MKESHA MKUBWA WA VIJANA PRISHI YA TEGETA KANISA LA FPCT
idara ya vijana kanisa la fpct parishi ya tegeta wameeandaa mkesha mkubwa wa vijana ambao utawakutanisha vijana wote wa jiji la Dar es salaam kumuabudu Mungu na kulitukuza jina la jehova shama katika mkesha huo
baadhi ya vijana wa kanisa la fpct tegeta
kwaya ya jerusalemu kutoka tageta watatoa huduma siku hiyo
Akizungumza na fpct tegeta blog mwenyekiti wa idara ya vijana kanisa la fpct parishi ya tegeta bwana Frank Gibebe amesema mkesha huo utafanyika katika kanisa la fpct madale jijini Dar es salaam siku ya ijumaa tarehe 31/10/2014 kuanzia saa mbili za usiku mpaka saa kumi na mbili alfajili ambapo amesema lengo la kufanya mkesha huo ni kutaka kuwakutanisha vijana kutoka makanisa tofauti na kujumuika pamoja kuliadhimisha jina la bwana yesu
Gibebe amesema katika mkesha huo watakuwa na maombi ya kuliombea taifa la Tanzania na mchakato mzima wa katiba mpya pamoja na kuwaombea viongozi wa taifa huku akidai kuwa watafanya maombi maalum kuwaombea viongozi wapya wa kanisa la fpct kitaifa pamoja na kuombea mahitaji mbali mbali ya vijana katika nyanja mbalimbali.
Aidha kiongozi huyo amesema idara hiyo imearika kwaya mbali mbali pamoja na waimbaji binafsi ambao watatoa huduma katika mkesha huo na kuongeza kuwa vijana wameandaa michezo mbalimbali kama maigizo ,vichekesho na ngonjera kwa lengo la kuhakikisha mkesha huo unakuwa wa tofauti na wa aina yake.
Frank Gibebe mwenyekit idara ya vijana kanisa la fpct parish ya tegeta
Hata hivyo amewaomba vijana kutoka maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam kuhudhuria katika mkesha huo huku akisema itakuwa siku ya kipekee na ya tofauti kwa sababu tunataka kutumia nguvu Mungu alizotupa sisi kama vijana kupambana na ibilisi na kuvunja ngome zote za shetani katika nchi yetu ya Tanzania hivyo naomba vijana wajitokeze kwa wingi na Mungu wa mbinguni atawabariki