwakilisha askofu mkuu wa  Jimbo la Fpct Kigoma Ask David Nkone ambaye hakuweza kuhudhuria sherehe hizo kutokana na sabababu zilizokuwa nje ya uwezowake.
Wakwanza kushoto ni Mch Boazi Muyengo akiwa na Mch J.J. Ntaseha mwenyeji wakiwa madhabahuni.
 Mchungaji ELIJAH MTISHIBI WA KANISA LA FPCT BOKO akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya tawi analo lichunga kwa sasa. Anasema kwa msaada wa Mungu anzidi kuwa ongeza kiidadi kutoka waumini 15 hadi 36 waliopo sasa tawi hilo lina muda wa miezi5tangu kuanzishwa,.
 Huu ulikuwa ni wakati wa Chakula watumishi wa Mungu kutoka Boko na Bunju kwa Pamoja wakipata chakula.
 Mzee kiongozi wa kanisa la FPCT TEGETA na mke wa mzee wa kanisa la fpct Madale Mrs Splian
                                  Mr and Mrs Splian wakipata chakula


 Waumini wakifuatilia kwa makini namna ya sherehe inavyo endelea Madhbahuni
 Mchungaji Boazi Muyengo akitoa ufafanuzi kidogo kabla ya kuzindiwa rasmi matawi hayo na kuwabariki walezi wa matawi hayo