Friday, 22 January 2016

IKIWA BWANA AMETENDA KWANINI TUSIMSHUKURU?

Hili ndilo swali unaweza ukajiuliza sana mala kwa mala pale tu unapokumbuka BWANA alichokifanya katika maisha yako. Lakini pia wapo watu wengi ambao wanasahau sana mambo makubwa Ambayo BWANA mefafanya katika maisha yao.

Sasa basi kwakulijua hilo kwamba Mungu anapswa kushukuliwa kwakila jambo na hatua tuna vuka,Kanisa la FPCT BOKO Kwa ushrika Mkubwa wa kanisa la FPCT TEGETA-Machinjioni,wameandaa ibada kubwa ya sifa na Shukrani kwaajili ya kumshukuru Mungu kwakujibu Mahitaji yao meengi lakini kubwa likiwa ni kwamba Mungu amewawezesha kanisa la FPCT BOKO kwa Mpemba lilipo chini ya Mchungaji ELIJAH MTISHIBI kupata Vyombo vizuri vya na vya kisasa vya muziki..
 
Ibada hiyo itafanyika tar 31/01/2016.Kuanzia saa8:00mchana katika Kanisa la FPCT Boko kwa Mpemba. Wimbaji mbalimbali watakuwepo kumtukuza Mungu kama :- Nuru kwaya,Jerusalem kwaya, Esther Band Kutoka Gongo la Mboto,Kefas Jacksoni, na wengine wengi.

Usikoseeee!!,. Mtaarifu na mwingine,Hakuna kiingiliooo..
ELIJAH MTISHIBI_ -MCHUNGAJI WA KANISA LA FPCT BOKO KWA MPEMBA.
MR $ MRS PASTOR ELIJAH MTISHIBI Waki mwimbia Mungu Moja ya wimbo uliopo katika vitabu vya Nyimba za WOKOVU.

Wednesday, 6 January 2016

TAZAMA PICHA JINSI IBADA YA SIFA NA KUABUDU ILIVYOKUWA NZURI NDANI YA KANISA LA FPCT TEGETA-MACHINJIONI

Ibada ilifanyika tar 03/01/2016 ilikua ni ibada ya sifa na shukrani kwa Mungu kwa kuumaliza mwaka 2015 salama na kumtaka Mungu azidi kuwa nasi katika mwaka 2016. Ibada hii iliandaliwa kwa ushirikiano wa Makanisa mawili ya FPCT BOKO -KWA MPEMBA chini ya MCH ELIJAH MTISHIBI na kanisa la FPCT TEGETA-MACHINJIONI linalo chungwa na Mch J.J. NTASEHA.
Frank Gibebe akiongoaza wimbo wa sifa katika hali ya kuashilia uelekeo wa ushindi na kumtazama Bwana kwa mikono hiyo na watu wote wakimfuata kuamnini kwamba nguvu ya Mungu ipo .Ni kweli hiyo iikua ni moja ya step nzuri iliyokuwa kivutio kwa watu wengi walio kuwapo siku hiyo.
Hawa ni sehem ya waimbaji wa sauti ya pili wakiimba.

Mwl Gabilo Hosea akiongoza moja ya wimbo wa Kuabudu. Nyuma ni kundi zima la sifa na kuabudu.

Wa kwanza mbele kushoto ni mwimbaji Baraka Muna na kushoto ni Gabilo Hosea wakiimba kwa pamoja na kucheza . Kma unavyoona hapo mikono ilikuwa imeshikilia kiuno kwa ishara kwamba kwa Mungu hakuna jeuri.

Kijana John Gabriel/Saranda akiongoza wimba wa kuabudu. 

Kijana Gabriel akipiga drums kwa ubora wa hali ya juu saana. Huyu ni moja ya wapigaji waliowabariki watu wengi sana na kuwavutia sana kutokana na umriwake na upigaji wake wa hali ya juu sana, Kijana huyu ana umri wa mika 12 lakini anapiga drums mithili ya mtu mzima . 

Anaitwa Daniel. Lakini huwa jina lake maarufu ni DANY MA DRUMS. Huyu kijana ni moja ya wapiga drums maarufu sana ndani ya jiji la Dar es salam, alpiga pia siku hiyo kwa ubara na viwango vya hari ya juu sana. 



Wapigaji wa kitaa la Base na Solo naopia walikuwa wakimpigia Mungu kwa ubora wa hali ya juu sana,. 




Wednesday, 16 December 2015

HIVI NDIVYO SIKUKUU YA WATOTO ILIVYO NOGASANA KATIKA KANISA LA FPCT TEGETE

Ni dhahiri shairi kwamba wakipewa nafasi wanaweza na wanadhihirisha kuwa wao ni tegemeo la baadae. Hii ni sikukuu ya watoto iliyofanyika jumapili ya tar 13/12/2015 katika kanisa la fpct Tegeta-Machinjioni ambapo waliungana na watotot wengine Tanzania katika kusherehekea sikukuu hiyoo..
 
     Watoto kwakushrikiana na walimu wao waliandaa mambo mengisana ,kwanza sikukuu hiyo ilitanguiwa na Kongamano kubwa la watoto kutoka matawi yote yanayounda parishi ya Tegeta zaidi ya watoto 150 walihudhuria. Katika kongamano hilo walijifunza masomo mbalimbali ya kiroho na kimwili pamoja na kufanya mazoezi ya viungo vya mwili na kutembelea sehem ya kuhifadhia wanyama iitwayo Tegeta Zoo..

       Mwisho hitimisho la sherehe hiyo ilifanyika jumapili iliyopita kwakuhudhuliwa na watu mbalimbali,wazazi,walezi,ndugujamaa na marafiki na hudhuliwa na mgeni rasm ambapo katika sherehe hiyo kiasi cha zaidi ya Tsh laki sita{600,000} ziliweza kupatikana kwaajili ya kununulia TV Cinema na vifaa vya kfundishia kama ilivyokua ombi lao katika Riasara waliyo msomea Mgeeni Rasm, Mgeni rasm katika sikukuu hiyo alikuwa ni ndg FRANCIS MWAKABANJE,lakini aliwakilishwa na Mch RUNGU kwa niaba,..
Mwakilishi wa mgeni Rasm katika sikukuu ya watotot. Mch Rungu.

Sehem ya watoto waliohudhulia sikukuu yao

Moja ya watoto wakifuatilia matukio mbalimbali katika sherehe yao.

Kwaya ya watotot wakiwa madhabahauni wakiimba.


Mtoto Debora Kimali akigongea moja ya wimbo ulikua ukiimbwa kwenya sikikuu yao.

Sehem ya wageni walialikwa katika sikukuu ya watototo

Mchungaji wa Knisa la FPCT TEGETA MCH JORAM J. NTASEHA

Mchungaji J. J NTASEHA [wa kwanza kushoto] akiwa na mgeni rasm. 

Good News Team wakihudum. 

Mtoto Rachel Yohana ambaye alipta fusla ya kusherehekea sikuyake ya kuzaliwa katika sikukuu ya watoto ambapo alikua akiadhimisha miaka kadhaa.

Hii ni sehem ya waigizaji wakiigiza 

Watoto wakiigiza igizo la Msamalia mwema.

Watoto wakisoma risara kwa mgeni rasm

Mtoto Prosper akionesha ushujaa wake kwakupiga push up kwa mkono mmoja.

Sehem ya wazazi wakishuhudia matukioo

Kiongozi wa ibada Yohana Mussa


Moja ya watoto wakiigiza
Huyu ni moja ya mtoto akijiandaa kuruka srakasi,kama sehem ya kuonesha kipaji chake...




Picha kwa hisani ya fpcttegeta.blogspot.com

Monday, 2 November 2015

NI ZAIDI YA MGUSO KATIKA TAMASHA LA SIFA NA KUABUDU -FPCT TEGETA

Kwa wale walio hudhulia tamasha la sifa na kuabudu siku ya jumapili ya tar 01/11/2015 lililofanyika ndani ya kanisa la FPCT TEGETA -MACHINJIONI unaweza kuungamkono maneno hayo kwamba Roho wa Mungu aliwagusa watu wake isivyo vya kawaida,nguvu ya Mungu ilishuka na kuwahudumia wale waliokua tayali kumpkea..
  Tamasha hilo lili andaliwa kwa ushirikiano wa makanisa mawaili ya FPCT TEGETA MACHINJIONI NA FPCT BOKO -KWA MPEMBA.na kuwashilikisha watu na wadau mbalimbali lilikua la kipekee na laaina yake ambapo lilikua lilisikika moja kwa moja kwanjia ya radio mtandaoni{POWER OF JESUS RADIO FM} Watu kutoka ndani na nje ya nchi waliweza kushiriki kwakuptia mtandao..
  Akizungumza na Mwandishi wetu Mwkt wa Mandalizi ya matamasha mbalimbali hapo kanisani Bwan FRANK GIBEBE alisema kuwa tamsha hilo limetoa mwanga wa kuandaa matamasha mengine ambapo alisema jumapili ya pili inayokuja kutakua na tamsha lingine kama hilo litakalo fanyika katika kanisa la FPCT BOKO Kwa Mpemba.Awali alianza kwakumshuru Mungu kwakaziyote aliyofanyika na kutoawito kwa watu wote wajiandae kuhudhulia siku hiyo..


Kundi la sifa na kuabudu wakiwa katika picha ya pamoja na mchungaji wa kanisa la FPCT BOKO Mch  ELIJAH MTISHIBI (katikati aliye vaa mavazi meupe)





Friday, 30 October 2015

BAADA YA UCHAGUZI NI MUDA WA KUJA KUMSHUKURU MUNGU ...HII SI YA KUKOSA

TAMASHA TAMASHA TAMASHA NI TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU LITAKALOFANYIKA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 1.11 .2015 KUANZIA SAA 9:00 Alasiri mpaka saa 12 :00 jioni NI KATIKA Kanisa La FPCT Tegeta waimbaji mbalimbali watakuwepo, Fpct tegeta praise &worship watahudumu itakuwa zaidi ya baraka ...KARIBUNI SANA  Mawasiliano ni 0768061291 au 0752040012