Friday, 29 May 2015

SEMINA SEMINA....NI SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MAOMBEZI

KARIBU KWENYE SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MAOMBEZI KANISA LA FPCT BOKO KWA MPEMBA

kanisa la fpct Boko kwa mpemba jijini Dar es salaam wanakukaribisha kwenye semina ya Neno la Mungu N a maombezi inayoendelea kanisani hapo kila siku kuanzia saa 9:00 Jioni mpaka Saa 12 :30 jioni kumbuka semina hii ilianza siku ya Jana alhamisi tarehe 28 na itahitimishwa siku ya Jumapili Tarehe 31.5.2015 Kumbuka mtumishi wa Mungu wa kimataifa EV.JASTINE MWINGEREZA na Mchungaji mwenyeji Pastor Elijah Mtishibi wanafundisha neno L a Mungu pamoja na kufanya maombezi njoo ukutane na muujiza wako ....walete wagonjwa na wenye shida mbalimbali Bwana wa majeshi atawafungua kutoka katika vifungo vya ibilisi
                  EV Jastine Mwingereza akifundisha kwenye moja ya mikutano...huyu ndio mwl wa semina
                                               Ev. Jastine Mwingereza mwalimu wa semina
 Mch. Elijah Mtishibi .mchungaji mwenyeji kanisa la Fpct boko kwa mpemba

karibuni sana mpate chakula cha uzima mawasiliano jinsi ya kufika    0652200176

Saturday, 23 May 2015

ASANTE MUNGU KWA KUMPONYA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI NA MAWSILIANO KANISA LA FPCT TEGETA

Hapa akiwa mapokezi hosptalini lakini akijiskia vibayasana.
Mkurugenzi wa idara ya habari na mawasilino bwana FRANK C.  GIBEBE wakati akiwa nyumbani alikuawa na hali ya kawaida tu lakini haikuawa rahisi kuweza kuamini kilicho tokea mara baada ya muda mfupi alipofkishwa Hosptalini,  Ila Mungu ni mwemasana Amemponya sasa ni mzima kabisa wa Afya, alilazwa kwa muda wa saa24 wakatihuo kwa masaa 12 alikuwa hawezi hata kuongea,.  asantenisana kwa maombi yenu nyote mlio muombea Mungu awabarikisana.

Hpa akipewa uji kwa mara ya kwanza lakini alishindwa kunywa.

Akiwa amelala baada ya kufikishwa hosptalini

Akipewa uji kwa mala nyingine tena,kidogo alijitahidi kunywa vijiko kama 3 ivi nya uji

Akiwa ameshilikiwa na dada yake mkubwa Ferista Gibebe baada ya kulala kwa muda mrefu . 

Wednesday, 20 May 2015

ILIKUA BARAKA SANA SIKU HII YA WANAWAKE FPCT TEGETA,TAZAMA PICHA







                                       

SOMA HII JINSI MWASABWITE ALIVYO NUSURIKA KUTOBOLEWA MACHO.

Katika harakatizangu za kila siku,nilikua nyumbani kwenda kariakoo kufika kariakoo nikakuta foleni….ilikuwa kubwa sana magari hayatembei unaganda sehemu moja kwa muda mrefu sana na hii ni kutokana na matengenezo ya barabara.

 Nikiwa nimetulia sijui nitatoka vp ghafla nikamuona mtu mbele kushoto kwangu ananiambia rudi  nyuma kidogo usije ukagonga daladala nikarudi nyuma.. Akanisogelea kwa dirishani na kuanza kuniambia tumekufuatilia sana tulitaka tukuibie.
 Nilikuwa nimeshusha vioo kidogo hewa ingie akaniambia kwa vile unaonekana mtu unaemsikiliza kila mtu hatuwezi kukuibia ila usirudie kuacha vioo vya gari wazi, akajieleza kama mtu mwema kumbe bado ana nia ya kuniibia akaniambia nikuonyeshe mfano jinsi mtu anaweza kufungua mlango  na ile hali tu  kioo kikiwa wazi akapenyesha mkono akatoa lok akafungua mlango wa gari huku nikiwa nimepigwa na butwaa nashangaa akaingia akakaa siti ya mbele akaniambia umeona nilivyoingia akaniambia naomba buku nikampa akaniomba elfu kumi nikamwambia sina akanitolea kisu huku akinitishia kunitoboa macho
''Ali niambia kati ya macho na pesa unapendakipi? ni kajibu macho akaniambia sawa pesa utazitafta lakini macho hauta yapata" akachukua pesa zote kwenye walet, alikuwa anachukua kwa kutoa mifano namshukuru Mungu hakunidhuru aliniachia simu akashuka. 

Jamani wenye magari unaposimama na gari yako kwenye foleni funga vioo kwani si bora kuacha vii wazi ni vizuri kuwa makini. Ni heri kuchoma mafuta ili uwashe kiyoyozi kuliko kuacha vioo wazi. (coted from to Mwasabwite facebook acoount Shukrani sana)

Thursday, 14 May 2015

NJOO USHIRIKI BARAKA NA MY VICTORY FAMILY OF GOD

Watu wote kabila zote ,Dini zote mnakaribishwa sana kwenye Tamasha la MY VICTORY FAMILY OF GOD Lengo la tamasha hili ni changizo la pesa kwa ajili ya kukamilisha video yao ambayo iko katika hatua za mwisho

Tamasha hili litafanyika jumapili ya wiki hii Tarehe 17/05/2015 saa 8:00 mchana  hadi saa 12 :30 jioni katika kanisa la Pentecoste Power Ministry ..kanisa hili liko barabara la Tegeta ya kwenda Wazo hill kama mita 200 ....Kanisa liko ndani ya fance maarufu kwa Mkabogo au [pastor Rungu]

Kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi watakuwepo .HAKUNA KIINGILIO NI BURE

                                          NYOTE MNAKARIBISHWA

mawasiliano ni 0712533001




Wednesday, 13 May 2015

TAZAMA PICHA NAMNA JUMAPILI YA BARAKA NA MGUSO WA KIPEKEE SEASON 2 ILIVYOKUWA

Hakika MUNGU ni mwema jumapili ya tarehe 10.5.2015 kulikuwa na ibada maalum ya sifa na kuabudu katika kanisa la fpct tegeta ijulikanayo kama JUMAPILI YA BARAKA NA MGUSO WA KIPEKEE SEASON 2, kweli Mungu anaketi katika sifa ....hebu endelea kutazama picha za matukio siku hiyo















Friday, 8 May 2015

MAANDALIZI JUMAPILI YA MGUSO SEASON 2 YAKO HATUA ZA MWISHO

 Kamati ya maandalizi,tamasha na sherehe katika kanisa la fpct tegeta jijini Dar es salaam imesema tayari maandalizi ya ibada ya sifa na kuabudu ijulikanayo kama Jumapili ya baraka na Mguso wa kipekee Season 2 yamekamilika kwa asilimia 80 huku na asilimia 20 zilizobakia ni maandalizi madogodogo.

  Akizungumza na Blog hii Katibu wa Kamati Exauds Wiston Alisema tayari wamefanikiwa kwenye hatua kubwa upande wa maandalizi hasa upande wa waimbaji ambapo tayari mwimbaji kutoka USA Fidel Murwa tayari ameshawasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma siku hiyo,na mwimbaji mwingine kutoka kenya Denis Lisoni atawasili nchini siku ya kesho majira ya Saa nane mchana.

 Exauds Alisema waimbaji wengine kutoka Tanzania kama Gabilo Hosea na Kepha Jackson tayari wako kwenye maandalizi kuelekea siku hiyo,huku Nuru kwaya,jerusalem kwaya,The hope singers,na The best of Jesus choir ni miongoni mwa kwaya zitakazohudumu katika siku hiyo.

 Aidha kiongozi huyo alisema kikundi cha sifa na kuabudu kutoka kanisa la fpct tegeta kiko tayari kwa huduma siku hiyo huku akiwaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kwenye ibada hiyo ya sifa na kuabudu kwani Mungu wa majeshi atakutana na uhitaji wa kila mmoja